Kwa msimamo huu wa spika Makinda; Naamini CCM inawatoa kafara la damu watanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa msimamo huu wa spika Makinda; Naamini CCM inawatoa kafara la damu watanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jul 19, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo yanayosikitisha. Ambayo hata ukiambiwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuamini. Ni kichaa peke yake, tena yule mwehu ambaye hajapata matibabu ndio anaweza kuamini kuwa, spika wa bunge anaendelea kuendesha bunge wakati ambapo kuna meli inazama ikiwa na mamia ya watu ndani yake. Tena sababu ya kuzama kwake ni kutokana na upepo mkali. Huu ni ujinga uliovuka mipaka, bunge ni mali ya umma. Ndiyo maana huwezi kuingia pale ukiwa kama mbunge bila idhini ya wananchi. Leo wanaokupa idhini wanaliwa na samaki baharini, wewe unasema tunaendelea na kikao cha bunge. Au spika anajua nini kinachoendelea? Au CCM ili mambo yake yawe safi ni lazima itoe kafara? Nashangaa, sijaona mbunge wa CCM Akiguswa na tukio hili. Hii inamaana walikuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea. Kwa mara nyingine tena narudia kusema kuwa, Sisi watanzania ni wanafiki wakubwa pia. Leo tunapiga domo tu kwa kulalamika bila kuchukua hatua. Hawa jamaa hawata ondoka kwa kura hawa hata milele. Isipokuwa kwa nguvu na umoja wa watanzania mashujaa wenye moyo wa ujasiri. Mtanzania! Vua ganda la woga. Vaa lile la ushujaa tupambane na udhalimu huu.
   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Hayo mambo yanahusiana vipi na shughuli za bunge? Ajali ikitokea vikosi vya uokoaji, polisi wanajeshi na wafanyakazi wengine wanaohusika ndio wanaoshughulikia. Sasa wabunge waahirishe kikao ili wafanye nini?.. Itasaidia nini? Kama Hamad alikuwa na udhuru si angeenda tu kuwapa pole wanajimbo wake, haijalishi saa nne asubuhi au saa kumi na mbili jioni.
  Ni mambo ambayo kusema kweli hayana maana yeyote zaidi ya kuleta mtafaruku ndani ya bunge...... Pointless!
   
 3. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa reasoning hii basi hata msibani tusiwe tunaenda
  maana kwenda kwetu hakuwezi kumsaidia marhem
  Bora tuwaache wachimba kaburi na waosha maiti tu
  Sisi tuendelee na shughuli zetu za kawaida. wasemaje?
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu, jaribu kuwa na ubinadamu kidogo. Pamoja na ubinadamu, pia kuna dawa unazoweza kutumia ili kuondoa kichwani mabaki ya bangi uliyowahi vuta zamani. Ukatili na kutokuwa na huruma ni dalili ya kuathiriwa na bangi katika akili. Kumbuka, ilipotokea ajali ya treni. Spika mwenye huruma aliahirisha bunge. Au ulikuwa bado hujazaliwa? Huo ni mfano rahisi tu kwako. Ndio maana huwa tunaacha kazi zetu na kwenda kuhudhuria misiba. Unataka kuniambia wabunge wote waliotoka bungeni hawana akili? Nakusihi mama Makinda uwe na huruma. Najua wewe ndiye uliyetuma ujumbe huo hapo juu. Una roho mbaya wewe mwanamke ndiyo maana huna hata mume.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Watakuwa Wana muwakilisha nani wewe gamba?
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kile Kimama/Kibibi inabidi......tukishikie bango kiondolewe kwenye kiti cha Uspika......damn!
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Nani wakulioa Hilo balaa watu Wana tamaa ya hela lakini kuliko kuishi na Hilo limama bora ukachumbie mwanamke kutoka mirembe
   
 8. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mwenyewe umejitahidi kuandika nimesoma hakuna la maana hapa
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Hapana, wala usielewe vibaya.
  Ungefananisha na kuahirishwa kusikilizwa kesi zote za mahakama leo kwa kuwa kuna ajali ya meli.
  Au kuahirishwa kwa shughuli zote za kiserikali ili kutoa nafasi kwa wafanyakazi kwenda kwenye ajali.
  Bunge ni mhimili wa serikali kama ilivyo mahakama na utendaji... what are they going to do????
   
 10. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,525
  Trophy Points: 280
  Angekufa kiongozi wa magamba ungesikia namna hoja hiyo ambavyo ingeungwa mkono.Ndio maana hata kwenye mgomo wa madaktari spika hakuona umuhimu wa kujadili kwani watu wanaokaa madarakani muda mrefu hufikia hatua ya kupuuza watu wao kwa kulewa madaraka na kujisahau.
  Jiuliize huyu mama ana hofu gani na wapiga kura kwani kila uchaguzi anapita sasa unafikiri mbali ya ubinadamu atakuwa na hofu gani juu ya waliompeleka bungeni ila hali kila uchaguzi yeye anapita
  Hivi ukiwa umeajiriwa na hakuna kipengele cha kufukuzwa kazi kweli utamheshimu mwajiri wako?Ingawa kwa hili lilihitaji zaidi ubinadamu wa spika na si kitu kingine ila kwa maoni yangu ameshajua udhaifu wa watanzania na ndio maana watu wa chama tawala hawana hofu na wapiga kura wao kwa lolote watakalofanya kwani hata hofu ya kufukuzwa kazi kwao ni ndogo.
  Hata hivyo,wajue wanajidanganya na watanzania watawapima kwa matendo yao.
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Ajali ya treni ilitokea wapi? na Bunge lilikuwa wapi?
  Kwani hao wabunge walitaka kwenda msibani? Au walikuwa wanataka posho ya siku nzima kwa kazi ya nusu siku?
  Unaacha kazi kwenda kuzika, kama ni ndugu wa karibu unapewa muda wa kuwa msibani. Kuhudhuria mazishi na kuhudhuria msiba ni vitu tofauti.
  By the way, bado navuta.
   
 12. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Unlike mahakama na utendaji bunge lina uhusiano wa moja kwa moja na wananchi sababu ni direct representation of the people. And this was touching the very person who voted for them. Sijasema kua ilikua ni makosa, au ilikua ni sawa kuendelea na shughuli, ila tu nimesema hiyo reasoning ya kwamba there is nothing they could do haijakaa sawa. Pia likija suali la what could they do. I think katika wabunge kuna mebers of the government pia ambao walikua na uwezo wa ku-speed up the rescue process.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Wewe Gamba!!!!!! hao ni wawakilishi wa wananchi na wapo pale kwa kura zao tofautisha na mahakama au shughuli nyingine. Naona unatafutia watu ban wewe
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tofauti ipo mama Makinda. Wabunge wanawawakilisha moja kwa moja wananchi kwa sababu huingia pale kwa kura zao. Tofauti na mihimili mingine. Wananchi wanapopata majanga mtu wa kwanza kwenda kushirikiana nao anatakiwa awe muwakilishi wao katika serikali. Sasa unataka hakimu aje akuwakilishe wewe na mumeo. We mama vipi?
   
 15. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Usiulize ajali ya treni ilitokea wapi! Ajali ni ajali tu. Kwa watanzani ikitokea ndani ya mipaka yao zote ni ajali sawa bila kujali imetokea umbali gani kutoka Dodoma lilipo bunge. Kwani wanaosafiri ndani ya mkoa wa Dodoma kwa akili yako ndiyo binadamu. Wakishatoka nje ya mkoa wanakuwa ngedere?
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  Nianze kwenye nyekundu, how?
  Kama unazungumzia bunge kwa sababu limechaguliwa directly na wananchi,je limechaguliwa ili likafanye nini?
  Kumbuka kuwa mbunge siyo kiongozi wa wananchi wa jimbo lake, ni mwakilishi tu kwenye utungaji wa sheria. Zaidi ya hapo, ni mwananchi kama wananchi wengine. Sasa kama hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu anafanya kazi (as a regular citizen) kwanini mbunge asifanye kazi?
  Mbunge siyo kiongozi, siyo mtekelezaji na wala siyo mfanyakazi wa utendaji. Kuhudhuria kwake msiba ni kama wananchi wengine .... baada ya kazi unless awe anahitajika kwenye kikao cha halmashauri ya wilaya/manispaa/jiji husika.
  Mbunge huwakilisha jimbo na wanajimbo wake na rais huwakilisha taifa as a whole. Kwa hiyo Ndesamburo kususa kwa sababu hakupewa off ya kwenda unguja msibani (I doubt if he'd have gone newayz) haileti mantiki. Labda kama mnataka ku-force mambo, but nah!,.... sorry.
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Unfortunately sikuweza kuangalia bunge live lakini nimeona tu kw taarifa ya habari wakati Nchimbi akiondoa hoja bungeni ili bunge liahirishwe...sijui makinda anashutumiwa kwa lipi maana alikubali hoja na akaahirisha bunge. Aidha, mapungufu yanayoweza kutokana na mchango wangu wa kulaumiwa ni mleta hoja hapa kwani ana assume wote tulikuwa tukiangalia bunge live...tuambie what she did tuweze kumhukumu kwa hilo. Pili mkuu kobello naungana na wewe kwani kila kitu lazima kiwe na utaratibu...na ndiyo maana ya kuwa na government machinery...polisi na vikosi kadha....hapa labda angetoka waziri wa mambo ya ndani ..ulinzi nk ningeelewa sana kuwa wanawa push wa chini yao wachukue hatua stahiki alkini si kwa wabunge...ingekuwa ni pale panda mbili au area c basi ningesema wanakwenda kutoa msaada... nasikia kuna waliotoka yet wakawa wanazunguka zunguka tu nje ya ukumbi wa bunge for about one hour.
   
 18. p

  popolipo Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Some people are just a nuisance...hearing there points just makes one sick...Time will tell...the speaker was out of point as usual...she thought it was mnyika speaking and without guessing or weighing just brushed it aside...and we saw what she did...
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bunge liliahirishwa wakati gani na madai ya wapinzani yalikuwa wakati gani? Kuahirisha kujadili hotuba iliyokuwa imepangwa haina maana wabunge wote waende kuzamia kwa ajili ya kuokoa watu. Ni spika kuruhusu hoja ya dharura ili bunge lijadili hatua gani ya dharura serikali ichukue. Kubali usikubali. Ni upuuzi kukataa hoja isemwapo na mpinzani huku hoja kama hiyo ikitolewa na CCM ikubaliwe.
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mbona alivokufa mamake spika hakukaa ofisini kuendelea na shughuli zake
   
Loading...