Kwa niaba ya Gambo, Mkuu wa wilaya ya Arusha aagiza ng'ombe wavishwe hereni

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dangalo, amewaagiza wataalamu wa mifugo na kilimo katika wilaya zote za mkoa wa Arusha, kuhakikisha wanafanya sensa ya kutambua idadi ya mifugo na kuivalisha hereni.

Dangalo ametoa kauli hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuboresha ng’ombe wa maziwa ADGG, uliowahusisha wafugaji kutoka halmashauri ya Arusha na jiji la Arusha iliyofanyika mkoani hapa.


Amesema maelekezo ya mkoa ni kuhakikisha ng’ombe wote waliopo kwenye wilaya, mkoani hapa, wanaingizwa kwenye mpango wa utambuzi kwa kuvalishwa hereni, chini ya mradi wa kuboresha mradi wa ng’ombe za maziwa wa ADGG.

Mratibu wa mradi huo Dk. Eliaman Lyatuu amesema suala la uwekeji hereni za kitaifa kwa ng’ombe wa maziwa kwa ajili ya utambuzi ni mpango mzuri ambao unafanyika kwa nchi mbalimbali duniani na tayari halmashauri ya Arusha na jiji la Arusha, wameshavalisha ng’ombe wa maziwa zaidi ya 300 .


Ameongeza kuwa mpango huo umepokelewa vizuri na wafugaji na utawasaidia kutambua ng’ombe wao hata pale watakapokuwa wanahamisha mifugo kutoka eneo moja kwenda eneo lingine, pia ng’ombe anapopotea ama kuibiwa inakuwa rahisi kumtambua.

Chanzo: Mpekuzi

*************
Huyu ni yule DC aliyeteuliwa hivi karibuni akitokea kikosi maalum cha ulinzi Wa viongozi wakubwa.

Hapa kasi tu
 
image_82_animal%20ear%20tag%20for%20cattle.jpg


Hakuna cha ajabu.
 
Nakubaliana na mpango uliopendekezwa na RC/DC. Vita kati ya wafugaji na wakulima sasa ni janga. Hatua hiyo ni sehemu ndogo ya long-shot to a permanent solution. Watekeleze na mengine sambamba na hilo ili tutoke hapa tulipokwama.
 
Back
Top Bottom