Kwa Nini CCM Inango'ka?

Kwa Nini CCM Inango'ka?

Ocampo four

JF Senior Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
5,789
Reaction score
2,159
1. November 2, 1991 wananchi wa Zambia walimchagua Ndg. Chiluba ambaye alimshinda aliyekuwa rais kwa zaidi ya miaka 27 na mpigania uhuru wa nchi hiyo Mzee Kaunda; pamoja na sababu zingine ila kubwa zaidi, wananchi hao walihitaji "Mabadiliko".

2. Dec. 2002 chama kikongwe Africa cha KANU chini ya Rais MOI (M o One) kilishindwa vibaya sana na muungano wa NARC chini ya Mwai Kibaki kwa sababu wananchi walihitaji "Mabadiliko"...

Africa hakuna chama kilichokuwa na nguvu kubwa kama KANU. KANU ilisifika kwa kujenga nchi mpaka wimbo maalum wa kitaifa ulitungwa kwa ajili ya kuisifu KANU... "KANU yajenga Nchi".... Ila wananchi walihitaji mabadiliko wakaziba masikio na kufumba mambo...

3. Sep. 2011 Michel Sata pamoja na uzee wake alimshinda Rupia Banda kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko".....

Ukisoma kitabu cha Dambisa Moyo "Why Zambia" anakueleza vizuri sana jinsi Banda kipindi akiwa rais alijitahidi sana kujenga miundombinu (hasa barabara) mpaka vijijini.

Ila kwa bahati mbaya wananchi hawakuona haya yote kwa sababu ndani ya mioyo yao walisukumwa na hitaji kuu ambalo ni "Mabadiliko"

4. 2012, Macky Sall alishinda uchaguzi wa Senegal na kumbwaga mkongwe wa siasa za Africa Abdoulaye Wade mtu aliyekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Kwa hakika haikuwa jambo jepesi wala kazi nyepesi lakini kwa kuwa wananchi walihitaji "mabadiliko" Rais Sall alishinda kwa zaidi ya asilimia 65%....

5. 2015 pamoja na kutukanwa juu ya umri wake, afya yake, na familia yake Ndg. Buhari aliibuka mshindi na kumgaragaza rais aliyekuwepo madarakani (sitting president) G. Jonathan kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko"..

Nakumbuka Gavana wa Itiki Ndg. Fayose alizunguka nchi nzima ya Nigeria akimtukana Buhari na kusema haifiki siku ya uchaguzi Buhari atakuwa amekufa. Ila leo hii tunashuhudia rais mpya wa Nigeria ni Buhari....

6. Pagan Amum (SG) wa SPLM, South Sudan aliwahi kusema kwamba, inafikia kipindi mabadiliko katika nchi yoyote ile hayakwepeki. Wananchi wanapodai mabadiliko haijalishi umewafanyia mazuri kiasi gani au mabaya kiasi gani ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko.....

Wananchi wanapotaka mabadiliko haijalishi na hawaitaji kujua yatakuwa mabadiliko ya namna gani, ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko...

Wananchi wanapohitaji mabadiliko hawahitaji kujua kama yatakuwa positive kwao au negative kwao wenyewe wanachokijua kwa wakati huo ni kupata mabadiliko....

Wananchi wanapohitaji mabadiliko alyways wanaziba masikio na kufumba macho... Ukiwa chama dola hata uwambie nitakuletea maziwa mlangoni kwako kamwe hawezi kukusikia.... Na akiwa kijana hata ukimuahidi kumpatia msichana mzuri sana kama Cinderela au Cleopatra hawezi kukuelewa... Kikubwa kwake ni kupata mabadiliko...

NB:.. Ndugu zangu CCM inango'ka kwa sababu wananchi wanahitaji mabadiliko. Tumechoka!....
 
Mada inajitosheleza asante mkuu labda wakiambiwa mara nyingi wataelewa hakuna njia nyingine tnataka mabadiliko nje ya ccm
 
Kwa wasiojua CCM ndio kikwazo nambari moja cha maendeleo nchi hii...

Bahati mbaya wenyewe wamefungwa nankupumbazwa hata wasijue hilo...

Siku watakayoondoka madarakani kuna kila namna chama hicho kitapoteza kabisa nguvu yake juu ya uso wa Tanzania...
 
1. November 2, 1991 wananchi wa Zambia walimchagua Ndg. Chiluba ambaye alimshinda aliyekuwa rais kwa zaidi ya miaka 27 na mpigania uhuru wa nchi hiyo Mzee Kaunda; pamoja na sababu zingine ila kubwa zaidi, wananchi hao walihitaji "Mabadiliko".

2. Dec. 2002 chama kikongwe Africa cha KANU chini ya Rais MOI (M o One) kilishindwa vibaya sana na muungano wa NARC chini ya Mwai Kibaki kwa sababu wananchi walihitaji "Mabadiliko"...

Africa hakuna chama kilichokuwa na nguvu kubwa kama KANU. KANU ilisifika kwa kujenga nchi mpaka wimbo maalum wa kitaifa ulitungwa kwa ajili ya kuisifu KANU... "KANU yajenga Nchi".... Ila wananchi walihitaji mabadiliko wakaziba masikio na kufumba mambo...

3. Sep. 2011 Michel Sata pamoja na uzee wake alimshinda Rupia Banda kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko".....

Ukisoma kitabu cha Dambisa Moyo "Why Zambia" anakueleza vizuri sana jinsi Banda kipindi akiwa rais alijitahidi sana kujenga miundombinu (hasa barabara) mpaka vijijini.

Ila kwa bahati mbaya wananchi hawakuona haya yote kwa sababu ndani ya mioyo yao walisukumwa na hitaji kuu ambalo ni "Mabadiliko"

4. 2012, Macky Sall alishinda uchaguzi wa Senegal na kumbwaga mkongwe wa siasa za Africa Abdoulaye Wade mtu aliyekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Kwa hakika haikuwa jambo jepesi wala kazi nyepesi lakini kwa kuwa wananchi walihitaji "mabadiliko" Rais Sall alishinda kwa zaidi ya asilimia 65%....

5. 2015 pamoja na kutukanwa juu ya umri wake, afya yake, na familia yake Ndg. Buhari aliibuka mshindi na kumgaragaza rais aliyekuwepo madarakani (sitting president) G. Jonathan kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko"..

Nakumbuka Gavana wa Itiki Ndg. Fayose alizunguka nchi nzima ya Nigeria akimtukana Buhari na kusema haifiki siku ya uchaguzi Buhari atakuwa amekufa. Ila leo hii tunashuhudia rais mpya wa Nigeria ni Buhari....

6. Pagan Amum (SG) wa SPLM, South Sudan aliwahi kusema kwamba, inafikia kipindi mabadiliko katika nchi yoyote ile hayakwepeki. Wananchi wanapodai mabadiliko haijalishi umewafanyia mazuri kiasi gani au mabaya kiasi gani ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko.....

Wananchi wanapotaka mabadiliko haijalishi na hawaitaji kujua yatakuwa mabadiliko ya namna gani, ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko...

Wananchi wanapohitaji mabadiliko hawahitaji kujua kama yatakuwa positive kwao au negative kwao wenyewe wanachokijua kwa wakati huo ni kupata mabadiliko....

Wananchi wanapohitaji mabadiliko alyways wanaziba masikio na kufumba macho... Ukiwa chama dola hata uwambie nitakuletea maziwa mlangoni kwako kamwe hawezi kukusikia.... Na akiwa kijana hata ukimuahidi kumpatia msichana mzuri sana kama Cinderela au Cleopatra hawezi kukuelewa... Kikubwa kwake ni kupata mabadiliko...

NB:.. Ndugu zangu CCM inango'ka kwa sababu wananchi wanahitaji mabadiliko. Tumechoka!....

Umemaliza kazi.Kweli kabisà wananchi wanahitaji Mabadiliko sio ahadi mpya.
 
CCM wanaamini wataizuia treni ya UKAWA kwa kulala kwenye reli...huo si ujasiri ni ujinga na ujinga hujenga kiburi. CCM wamelewa na kujawa kiburi cha kutisha hadi wanasahau hii ni nchi yetu sote na hivyo kuanza kuropoka hovyo kama vile wanayo hatimiliki katika utawala. Wasichotambua ni kwamba mabadiliko wakati wake ukifika hayazuiliki na kama hukuyapisha yatakupitia kama gari moshi inavyompitia mlevi aliyelala kwenye reli.
 
"Tanzania mpya inakuja" sauti hii wanajamvi ina nipa nguvu ya kwenda mbele na kupigania mabadiliko.CCM Imeng'oka tayari
 
Sijawahi changia hata siku moja hapa jamvini lkn nimekuwa msomaji sana wa mada mbali mbali. Lkn hii ya leo nafsi inanisuta nisipotoa HESHIMA KWAKO Big up sana

Et "sijawahi changia hata siku moja" na hiyo nayo ni sifa?
 
Back
Top Bottom