Kwa miaka mingi siasa za Tanzania ndo ziko hivi

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Ni kwamba, kama kuna issue serious sana Bungeni kuhusu jambo fulani huwa kuna mikakati maalumu kabisa. Kwa mfano, kama kuna Mbunge ambaye ni wa upinzani na anaonyesha kuwa knowledgeable katika jambo hilo mara nyingi huja mbinu fulani na huondolewa Bungeni.

Haya yalifanyika sana tangu wakina Zitto wakiwa wanapinga mikataba mibovu ya madini na wakina Lissu. Hili la leo la J J Mnyika ni mikakati ya kisiasa. Ni dhambi kubwa ambayo tumeifanya miaka mingi na hatuwezi kuiacha. Mnyika ni Waziri Kivuli wa Nishati na madini, leo ameondoshwa bungeni kwa hiyo mtu mojawapo muhimu sana mwenye uelewa zaidi katika sekta ya Madini kutoka upinzani hatakuwepo kwenye mjadala.

Hizi ndo siasa za miaka na miaka. Mtu akipinga mikataba mibovu huyo huyo anawajibishwa na tumeyaona sana. Leo hii mtu katamka eti Mnyika mwizi wa Madini na Mnyika akasisitiza hiyo kauli ichukuliwe hatua na Spika naye bila kutafakari kwa kina akajaa na mchezo ukaisha baada ya Mnyika kutolewa nje na kuzuiwa kuhudhuria vikao kadhaa. Mwisho mnasema eti tunaibiwa madini wakati watu wanaotetea ukweli hamuwataki kuwasikia miaka yote.
 
Spika huyu ndiye aliyempiga wenzake bakora jimboni. What level of integrity one would expect from such a person.
 
Back
Top Bottom