Kwa msimamo huu wa spika Makinda; Naamini CCM inawatoa kafara la damu watanzania!


kapime akili faza....
 
Kobello may be you are right in your own context maana ila ulipokosea ni kuwa unajenga hoja ambayo ni internal inherited or yours is backed by any school of thought. Maana hata watu wanaofuata Hegelian philosophy ambayo huamini mwafrika si mali kitu nao wanao wafuasi japo their context ni prejudiced, biased, inhuman and contains highest degree of segregation. Sasa turudi kwenye msimamo wako kuwa hakukuwa na haja ya kuahirisha bunge ili kuwapa wawakilishi nafasi ya kwenda kulia na wenzao, kuokoa na kufariji. Huu ni ufinyu wa kufikiri nje ya box. Inawezekana falsafa yako inakufanya kuyaona mambo katika umbali wa pua. Hivi wabunge kama binadamu unaona hawana msaada wanaoweza kuutoa wakati wa maafa/majanga hata kama yametokea mbali. Hawewezi kutao damu kwa yule mwenye kuhitaji? Wengine ni madaktari kwa taaluma, wengine wana ujuzi wa uokozi na wengine wanaweza kutoa mawazo endelevu ya kutatua tatizo as long as they in the field. Najua umependa sana ideology yako na unataka kila mfuasi wa ideology hiyo asiguswe na uamuzi wake ni sahii lakini huku ni kuifanya ideology iwe dead if not existinct. Lakini hata hivyo bunge linegeendelea kujadili nini wakati watu wanakufa? Chombo cha usafiri ni mtakuja ni ufinyu wa fikra ukidhani madhali walitokea Dar kwenda Zanzibar basi walikuwa ni wa upande mmoja wa nchi kwa hiyo hawakuwepo wa Kongwa, Gairo, Dodoma kiasi cha kuwafanya wabunge wajumuike na wapiga kura wao. Amka, toka ndani ya box na kuwa karibu na watu
 
Last edited by a moderator:

This reflects the apex of your analytical capacity and understanding of the political mathematics and acrobatics!! Pole. Wabunge ni wanasiasa, katika matukio ya aina hiyo wanasiasa wanayo moral obligation ya kuwa karibu sana na wapiga kura wao; majanga kama haya huibua hisia kali na yaweza kusababisha uvunjifu wa amani ikihisiwa kuwa viongozi wao hawajali shida zao, majuzi tumemshuhudia Prezo Obama akiweka pembeni kila shughuli ya taifa hilo kubwa kwenda kuwafariji wananchi wake wa jimbo la Colorado ambao walipata janga la moto wa kiangazi, a week ago Preso Putin wa Russia aliacha kazi zote katika taifa hilo kubwa pia kwenda kuwafariji wanachi wake kusini mwa nchi hiyo waliokumbwa na janga la mafuriko na maporomoko ya ardhi; hiyo ni kazi muhimu kwa wanasiasa vinginevyo hawataeleweka kwa wapiga kura wao hata kidogo.
tatizo la makinda lilikuwa kudhani waluiokufa ni wana Chadema kwa hiyo sio kitu!!!!!!!!!!!!!! kawatambua wazenj.
 
Sasa hawa jamaa mbona wanagongana na figure za waliokufa............ kila moja ana namba yake. Hizo source ni akina nani?? Inakuwaje waziri, serikali na vyombo vya habari vinatoa namba inayotofautiana kiasi hicho?? CCM wanaweza kuishia na hiyo namba 6 ili kuonyesha umma kuwa maafa hayakuwa makubwa.


 
Kwa reasoning hii basi hata msibani tusiwe tunaenda
maana kwenda kwetu hakuwezi kumsaidia marhem
Bora tuwaache wachimba kaburi na waosha maiti tu
Sisi tuendelee na shughuli zetu za kawaida. wasemaje?

Unajua mwali tatizo ni wabunge kutaka umaarufu wakati watu wanaumia. Kuahirisha bunge siyo kuonyesha kwamba wabunge ndiyo wanajali. Maana baada ya hapo walianza kuzurura tu pale nje. Suala lilikuwa kuahirisha hoja ya bajeti ya wizara mambo ya ndani halafu waziri anayeshughulikia na hayo masuala ya usafiri atoe statement (wenzetu wa kenya huita ministerial statement). Hapo wabunge wangetaka Waziri aseme hadi wakati ule kuna juhudi gani za uokozi zinazofanyika, kwa wakati ule kuna wangapi wamefariki na wangapi wamejeruhiwa na nini kinafanyika kuokoa maisha ya majeruhi nk. Pia Waziri angetakiwa kueleza kwa nini hizi ajali zinatokea mara kwa mara na hatua zipi zitachukuliwa ili kuzuia hayo mambo. Hapo wabunge wangekuwa wamewasaidia sana wananchi badala ya wao kutoka na wananchi kuanza kutegemea vyombo vya habari.

Kwangu mimi nadhani wabunge walitakiwa kuchukua jukumu la kiuongozi ili kuifanya serikali iwajulishe wananchi badala ya wao kuanza kukimbilia kutoa pole na kuiacha serikali itoe taarifa tu pale inapojisikia. So they were wrong, they are just doing a moral blackmail.
 

Ubongo wako utakuwa "shake before use"
 
Jamani Wana JF, msimshambulie sana huyu mama Makinda ni MGUMBA hawezi kuwa na uchungu wa wana wa Nchi.
Wagumba waliokosa watoto bila mapenzi yao wana uchungu na wana wa nchi. Huyu ni tofauti na hao.
 
Acha kujenga hoja zisizo na tija wewe nyangau gamba mkubwa usiye na huruma na roho za watu shwain
 
President = head of the executive.
Wabunge, waliendelea na vikao vyao.
Sana sana umejidhihirisha kuwa wewe ni limbukeni anayefikiri anajua sana .... very dangereous combination
 
Tujifunze katika hili, Makinda hakuwa sahii kwa maneno bali alikuwa sahii wa decision aliyochukua, japo watanzania hawawezi elewa! Tunajijua sie wabongo tunapenda sana unafiki! Sioni logic ya mtu kukurupuka kutoka bungeni, then akaishia kaunta. Dom Hotel anapiga simu tuu!

Sidhani hata ukiwa ofisini ukaambiwa baba yako kafa unakimbia hovyo bila kuuliza vizuri na ku handle over kazi za watu!

Au kama mama yako anafanyiwa operesheni utashinda umesimana mlango wa theatre unasubiria tuu!
 
Tuachwe tupumue hamuna udugu,ajali hii ni janga la taifa ililazimika kikao kimalize au kifungwe wabunge wakaungane na wananchi wao,lakini wapii ? Kwa wale wazanzibari wenye kuukumbatia muungano sasa wamejionea wenyewe,watanganyika sio ndugu zetu ni majirani zetu tu,muungano basi.
 

Uko sahihi kuhusu ministerial statement na Hamad Rashid alikuwa anaongea along those lines. Aliomba Spika aruhusu bunge lipitishe bajeti ya Home Affairs kwa mafungu ili kuruhu bunge lijadili jambo la dharura lililotokea na lenye manufaa kwa umma then baadae wabunge wengine wapate pia fursa ya kwenda kwenye tukio.

Kanuni zinaruhusu lakini Spika si tu alikataa ila kubwa alikataa kwa kutumia kauli ya kuudhi sana (na hii italeta shida ngoja watu wamalize kuzika).

Baada ya kukataa wabunge wa upinzani na baadhi CCM-zanzibar wakatoka nje. Huku nyuma wakawa wamebakia wabunge 49 tu, idadi ambayo ni chini ya threshold inayotakiwa kupitisha hoja.

Still, Spika na mawani yake hakuliona hilo hadi pale Nchimbi alipogundua idadi ndogo ya wabunge na kuindoa hoja yake mezani kwa kutumia kanuni za bunge.

Hivyo, technically speaking Spika hakuahirisha bunge, ila bunge lilikosa cha kujadili kwa sababu serikali iliondoa hoja yake mezani! Na hakukuwa na kitu kingine cha kujadili kwa siku hiyo so they had to go home/hotel rooms etc.

Hili kosa la Spika linaweza kutumika kama case study nzuri kuelezea umuhimu wa kuwa mtu mwenye ujuzi wa sheria kuongoza legislatures.lakini hata kwa kutumia busara ndogo sana bunge haliwezi kuendelea na kama kawaida in the midst of a national disaster. Walitakiwa wabadilishe hoja na kujadili ajali ya meli pamoja na hatua za haraka ili kukabiliana na mkasa huo.

Kwa kumalizia, spika na team yake wanatakiwa sasa wakubali udhaifu wao na wajifunze kutumia lugha za heshma bungeni. Wabunge wote wako pale kwa nujibu wa sheria na ni watu wazima, haiwezekani spika na wenzake kuendelea kuwa-treat kama watoto au watu wasioelewa mambo. Hasa Spika anatakiwa aachane kabisa na huu mtindo wa kudhani kuwa ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuelewa kanuni za bunge. Zile kanuni sio manual ya kutengeneza rocket, zinaeleweka kirahisi sana. Lakini pia huwezi kusoma kanuni in isolation bila kuzingatia katiba. Bunge la sasa lina udhaifu mkubwa kwenye uelewa/appreciation ya sheria. Busara (or lack of it) ndio inaonekana kushika usukani. Matokoeo yake ndiyo haya tunayoona sasa kwamba bunge linaanza kupoteza ligitimacy mbele ya wananchi. Nani anatakiwa kuwajibika kwa hapa tulipofikia?
 
More than 100 missing after Zanzibar ferry sinks

Rescue workers fought rough seas on Thursday to search for more than 100 people missing after an overcrowded ferry sank near the Indian Ocean archipelago of Zanzibar, but hopes of finding survivors were slim.

At least 38 people, including an American citizen, were confirmed dead and 145 were rescued after the MV Skagit/Kalama passenger boat capsized on Wednesday around midday near Chumbe island, west of Zanzibar.

Zaidi hapa More than 100 missing after Zanzibar ferry sinks | Top News | Reuters
 
Mkuu unaweza ku-fabricate story ili i-fit maoni yako, and I can do the same.

Kusema kuwa "Technically bunge liliahirishwa based on quorum unaweza ukawa sahihi, ila hansards hazitaonyesha hilo na bunge liliahirishwa kutokana na ajali iliyokuwa inaendelea, ambayo ilimhusu waziri aliyeleta hoja.Speaker alishaongea na waziri kuhusu kuwapo kwa ajali na wakakubaliana kuwa taarifa kamili (kiserikali) itakapotoka, wanaweza kuliongelea hilo bungeni( hiyo ni kabla ya Hamad kutoa hoja).

Kabla ya taarifa kutoka serikalini, mbunge wa Wawi akatoa taarifa kuhusu ajali hiyo.

Sasa hapo ndipo siasa na utekelezaji vinapogongana. Kwa kuwa umepigiwa simu au umeona tukio kwenye Tv, haimaanishi kuwa officially hilo tukio limetokea, kuna logistics ambazo kama wewe upo serikalini unatakiwa uzijue na ufuate protocols zilizopo.
Ukipigiwa simu haimaanishi kuwa ndiyo taarifa rasmi. Kwa mfano mzee Paw angempigia simu Hamad kuwa Tanzania imevamiwa na Comoro na Hamad akataka kusitisha hoja kisa amepata simu kutoka kwa mzee Paw, atakuwa amekosea.

Speaker alikuwa na habari hiyo, ila ilibidi waziri baada ya kupata taarifa rasmi ndiyo angeomba bunge lijadili cha kufanya (kupiga picha kwa ajili ya facebook). Na siyo mbunge aliyepewa taarifa na jirani yake.

Kwa hiyo kususa kwa wabunge ni ulimbukeni wa sheria na taratibu za kazi (uswahili mwingi) kwa upande wa wabunge. Hasa wa CHADEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…