Nini kifanyike? Jibu lao ni hili. Kuwe na miti ya kuchuma pesa ili kila demu awe anamiliki gari kwa jasho lake mwenyewe, yaani kadri anavyochuma hizo pesa ndipo uwezo wa kununua gari alitakalo utamruhusu. Kwa kweli kwa hapa Bongo kwa sasa hakuna mapenzi bali ni Bongo majanga/movie. Kila mtu ni msanii wa mapenzi, utakuta unachumbia demu lakini bado tu analiwa nje na wauza unga hoping kwamba atapata jamaa mwenye uwezo zaidi shinda wewe ili aonekane kwa wenziwe kuwa kapata. Inasikitisha.