KWA NINI NI VIKOBA NA SI MKURABITA?

KWA NINI NI VIKOBA NA SI MKURABITA?

Rwegasiram

Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
7
Reaction score
2
Mwaka 2004/5 serikali ya Tanzania, iliasisi Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) lengo likiwa ni kuwezesha wananchi wanyonge kutumia raslimali na biashara zilizorasmishwa kupata mikopo kutoka benki na taasisi nyingine za kifedha. Kwa bahati mbaya, hali halisi inaonyesha kuwa MKURABITA haujawa kimbilio la wanyonge kupata huduma ya mikopo. Badala yake wananchi wamebuni mifumo mbadala kama vile VICOBA, VSLA na "michezo" ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kuwawezesha kupata huduma ya kifedha. Kwa nini wananchi wengi wananufaika kupitia VICOBA, VSLA, UPATU na "michezo" badala ya MKURABITA?
 
Back
Top Bottom