Ndugu wana JF, nawasalimu na kuwapongeza kwa kujadili mada na sio kujadili watu!
Napenda kutoa masikitiko yangu makubwa kwa wizara yetu ya ardhi, masikitiko yangu yanalenga hasa katika zoezi hili linalo endelea la upimaji wa viwanja katika halmashauri mbali mbali hapa nchilni.
zoezi hili ni zuri sana, hasa ukizingatia miji yetu mingi ilivyojengwa kiajabu, hakuna mpangilio wala mitaa ya kueleweka, sasa tatizo hapa ni hawa watendaji wa hizo idara za ardhi katika halmashauri, walio wengi sasa wanaona ndipo pa kutajirikia, kwa mwananchi wa kawaida kupata kiwanja kwa bei ya serikali ni ngumu sana, ila ukiwafuata wao kwa mlango wa nyuma viwanja wanavyo wamegawiana wao ili wauze kwa bei ya juu, hili ni tatizo kubwa tena ni ufisadi.
tatizo jingine kubwa ni kwamba bei ya ardhi ni kubwa sana kwa wananchi wa kipato cha chini. nitatolea mfano kigamboni eneo la Geza ulole ambako zoezi la upimaji viwanja linaendelea, serikali inauza sqm1 kwa Tsh 6,000/= hadi tsh 8,000/=, sasa hii bei ni kubwa kwa wanachi wa hali ya chini na mbaya zaidi wanatoa siku 21 ili mtu awe amemaliza kulipia kiwanja, kwa mfano mtu ukipewa kiwanja chenye ukubwa wa sqm 800 unatakiwa kulipa Tsh 4,800.000/= na gaharama nyingine za upimaji. sasa niambieni kwa mtanzania wa kipato cha chini (mamalishe,machinga, na wafanyakazi wenye mishahara ya kima cha chini ) je wataweza kulipa ndani ya hizi siku 21 kweli? kwa nini wasipewe walau miezi 6 walipe kidogo kidogo?
Ombi langu kwa serikali maana najua kunawengi tu wapo humu JF, nawaombeni kama kweli wana nia ya kuwauzia wananchi wa kawaida viwanja vilivyopimwa na wao waishi katika mitaa iliyopangika, wawape muda wa kutosha wa kulipia ardhi, wapewe miezi 6 hadi mwaka mzima.
wana JF naomba wenye uwezo wa kulifikisha hili kunakohusika walifikishe tuwasaidie wananchi wenzetu wenye kipato cha chini. na hasa likienda Bungeni litasaidia hawa wananchi wanaohitaji kupata makazi bora pia.
nawasilisha.