Kwa nini makanisa yenye wafuasi wengi ni Yale ambayo BIBLIA sio Kipaumbele?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Historia ya hizi imani inaonyesha enzi za ujima wakidini ni wakati ambapo waumini walizuiwa kusoma na kutafsiri neno kwa akili zao, hiyo kazi ilikuwa ikifanywa na kiongozi tu..

Miaka ya hivi karibuni, naona kama dini zinarudishwa ujimani tena. Ni Nadra sana kukutana na muislam ambaye anajisomea mushaf. Huku ukristoni zikiimbwa nyimbo wote wanasisimka likisomwa neno watu wanalala. Anachokisema aliyesimama kwenye madabahu ndio sheria Bila kujali Lina msingi kwenye neno au ni porojo zake.

Ni kawaida Sasa kukuta kanisa limejaza hadi barabarani watu waliokuja kuhadithiwa vitu ambavyo vimo kwenye vitabu mikononi mwao lkn hawavisomi.

Kataa kurudi kwenye dini za kijima na kusomewa. Soma bibilia muislam soma msaafu haaminiki mtu dunia imeharibika hii wakuu.
 
Wanao soma Biblia/Quran Ni wengi lakini wanao elewa Ni wachache Sana tena Sana Na lazima wawe wateule. Wengi wanasoma ukiwemo wewe mtoa mada lakini hawaelewi Na Ni wakali kweli kukiri kuwa hawaelewi, ndio maana Mungu aliwaleta wateule wachache waje kuwaelimisha wengi ambao hata wangekesha Na kulala Na Biblia/Quran Kama mito bado hawata elewa isipokuwa kupitia kwa wateule wachache watakao wafundisha maandiko yanamaanisha nini
 
Muislamu kutokusoma Quran ni kughafilika kwake, ila hakuna ibada wala mazungumzo ya kiislam yanayofundishwa nje ya Quran ama Sunnah za mtume
Kusikiliza na kusoma mkuu kunatofauti kubwa. Tunasoma kuthibitisha kama yanayosemwa ndio yaliyoandikwa na kuyahifadhi kichwani. Kusikiliza ni 20%. Tusome hivi vitabu mkuu na kuyaweka kichwani sio kusomewa...

Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yoshua 1:7-
 
Kingine watu wanataka sana kuona miujiza ktk maisha yao ikitendwa,kijana kazi hafanyi anategemea kwenda kwa mchungaji fulani apate gari nzuri,nyumba nzuri mke mwema etc huku hayaangalii maisha yake anayoishi kama anampendeza Mungu au la,Biblia Takatifu inatuasa kufanya kazi kwa bidii na kumtolea Mungu yaliyokuwa ya haki ndo tutafanikiwa{pamoja na kutoa ktk nyumba za Ibada,kusaidia wasiojiweza nako ni Ibada,mtu anaambiwa na mchungaji fulani toa laki kesho utapata mill anatoa,anasahau alipokuwa anaelekea hapo kanisani kuna maskini kalala njaa jana alimuomba japo 500 akanunue unga akakoroge uji apoze njaa na hakumpa,utoe hata 100mill hutokaa ufanikiwe coz hufanyi kile ulichoelekezwa}mtu sheria za Mungu zimeandikwa kwenye Bible sio kuziishi tu hata kuzitamka hajui.wanawake nao wanategemea miujiza iwaokoe waolewe wanasahau kwamba mavazi wanayovaa yanawakimbiza waowaji, wengine Mungu alipowapa watu sahihi kwao kwa sababu ya kutokumcha Mungu waliwakataa eti kisa hawana pesa,wafupi sijui sura zao haziendani nao alimradi vurugu sasa wanaona menopause inaingia wanamkimbilia Mungu na tena sio wao kusali kujiombea unakuta wanamtegemea mtu awawekee mikono ili wafanikiwe.
 
Wanao soma Biblia/Quran Ni wengi lakini wanao elewa Ni wachache Sana tena Sana Na lazima wawe wateule. Wengi wanasoma ukiwemo wewe mtoa mada lakini hawaelewi Na Ni wakali kweli kukiri kuwa hawaelewi, ndio maana Mungu aliwaleta wateule wachache waje kuwaelimisha wengi ambao hata wangekesha Na kulala Na Biblia/Quran Kama mito bado hawata elewa isipokuwa kupitia kwa wateule wachache watakao wafundisha maandiko yanamaanisha nini
hizi ni lugha za kitapeli zinazotumika kuwafanya watu wawe watumwa wa wanadamu wenzao.
"Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisikutende ubaya"zaburi 119:11---> Sio nimewekewa na religious elites

Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonika. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli.
Matendo ya mitume 17:11

Ni utapeli kuwaambia watu hawawezi kuelewa neno. Chochote anachokisema mtumishi lazima kihakikiwe kama ni cha kweli.

Kwa waislamu - Quran maana yake ni kuyaweka kichwani/Moyoni maneno ya Mushaf/Msaafu.

Watu wakiwaweka maneno ya vitabu kichwani/moyoni/akilini wanakuwa na true religious freedom
 
Mkuu umesema ukweli mtupu,halafu hawa ambao hata biblia hawasomi ni wabishi kuliko!!Na wanaamini kila wanachoambiwa ni kweli maana hutoka usingizingizini wakiota magari na magorofa.
Ukiona mtu anarusha ngumi au tusi kwa sababu ya dini awe muislamu au mkristo ni ishara ya utupu wa neno kichwani mkuu.
 
Hata Biblia inasema,mmoja asome na afundishe wengine..! Mkisoma wote, nani atamfundisha mwenzake, ndio mwanzo wa ubishi huo...!
 
Kingine watu wanataka sana kuona miujiza ktk maisha yao ikitendwa,kijana kazi hafanyi anategemea kwenda kwa mchungaji fulani apate gari nzuri,nyumba nzuri mke mwema etc huku hayaangalii maisha yake anayoishi kama anampendeza Mungu au la,Biblia Takatifu inatuasa kufanya kazi kwa bidii na kumtolea Mungu yaliyokuwa ya haki ndo tutafanikiwa{pamoja na kutoa ktk nyumba za Ibada,kusaidia wasiojiweza nako ni Ibada,mtu anaambiwa na mchungaji fulani toa laki kesho utapata mill anatoa,anasahau alipokuwa anaelekea hapo kanisani kuna maskini kalala njaa jana alimuomba japo 500 akanunue unga akakoroge uji apoze njaa na hakumpa,utoe hata 100mill hutokaa ufanikiwe coz hufanyi kile ulichoelekezwa}mtu sheria za Mungu zimeandikwa kwenye Bible sio kuziishi tu hata kuzitamka hajui.wanawake nao wanategemea miujiza iwaokoe waolewe wanasahau kwamba mavazi wanayovaa yanawakimbiza waowaji, wengine Mungu alipowapa watu sahihi kwao kwa sababu ya kutokumcha Mungu waliwakataa eti kisa hawana pesa,wafupi sijui sura zao haziendani nao alimradi vurugu sasa wanaona menopause inaingia wanamkimbilia Mungu na tena sio wao kusali kujiombea wanamtegemea mtu awawekee mikono ili wafanikiwe.
Viongozi wa dini na waanzilishi walikuwa ni wachapakazi..., Muujiza mkuu ni kubadilika na kuacha maisha ya ovyo,
Mungu amempa kila mwanadamu hai uwezo wa kufanikiwa, uvivu na utegeaji ni dhambi...
Kumbukumbu 8:18
But remember the LORD your God, for it is he who gives you the ability to produce wealth, and so confirms his covenant, which he swore to your ancestors, as it is today.

Ujawahi kujiuliza kwa nini Mchungaji anatajirika kwa kuwafundisha watu wawe matajiri, Ukifuatilia wengi anaojihusisha nao ni matajiri tayari sio wale makapuku.
 
Hata Biblia inasema,mmoja asome na afundishe wengine..! Mkisoma wote, nani atamfundisha mwenzake, ndio mwanzo wa ubishi huo...!
Akisoma na kufudisha, Wengine nanyi mnasoma kuona kama anachosoma na kusema ni chenyewe au ni mawazo yake.
Ndio maana duniani kuna watu wengi wanaamini vitu ambavyo havipo kwenye bibilia au msaafu kwa sababu ya kusikia.

Mfano
"Jisaidie na mimi (Mungu) nitakusaidia" haya ni maoni ya watu ila sio bibilia iliyoandika hayo.

Soma soma soma neno liweke kichwani na moyoni, usisubiri kuadithiwa mkuu
 
Mwanzo - Mungu aliumba mwanga alafu baadae akaumba chanzo cha mwanga nimeshindwa kuendelea kusoma biblia maana sielewi.
 
Mbona jibu rahis tu,,,njia za kuwapiga hela watanzania

(1) hubiri kupatikana kwa hela
(2) danganya unazo dawa za nguvu za kiume. Mbona fasta tu unatoka
 
Back
Top Bottom