Kwa nini serikali haitumii maoni na ushauri wa kitaalamu?

Mar 28, 2011
11
0
Jamani wana wa jamii forums naomba kupata mchango wenu juu ya hili. Mara nyingi sana nimekuwa nikifuatilia utekelezaji unaofanywa na serikali kufuatia ripoti za tafiti mbalimbali kuhusu ufumbuzi wa matatizo yanayokwaza maendeleo ya taifa katika nyanja tofauti. Lakini kwa hakika kinachoendelea ni kwa serikali kufumbia macho na kuziba kabisa masikio hasa pale panapokuwa na mapendekezo yenye masilahi kwa taifa. Ndo kusema viongozi hawalitakii mema taifa au labda kuna jinsi wanavyofaidika na matatizo yanayolikabili taifa?
 
Mkuu, ukiona mtu mzima kama kiongozi wa Taifa anapuuza ushauri wa kitaalamu basi ujue kuna agenda chafu nyuma yake. Viongozi wengi wamekuwa na tabia hiyo, na isitoshe wanaonufaika na maamuzi yao ni kundi dogo sana, natumaini tukiandika katiba mpya na kuweka vipengele ambavyo vitawabana kwa masuala kama hayo tutafanikiwa.
 
Back
Top Bottom