Kwa mikakati hii dhaifu, vyama pinzani kwaheri

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Tunaona huko Uganda, pamoja na Museveni kutumia mbinu kama zile za ccm, Mugabe, Kagame, n.k ili kushinda uchaguzi bado tunaona wapinzani wanaleta amsha amsha baada ya uchaguzi kwa kwenda mahakamani.

Hii inasaidia sana kuendelea kuviweka masikioni na akilini mwa wananchi vyama pinzani na hivyo kuvipa uhai zaidi.

Kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa! Upande wa bara, wakati matokeo ya urais yakiendelea kusomwa na tume tukaambiwa UKAWA haikubaliani na matokeo yanayosomwa.

Na wakaiandikia tume waraka wa kuiomba isiendelee kuyasoma ili waweke utaratibu wa uhakiki manually.

Tume ikatupilia mbali pingamizi lile na ikaendelea kusoma hadi mwisho. Matokeo ya mwisho yaliposomwa ukawa ikatoa tamko la kutokubaliana na matokeo na tukaambiwa itaenda ICJ kushitaki. Mpk leo jiiiiiiiii!!!!!....!!!!!!.

Hatuoni harakati zozote za kisiasa zikiendelea. Wafuasi huku mitaani wamekata tamaa na inaelekea hata viongozi wamekata tamaa. Ukawa inasubiria matukio ndipo wayavalie njuga. Bahati mbaya JPM anaonekana kuzuia kabisa matukio yatakayotoa kiki kwa upinzani. Hali hii itapelekea kifo cha ukawa kimya kimya.....!!

Kwa upande wa Zanzibar baaday ya uchaguzi kufutwa kwa tamko batili (kama ilivyoelezwa na cuf) la Jecha S. Jecha hatukuona siasa za hamasa zilizokuwa zikifanywa na cuf kuzuia ama kunusuru utimilifu wa tamko la Jecha.

Zaidi tukaona Maalim Seif akicheza ngoma ya ccm ya kuingia peke yake kwenye mazungumzo ya kutanzua mgogoro wa kisiasa huku wanaccm wakiwa 5. Hii ilishangaza wengi. Iweje aende peke yake? Kwani ni mgogoro wa familia? Viongzi wenzake walikuwa wapi?

Sasa wamesusa uchaguzi ccm wamefanya yao na ulinzi madhubuti juu. Cuf kimyaaa!! Kimya hiki siyo tu kwenye majukwaa hata katika vyombo mahususi vya kutoa maamuzi hawatakuwepo. Hawatapata ruzuku. Chama kitakuwa na ukata.

Mikakati ya Kiza Besigye hatuioni. Mahakama hamuzioni? Najua mtasema tume za uchaguzi hazishitakiwi. Kwahiyo mnatumbiaje? Kwamba no way forward? Acheni siasa basi.

Kwa mikakati na mbinu hizi mbovu za vyama vya upinzani ccm itadumu. Maana ni kana kwamba mnasubiria siku ccm itawapa dola kama zawadi. Hilo halipo.

Chadema mmepoteza muelekeo wa misingi yenu ya kupinga ufisadi na hivyo mmepoteza imani kwa wananchi. Mtasema nn? Utamuambia nani akaandamane? Wakati wafia chama kama kina Dr. Slaa mliwanyanyapaa?
 
Tanzania rais akitangazwa huruhusiwi kupeleka kesi katika mahakama yoyote iwe duniani au mbinguni

CHADEMA Hawajawahi Kusema wanaenda ICJ
 
Mtu anatoa hoja badala ya kujibu kwa hoja mnaanza kujibu kejeli. Mnafikiri tunavisaidia hivi vyama bila sisi wananchi kuwaambia ukweli badala ya mapambio ya sifa kila siku ...
 
Bongo upinzani ni dhaifu na wakinafki

Sisi tunamchukia shein wao wanacheka tu
Shein, Maguful wameenda kumuona maalim seif wanacheka tu unafkir sisi tunachukuliaje
 
mtoa hoja mwenye hoja yake umejaa kejeli sasa watu kwann wasireply kejeli pia
 
Tunaona huko Uganda, pamoja na Museveni kutumia mbinu kama zile za ccm, Mugabe, Kagame, n.k ili kushinda uchaguzi bado tunaona wapinzani wanaleta amsha amsha baada ya uchaguzi kwa kwenda mahakamani. Hii inasaidia sana kuendelea kuviweka masikioni na akilini mwa wananchi vyama pinzani na hivyo kuvipa uhai zaidi.
Kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa! Upande wa bara, wakati matokeo ya urais yakiendelea kusomwa na tume tukaambiwa UKAWA haikubaliani na matokeo yanayosomwa. Na wakaiandikia tume waraka wa kuiomba isiendelee kuyasoma ili waweke utaratibu wa uhakiki manually. Tume ikatupilia mbali pingamizi lile na ikaendelea kusoma hadi mwisho. Matokeo ya mwisho yaliposomwa ukawa ikatoa tamko la kutokubaliana na matokeo na tukaambiwa itaenda ICJ kushitaki. Mpk leo jiiiiiiiii!!!!!....!!!!!!.
Hatuoni harakati zozote za kisiasa zikiendelea. Wafuasi huku mitaani wamekata tamaa na inaelekea hata viongozi wamekata tamaa. Ukawa inasubiria matukio ndipo wayavalie njuga. Bahati mbaya JPM anaonekana kuzuia kabisa matukio yatakayotoa kiki kwa upinzani. Hali hii itapelekea kifo cha ukawa kimya kimya.....!!
Kwa upande wa Zanzibar baaday ya uchaguzi kufutwa kwa tamko batili (kama ilivyoelezwa na cuf) la Jecha S. Jecha hatukuona siasa za hamasa zilizokuwa zikifanywa na cuf kuzuia ama kunusuru utimilifu wa tamko la Jecha. Zaidi tukaona Maalim Seif akicheza ngoma ya ccm ya kuingia peke yake kwenye mazungumzo ya kutanzua mgogoro wa kisiasa huku wanaccm wakiwa 5. Hii ilishangaza wengi. Iweje aende peke yake? Kwani ni mgogoro wa familia? Viongzi wenzake walikuwa wapi?
Sasa wamesusa uchaguzi ccm wamefanya yao na ulinzi madhubuti juu. Cuf kimyaaa!! Kimya hiki siyo tu kwenye majukwaa hata katika vyombo mahususi vya kutoa maamuzi hawatakuwepo. Hawatapata ruzuku. Chama kitakuwa na ukata.
Mikakati ya Kiza Besigye hatuioni. Mahakama hamuzioni? Najua mtasema tume za uchaguzi hazishitakiwi. Kwahiyo mnatumbiaje? Kwamba no way forward? Acheni siasa basi.
Kwa mikakati na mbinu hizi mbovu za vyama vya upinzani ccm itadumu. Maana ni kana kwamba mnasubiria siku ccm itawapa dola kama zawadi. Hilo halipo.
Chadema mmepoteza muelekeo wa misingi yenu ya kupinga ufisadi na hivyo mmepoteza imani kwa wananchi. Mtasema nn? Utamuambia nani akaandamane? Wakati wafia chama kama kina Dr. Slaa mliwanyanyapaa?
pengine ni hamu yako kuona hivyo lakin bahat mbaya hlo haliwez kutokea kwan hata kama chadema ikifa watakuja wengine na wengine na wengine yaan usije tarajia kwamba ipo cku itakuja tokea hapa tanzania hakutakua na chama cha upinzan chenye ushawishi mkubwa....kulikua na Nccr cuf na sasa chadema..vitakuja na vngne na vngene mkuu hadi mwishowe itakuja na CCM nayo itakua chama cha upinzan kizuri tu...upinzani hauwez kupotea kamwe
 
Bongo upinzani ni dhaifu na wakinafki

Sisi tunamchukia shein wao wanacheka tu
Shein, Maguful wameenda kumuona maalim seif wanacheka tu unafkir sisi tunachukuliaje
ni kweli mkuu but upinzan c vurugu,iko cku nguvu ya wananchi itakua kubwa zaidi yao hapatakua hata na justification za kurudia uchaguz....kwan mkuuu ni vyama vngapi vya ukombozi vilivyosalia madarakan mpk leo africa? hata hawa ccm wataondoka tu kama wenzao ni swala la muda tu
 
Tanzania rais akitangazwa huruhusiwi kupeleka kesi katika mahakama yoyote iwe duniani au mbinguni

CHADEMA Hawajawahi Kusema wanaenda ICJ
Yeriko Nyerere na G Malisa wakikusikia watakusuta.
Tena nadhani Malisa ndo alitoa ufafanuzi wa mahakama kuwa sio ICC bali ni ICJ
 
Bunge lisiporushwa live ndio kaburi la wapinzani, pia Magufuli amewaovataki, hawapi pass kama Mkwere,
 
Tunaona huko Uganda, pamoja na Museveni kutumia mbinu kama zile za ccm, Mugabe, Kagame, n.k ili kushinda uchaguzi bado tunaona wapinzani wanaleta amsha amsha baada ya uchaguzi kwa kwenda mahakamani. Hii inasaidia sana kuendelea kuviweka masikioni na akilini mwa wananchi vyama pinzani na hivyo kuvipa uhai zaidi.
Kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa! Upande wa bara, wakati matokeo ya urais yakiendelea kusomwa na tume tukaambiwa UKAWA haikubaliani na matokeo yanayosomwa. Na wakaiandikia tume waraka wa kuiomba isiendelee kuyasoma ili waweke utaratibu wa uhakiki manually. Tume ikatupilia mbali pingamizi lile na ikaendelea kusoma hadi mwisho. Matokeo ya mwisho yaliposomwa ukawa ikatoa tamko la kutokubaliana na matokeo na tukaambiwa itaenda ICJ kushitaki. Mpk leo jiiiiiiiii!!!!!....!!!!!!.
Hatuoni harakati zozote za kisiasa zikiendelea. Wafuasi huku mitaani wamekata tamaa na inaelekea hata viongozi wamekata tamaa. Ukawa inasubiria matukio ndipo wayavalie njuga. Bahati mbaya JPM anaonekana kuzuia kabisa matukio yatakayotoa kiki kwa upinzani. Hali hii itapelekea kifo cha ukawa kimya kimya.....!!
Kwa upande wa Zanzibar baaday ya uchaguzi kufutwa kwa tamko batili (kama ilivyoelezwa na cuf) la Jecha S. Jecha hatukuona siasa za hamasa zilizokuwa zikifanywa na cuf kuzuia ama kunusuru utimilifu wa tamko la Jecha. Zaidi tukaona Maalim Seif akicheza ngoma ya ccm ya kuingia peke yake kwenye mazungumzo ya kutanzua mgogoro wa kisiasa huku wanaccm wakiwa 5. Hii ilishangaza wengi. Iweje aende peke yake? Kwani ni mgogoro wa familia? Viongzi wenzake walikuwa wapi?
Sasa wamesusa uchaguzi ccm wamefanya yao na ulinzi madhubuti juu. Cuf kimyaaa!! Kimya hiki siyo tu kwenye majukwaa hata katika vyombo mahususi vya kutoa maamuzi hawatakuwepo. Hawatapata ruzuku. Chama kitakuwa na ukata.
Mikakati ya Kiza Besigye hatuioni. Mahakama hamuzioni? Najua mtasema tume za uchaguzi hazishitakiwi. Kwahiyo mnatumbiaje? Kwamba no way forward? Acheni siasa basi.
Kwa mikakati na mbinu hizi mbovu za vyama vya upinzani ccm itadumu. Maana ni kana kwamba mnasubiria siku ccm itawapa dola kama zawadi. Hilo halipo.
Chadema mmepoteza muelekeo wa misingi yenu ya kupinga ufisadi na hivyo mmepoteza imani kwa wananchi. Mtasema nn? Utamuambia nani akaandamane? Wakati wafia chama kama kina Dr. Slaa mliwanyanyapaa?
Aisee mkuu you deserve a bottle of Wine. Salute and much respect..
 
Duh.! Umeandika Kwa uchungu sana, kiukweli vyama vyetu vya upinzani havina siasa mbadala zaidi ya kucheza midundo ya ccm.!
Kama havina siasa ni kwa nini CCM inatumia kila mbinu chafu kuvikabili? Hapa Iringa Mbunge wa viti maalum CHADEMA, Rose Kamili alitekwa na kupelekwa kwenye Ofisi za CCM ambako ndiko polisi walikwenda kumchukulia mbele ya viongozi wa CCM na mpaka sasa serikali imeshatumia zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumtibia, kama ni dhaifu huo utekaji ulifanywa kwa madhumuni gani?
 
Mkuu kwa vile CCM hawataki kuondoka madarakani kwa njia ya kidemokrasia basi nadhani kuna haja ya mabadiliko ya dhana nzima ya upinzani hapa Tanzania. Umefika ule wakati ambapo Wapinzani sasa wafuate kwa vitendo zile sera za Jino kwa jino.
 
Kama havina siasa ni kwa nini CCM inatumia kila mbinu chafu kuvikabili? Hapa Iringa Mbunge wa viti maalum CHADEMA, Rose Kamili alitekwa na kupelekwa kwenye Ofisi za CCM ambako ndiko polisi walikwenda kumchukulia mbele ya viongozi wa CCM na mpaka sasa serikali imeshatumia zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumtibia, kama ni dhaifu huo utekaji ulifanywa kwa madhumuni gani?

Sijaona ccm wakitumia nguvu kubwa kuukabili upinzani, Ila nimeshuhudia ulaini wa matamko ya viongozi wa upinzani.
Na sidhani Kama wapinzani wa Tanzania wanaweza kujifanisha hata nusu ya uwezo wa wapinzani wa Uganda ambao mpaka Leo wako Chini ya ulinzi, lakini bado hawaishi kwenda mahakamani.

Tuambie na huyo mama Rose Kamili aliumizwa nini mpaka matibabu yake yafikie million miambili fedha za walalahoi wa Tanzania, nikisema huo nao ni sehemu ya ufisadi kwa wapinzani utabisha?
 
Kwani serikali inayolipia hayo matibabu iko chini ya wapinzani. Kwa nini fedha itolewe na serikali inayoongozwa na CCM ufisadi uwe ni wa wapinzani? Badala ya kuuliza Rose Kamili alifanywa nini jiulize hao waliomfanya nini wamefanywa nini mpaka sasa!?
 
Kama havina siasa ni kwa nini CCM inatumia kila mbinu chafu kuvikabili? Hapa Iringa Mbunge wa viti maalum CHADEMA, Rose Kamili alitekwa na kupelekwa kwenye Ofisi za CCM ambako ndiko polisi walikwenda kumchukulia mbele ya viongozi wa CCM na mpaka sasa serikali imeshatumia zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumtibia, kama ni dhaifu huo utekaji ulifanywa kwa madhumuni gani?
Duh,hawaku ng'oa kucha!?
 
Back
Top Bottom