Kwa Mtaji huu wenye kipato cha chini watamiliki viwanja?

mbogo31

JF-Expert Member
Nov 28, 2008
711
173
Ndugu wana JF, nawasalimu na kuwapongeza kwa kujadili mada na sio kujadili watu!

Napenda kutoa masikitiko yangu makubwa kwa wizara yetu ya ardhi, masikitiko yangu yanalenga hasa katika zoezi hili linalo endelea la upimaji wa viwanja katika halmashauri mbali mbali hapa nchilni.

zoezi hili ni zuri sana, hasa ukizingatia miji yetu mingi ilivyojengwa kiajabu, hakuna mpangilio wala mitaa ya kueleweka, sasa tatizo hapa ni hawa watendaji wa hizo idara za ardhi katika halmashauri, walio wengi sasa wanaona ndipo pa kutajirikia, kwa mwananchi wa kawaida kupata kiwanja kwa bei ya serikali ni ngumu sana, ila ukiwafuata wao kwa mlango wa nyuma viwanja wanavyo wamegawiana wao ili wauze kwa bei ya juu, hili ni tatizo kubwa tena ni ufisadi.

tatizo jingine kubwa ni kwamba bei ya ardhi ni kubwa sana kwa wananchi wa kipato cha chini. nitatolea mfano kigamboni eneo la Geza ulole ambako zoezi la upimaji viwanja linaendelea, serikali inauza sqm1 kwa Tsh 6,000/= hadi tsh 8,000/=, sasa hii bei ni kubwa kwa wanachi wa hali ya chini na mbaya zaidi wanatoa siku 21 ili mtu awe amemaliza kulipia kiwanja, kwa mfano mtu ukipewa kiwanja chenye ukubwa wa sqm 800 unatakiwa kulipa Tsh 4,800.000/= na gaharama nyingine za upimaji. sasa niambieni kwa mtanzania wa kipato cha chini (mamalishe,machinga, na wafanyakazi wenye mishahara ya kima cha chini ) je wataweza kulipa ndani ya hizi siku 21 kweli? kwa nini wasipewe walau miezi 6 walipe kidogo kidogo?

Ombi langu kwa serikali maana najua kunawengi tu wapo humu JF, nawaombeni kama kweli wana nia ya kuwauzia wananchi wa kawaida viwanja vilivyopimwa na wao waishi katika mitaa iliyopangika, wawape muda wa kutosha wa kulipia ardhi, wapewe miezi 6 hadi mwaka mzima.

wana JF naomba wenye uwezo wa kulifikisha hili kunakohusika walifikishe tuwasaidie wananchi wenzetu wenye kipato cha chini. na hasa likienda Bungeni litasaidia hawa wananchi wanaohitaji kupata makazi bora pia.

nawasilisha.
 
Ndugu wana JF, nawasalimu na kuwapongeza kwa kujadili mada na sio kujadili watu!

Napenda kutoa masikitiko yangu anatoa siku 21 ili mtu kulipa Tsh 4,800.000/= na gaharama nyingine za upimaji.
Nafikiri madiwani ndo wakubeba kilio hiki, vinginevyo tunatengeneza matabaka, angalia kima cha chini cha serikali ni 150000 ili itimie 4.8mil ni miezi 32 kweli kuna lengo la kumkomboa mnyonge? Ni vigezo gani vinatumika kupanga hizo bei? Wataalam wa sera na sheria watujuze na nani anawajibika kwa hili? Utauza maandazi miaka mingapi upate 4.8mil, tena sio huko Gezaulole tu hata ilala nao rate zao zafanana! Wawakishi wa wananchi mpeleke kilio chetu ngazi husika!

Hii style ni kuiweka nchi yetu kwa mapepari wachache wenazo!!
 
Na hapo umeassume mshahara wote ni kwa ajili ya kulipia kiwanja tu, hali,hasomeshi nk.
 
Ni lipi serikali haijui kuhusu maisha na uwezo wa wananchi wake? Serikali inafanya tu makusudi na imewadharau mno wananchi wake na haina huruma japo serikali ni watu.
 
Unaongelea Wizara iliojaa majambazi, majizi, wauaji, dhulumati hasa katika taasisizake hadi Wilayani.
 
Wako wapi watetezi wa wanyonge?, haya ndo maisha bora? Hii ndo mipango ya uchumi endelevu unaotaka kupaa? Nani hajui unapozungumzia uchumi huwezi kuacha ardhi! Kila cku takwimu zinatolewa kuwa wastani kipato cha mtz halisi ni chini dola moja ndo walio wengi haya mil 4.8 ndani ya cku 21 atazitoa wapi?. Hawa watu wanaopanga haya ni watz au wametoka sayari ya mars?. Au mama Tiba hajapelekewa walau kuperuzi wakati wanapanga hizi rate? Walueleweshe namna gani wamezingatia takwimu za hali ya uchumi ktk kuamua haya! Au ndo hujuma ili wananchi wazidishe hasira kwa serikali? Inashangaza sana na naona twapotea! Ni ipi kesho yetu?
 
Wizara hii kwa sasa imejaa dhuluma huyu Mama Tibaijuka na Katibu Mkuu wake Rutabanzibwa hawana malengo ya kuwanufauifaisha watanzania wanatumia nafasi zao kujitajirisha zaidi kwa kunyanganya wananchi viwanja.
 
Nafikiri madiwani ndo wakubeba kilio hiki, vinginevyo tunatengeneza matabaka, angalia kima cha chini cha serikali ni 150000 ili itimie 4.8mil ni miezi 32 kweli kuna lengo la kumkomboa mnyonge? Ni vigezo gani vinatumika kupanga hizo bei? Wataalam wa sera na sheria watujuze na nani anawajibika kwa hili? Utauza maandazi miaka mingapi upate 4.8mil, tena sio huko Gezaulole tu hata ilala nao rate zao zafanana! Wawakishi wa wananchi mpeleke kilio chetu ngazi husika!

Hii style ni kuiweka nchi yetu kwa mapepari wachache wenazo!!

Mkuu,

Mfalme Haile Selasie wa Ethiopia alishawahi kuambiwa kuwa watu wake wanakufa kwa kukosa "mkate" ikiwa na maana kuna njaa sana. Yeye aliwajibu kuwa "Kama hakuna mkate basi wale keki". Walio juu serikalini wamejisahau sana. Hawaelewi hiyo shida unayoizungumzia wewe. Wamelewa anasa na majigambo. Chukulia hili; Gavana wa benki kuu anakarabati nyumba kwa Tshs 2 billion; Mkurugenzi anapanda gari la TShs 200 million; etc etc. Hilo sio la kushangaza, bali cha kushangaza ni watawala kutetea kuwa hakuna cha ajabu hapo. Ni sawa na haki kwao kufanya hivyo halafu WaTZ wanakaa kimya.

Hivyo viwanja vitanunuliwa mpaka na mhudumu wa ofisi. Alikotoa hela usimuulize, hiyo ndiyo TZ. Atakayeshindwa ni Mwalimu, ambaye hana safari wala faili la kuficha au vocha ya kufoji, Nesi ambaye kia siku Takukuru wako mgongoni, na wengine wa aina hiyo.
 
Kaka nashukuru,

sasa tunawasaidia je hawa watu wa chini?, au hakuna watu walio karibu na huyu mama Tiba ili wamjuze, nawahurumia sana WTZ wenzangu ambao wanaona haya matatizo lakini wanasema sasa tufanyeje, wakati watz tupo more than 40m na watawala wanao tuburuza hawazidi hata laki moja.
 
Twaomba serikali itoe bure viwanja kwa wananchi wasio na uwezo! Ardhi hii ni ya mwenyezi mungu ambayo aliwapa viumbe wake waimiliki iweje sasa ifanywe kuwa biashara? Isitoshe hizo fedha zinazodaiwa wananchi wa kawaida wanazitoa wapi? Kwa maana nyingine serikali haitaki wananchi wa kawaida wamiliki ardhi wakati wananchi hawa ndio waliofyeka mapori na kujitengenezea viwanja kwa gharama zao halafu serikali inataka kuchukua maeneo na kuwalipisha! Uonevu mtupu.
 
this is something very serious. kumiliki kiwanja kwa ajili ya makazi iwe ni haki ya kikatiba.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom