Kwa nini mtu anaitwa Profesa hata kama hafundishi?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hii inatokea Tanzania kwetu tu, kwamba mtu hafundishi na wengine hata ana miaka 10 hajawahi kukanyaga Chuoni lkn anaitwa Profesa, sasa kwa nini?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hii inatokea Tanzania kwetu tu, kwamba mtu hafundishi na wengine hata ana miaka 10 hajawahi kukanyaga Chuoni lkn anaitwa Profesa, sasa kwa nini?
Ngoja nim tagi wakili msomi, nguli ambaye nina mwamini kwa kila jambo labda anaweza kutoa mchango wake maridhawa kwenye huu uzi: Petro E. Mselewa
 
Haaaaaa, kwani prof lazma ufundishe? Hiyo ni elimu sawa na zingine. Mfn unaweza kua mwl, daktari wa binadamu, wanyama, baada ya elimu hiyo usiitumikie lakini hiyo haiondoi ww usiitwe jina la taaluma yako.
 
Profesa sio kufundisha peke yake.. Angalau kibongobongo ndo tulivyozoea..! Uprofesa huja kutokana na tafiti zako, vitabu vyako pamoja na makala zako ulizoandika ndizo zinazokupa points za kupanda..!

Sasa shida inakuja watu wengi hujiita maprofesa kwa vile jina lake linapendezea.. Or wengine ni kutokana na mchango wake ambao haupo rasmi.. Mfano ... na ....
 
Professor ni kiwango cha juu cha kitaaluma Aidha unafundisha colleges/university au unafanya tafiti katika taluuma yako na jopo la maproffesa likiridhia unapewa u-proffesor.

Sasa ukishapewa unaitwa tu. Kitakachotengua jina lako aidha ugundulike ulicheat kuupata u-proffesor. Ndiyo maana unaona shivji hafundishi lakini bado ni prof. N.k.

Au mkuu wewe nani kakuuma kuona hafundishi ila bado anaitwa prof??
 
Ngoja nim tagi wakili msomi, nguli ambaye nina mwamini kwa kila jambo labda anaweza kutoa mchango wake maridhawa kwenye huu uzi: Petro E. Mselewa
Mkuu,nashukuru kwa kuniita hapa. Labda niseme mwanzo mwanzoni kuwa kuna majina ya aina mbili. Kuna majina halisi na majina bandia/ya umaarufu. Ndiyo kusema, kuna Prof./Dr. kwa uhalisia na yule aliyepachikwa au kujipachika mwenyewe. Prof.halisi ni yule mwenye Shahada ya Uzamivu na aliyefundisha chuo kikuu na kuandika maandiko mbalimbali ya kitaaluma na kupata alama za kumpandisha kufikia ngazi hiyo.

Lipo jambo la kuzingatia kwa Madokta. Wahitimu wote wa shahada za Uuguzi mfano MD, huitwa Madokta. Ijapokuwa, Wapo kati yao wenye Ph.D na hata Maprofesa.Kimsingi, Prof. ni cheo cha kitaaluma kama alivyo Askofu au Kadinali kwenye dini ya kikatoliki. Maprofesa wote ni lazima kwanza wawe Madaktari (wawe na Ph.D) kama walivyo Maaskofu na Makadinali wote lazima wawe Mapadre. Lakini, wapo wanataaluma ambao walikuwa Maprofesa hata kabla ya kupata Ph.D. Mfano mmojawapo ni Prof. Gamalieli Mgongo-Fimbo, Profesa wa Sheria,UDSM.

Maprofesa pia wamegawanyika katika Maprofesa Washiriki (Associate Professors) na Maprofesa 'Kamili' (Professors) kulingana na uandishi niliousema na utafiti wanaoendelea kuufanya kitaaluma. Kwakuwa mleta mada amejaribu kuhoji kibinafsi, amtaje/awataje wanaoitwa Maprofesa halafu tuchambue namna walivyoupata huo uprofesa wao.
 
Professor ni kiwango cha juu cha kitaaluma Aidha unafundisha colleges/university au unafanya tafiti katika taluuma yako na jopo la maproffesa likiridhia unapewa u-proffesor.

Sasa ukishapewa unaitwa tu. Kitakachotengua jina lako aidha ugundulike ulicheat kuupata u-proffesor. Ndiyo maana unaona shivji hafundishi lakini bado ni prof. N.k.

Au mkuu wewe nani kakuuma kuona hafundishi ila bado anaitwa prof??

Huu mfumo tumeuiga wapi? Kwa maana sijawahi kusikia kwa Wazungu hata kwenye vyombo habari mtu akisema Profesa Einstein au sijui Profesa Stephen Hawkins, huitwa tu Profesa Hawkins pale ambapo yuko Chuo Kikuu lkn nje ya hapo hakuna anayetumia neno Profesa, sasa sisi mfumo wetu umetokea wapi?
 
Labda ujue Chanzo na maana ya profesa... Hili ni neno lililotokana na neno la kihispaniola le profeseri... Ni kweli neno hili Lina maana ya moja kwa moja kuwa ni mwalimu kwa Spanish. Lakini Lina maana ya yeyote anayejua kitu anachoweza kumuelimisha mwingine. Kwa maana nyingine hapa Mimi ni le profeseri wako.
 
Mkuu,nashukuru kwa kuniita hapa. Labda niseme mwanzo mwanzoni kuwa kuna majina ya aina mbili. Kuna majina halisi na majina bandia/ya umaarufu. Ndiyo kusema, kuna Prof./Dr. kwa uhalisia na yule aliyepachikwa au kujipachika mwenyewe. Prof.halisi ni yule mwenye Shahada ya Uzamivu na aliyefundisha chuo kikuu na kuandika maandiko mbalimbali ya kitaaluma na kupata alama za kumpandisha kufikia ngazi hiyo.

Lipo jambo la kuzingatiia kwa Madokta. Wahitimu wote wa shahada za Uuguzi mfano MD, huitwa Madokta. Ijapokuwa, Wapo kati yao wenye Ph.D na hata Maprofesa.Kimsingi, Prof. ni cheo cha kitaaluma kama alivyo Askofu au Kadinali kwenye dini ya kikatoliki. Maprofesa wote ni lazima kwanza wawe Madaktari (wawe na Ph.D) kama walivyo Maaskofu na Makadinali wote lazima wawe Mapadre. Lakini, wapo wanataaluma ambao walikuwa Maprofesa hata kabla ya kupata Ph.D. Mfano mmojawapo ni Prof. Gamalieli Mgongo-Fimbo, Profesa wa Sheria,UDSM.

Maprofesa pia wamegawanyika katika Maprofesa Washiriki (Associate Professors) na Maprofesa 'Kamili' (Professors) kulingana na uandishi niliousema na utafiti wanaoendelea kuufanya kitaaluma. Kwakuwa mleta mada amejaribu kuhoja kibinafsi, amtaje/awataje wanaoitwa Maprofesa halafu tuchambue namna walivyoupata huo uprofesa wao.

Kwanini hakuna anayesema Profesa Einstein? Au Profesa Obama?
 
Mkuu,nashukuru kwa kuniita hapa. Labda niseme mwanzo mwanzoni kuwa kuna majina ya aina mbili. Kuna majina halisi na majina bandia/ya umaarufu. Ndiyo kusema, kuna Prof./Dr. kwa uhalisia na yule aliyepachikwa au kujipachika mwenyewe. Prof.halisi ni yule mwenye Shahada ya Uzamivu na aliyefundisha chuo kikuu na kuandika maandiko mbalimbali ya kitaaluma na kupata alama za kumpandisha kufikia ngazi hiyo.

Lipo jambo la kuzingatiia kwa Madokta. Wahitimu wote wa shahada za Uuguzi mfano MD, huitwa Madokta. Ijapokuwa, Wapo kati yao wenye Ph.D na hata Maprofesa.Kimsingi, Prof. ni cheo cha kitaaluma kama alivyo Askofu au Kadinali kwenye dini ya kikatoliki. Maprofesa wote ni lazima kwanza wawe Madaktari (wawe na Ph.D) kama walivyo Maaskofu na Makadinali wote lazima wawe Mapadre. Lakini, wapo wanataaluma ambao walikuwa Maprofesa hata kabla ya kupata Ph.D. Mfano mmojawapo ni Prof. Gamalieli Mgongo-Fimbo, Profesa wa Sheria,UDSM.

Maprofesa pia wamegawanyika katika Maprofesa Washiriki (Associate Professors) na Maprofesa 'Kamili' (Professors) kulingana na uandishi niliousema na utafiti wanaoendelea kuufanya kitaaluma. Kwakuwa mleta mada amejaribu kuhoji kibinafsi, amtaje/awataje wanaoitwa Maprofesa halafu tuchambue namna walivyoupata huo uprofesa wao.
Home of the great thinker.....
 
Huu mfumo tumeuiga wapi? Kwa maana sijawahi kusikia kwa Wazungu hata kwenye vyombo habari mtu akisema Profesa Einstein au sijui Profesa Stephen Hawkins, huitwa tu Profesa Hawkins pale ambapo yuko Chuo Kikuu lkn nje ya hapo hakuna anayetumia neno Profesa, sasa sisi mfumo wetu umetokea wapi?
Albeit eist. Alikuwa professor usiende mbali tu nenda Google jamaa kwa tafiti zake alikuwa qualified prof. Sema katika docs zake alikuwa hajiiti ila alijulikana kama professor.

Sisi tunafuata mfumo wa British na kama unavyojua tupo common wealth.
 
Back
Top Bottom