Kwa mtazamo wa kiimani , je ni kweli waafrika walilaaniwa?

Bornventure

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
529
523
Nianze kwa kusema kwamba binafsi uwa nawaza saana nikiitafakari hii dunia na historia ya binadam mabadiliko na maendeleo yake huku nikijaribu kuitazama nafasi ya mtu mweusi ktk mwendo huu wa historia mabadiliko na maendeleo binafsi naishia kuumia sana hasa pale ninapojaribu kuwaza tena nafasi ya mtu mweusi was Africa ktk siku zijazo.
Najiuliza maswali mengi ambayo nahitaji mchango wenu wadau,
1. Kwa mtazamo wa kiimani , je ni kweli waafrika walilaaniwa wawe hivi walivyo?
2.Je waafrika wana asilimia kubwa ya u-mnyama mnyama na asilimia ndogo saaana ya binadam that's why ni ngumu kumbadilisha mwafrika kwa nyenzo yoyote ile (mf elimu, imani, mazingira nk?
 
1.Suali la kiimani linapaswa kujibiwa kiimani yako husika kwani likitolewa nje ya imani yako hata lipambwe vp bado utalitilia shaka na ndio maaaana ikaitwa imani ni bora ungejitambulisha unaamini dini ipi ili tushuke kwa dini yako na km si muamini dini ukutane na wenzio akina kiranga wakudadavulie.

2. Nanukuu ( mf. Elimu, imani, mazingira n. k)
Sijajua umefanya tafiti ya aina gani hadi ukaamini hivyo ulivyovitaja waafrika hatuvizingatii kiusahihi au hatuna ueredi navyo.
Nianze na...
Elimu.......
Binafsi nimesoma kayumba ila sijawahi kusikia kwa wale walosoma international school na watoto wa kizungu, kichina n.k kuwa wao cku zote ndo wanaongoza darasa bali utaskia wenzetu wanaongoza wao ndo wanafuatia na ukitokea kuongoza ni nadra km TO wa kipindi 2015 na sidhani km alishawahi kutokea b4.

IMANI....
Hili kidogo nitakuwa na mushkiri nalo ila si ktk kuamini dini. Ila ni utofauti wa ktk kuamini na hapa lile neno ulilotumia AKILI FINYU linaweza likawa mahala pake ni hivi majuzi tu ktk pitia pitia za social media nikakutana na orodha ya viongozi wa dini moja wenye nazo kidunia ikaoonesha top 10 inashikiliwa na waafrika nikawa najiuliza hivi ni kweli wazungu wako tayari kumpa mtu pesa km sadaka alafu baada ya mwezi wamuone ananunua hekalu Las Vegas wakakubali kuendelea kumpa tena pesa mtu km huyu ndo nikajua kwa wenzetu haliwezekani ila huku kwetu ni kawaida na hata wale viongozi wa dini wa rangi nyingine ukiskia ana pesa nyingi ukimfuatilia utaskia misafara mingi anaifanya Africa kiasi fulani wanatutumia kiutumwa wa kiimani ndio maana wakatoliki wakawa na mfumo mzuri wa makusanyo ya sadaka na kuwapelekea wanaostahili.

MAZINGIRA...
Hapa mkuu umeniacha njia panda Sijajua ni mazingira kinamna ipi maana naona kila sehenu anayoishi mzungu na mwafrika anaishi ila tumetofautiana uasili ya sehemu tulizolowea.
 
Nashukuru kwa mchango wako bwana mkandu. Nifafanue tu zaidi kwamba nilipoongelea
1.Elimu, kuna tofauti kubwa ya tabia na mitizamo kati ya mwafrika msomi na race nyingine. Asilimia kubwa ya wasomi wa kiafrika elimu imewafanya badala ya kuwaza au kuibua mambo mapya ya kuibadilisha afrika (positively) na kuwawezesha waafrika wengine wa kawaida kuinuka wao wamebadilika na kuwa wabinafsi zaidi, na wakiibua mbinu za kuwakandamiza zaidi waafrika wasio na elimu.?
2.Mazingira, kiufupi ninaelewa kwamba akili kubwa humuwezesha mtu ku master vyema mazingira yake kuyafanya yawe safe, supportive, productive and attractive zaidi. Nadhani kwa kuyaangalia tu mazingira mengi afrika unaweza ukapata picha ya ufinyu wa akili zetu bila kujali tumeelimika au lah.
Hata kwenye suala la imani pia no shida japo hilo ningependa wataalam wanisaidie zaidi.
 
Back
Top Bottom