kwa nini Barca wameanzia ugenini ktk mechi zote za mtoano msimu huu?

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,682
tunafahamu kuwa timu itakayoshika nafasi ya kwanza ktk hatua ya Makundi ya UEFA champions league basi tunapoingia ktk raundi ya pili anatakiwa aanzie ugenini kisha anakuja kumalizia nyumbani.

Sasa je kigezo gani alichonacho Barca kilichompa upendeleo wa kuanzia ugenini ktk mechi ya robo fainali dhidi ya AC Milan na kisha kesho watakuwa London kwa Chelsea kuanza mechi ya kwanza ya nusu fainali kisha mechi ya pili itakwenda kupigwa Nou Camp.

So kama kuna anayeelewa anidokeze kabla sijafunga safari mpaka Uswis yalipo makao makuu ya shirikisho hilo la Soka barani Ulaya.
 
nadhani ni kwa sababu barca ni mabingwa watetezi...kwahiyo wanaazia kucheza ugenini ili kuzipendelea timu nyingine kwa sababu ukianzia kwenye kiwanja cha nyumbani unakuwa na ka advantage kidogo ka ushindi...ila kwa barca haijalishi umeanzia nyumbani kwako au nou camp...ni kuchezea kichapo tu...!
 
Mwambie huyo.
 
mfumo wa Fifa ni Kuwa ile timu yenye rank ya Juu.. Ndio inayoanzia ugenini duniani kote hata ukiangalia mechi za CAF.. Mfano simba ilipokuwa inacheza na kiovu ilianzia Rwanda kwasababu Simba Iko Juu ya Kiovu.. Au Beyern walivokuwa wanacheza na Marseile.. Utaratibu uko hivo kaka ranking ndo inaamua
 
Mtoa mada amezungumzia UEFA.
Hayo mambo ya CAF na FIFA yako nje ya Mada.
 
mkuu naona bado una machungu ni kichapo barca walichowapa milan!

by ze the way, gaucho anaendeleaje ni kile kitambi chake huko brazil?

Hivi unajuwa Companero kuna posti zako nyingine huwa unachuma dhambi dhahiri shahiri...
Dinho ni mbarikiwa
 
Wadau naona wote mmechangia ila sijaona aliyetoa jibu sahihi katika hii hoja...Ni hivi miaka ya nyuma walikuwa wanachagua kwa kuzingatia matokeo yaliyotangulia katika hatua iliyopita.timu iliyofanya vizuri zaidi inapewa advantage ya kuanza ugenini..kwa mfano Chelsea walimfunga Benfica 1-0 ugenini na 2-1 nyumbani (agg 3-1) wakati Barca walidraw milan na kumfunga 3-1 AC Milan nyumbani..kwa sababu Chelsea walikuwa na aggregate sawa na Barca kwa hii old rule wangepewa advantage ya kuanzia away kwa sababu wana better away result,kwa kumfunga Benfica nyumbani kwake LAKINI old rule hii haitumiki kwa sasa badala yake wakati wanafanya draw ya hatua zote hadi fainali,sio tu draw ya nani anacheza na nani bali pia ya nani anaanzia wapi..Kwa mfano maneno ya mtangazaji " We are going for the semi final draw now,remember the first team to be drawn will be playing the first leg away.<<.balls rolling>>..Its Barcelona..so Barcelona will play the first semi final leg away against who?..<<balls rolling>>..Chelsea..so our first semifinal will be Chelsea vs Barcelona..
 
Mimi naona ile ni timu bora na kama ni mabingwa ni bora wapendelewe na kama timu inataka upendeleo ioneshe ubora wake
 
hivi kwanini mmetoa "STICKY" thread ya BARCELONA TEAM/FANS?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom