Kwa mfano itokee mtake kuandamana mtapata wapi watu?

Kwa mfano itokee mtake kuandamana mtapata wapi watu?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,669
Reaction score
57,082
Swali hili Ni kwa wapinzani nawauliza.zamani za chadema ya dk slaa mlikuwa mna uwezo wa kutangaza tu maandamano na kweli watu hata bila kuwaratibu wakajitokeza kwa wingi.Je kwa Sasa mtapata wapi watu kwa sababu mimi napopita mitaani naona yafuatayo
1.watu wako busy kutafuta fedha za kuendesha maisha ukija ukiwaambia muandamane watakudharau Ni Kama vile unawamaliza nguvu zao tu
2.wanaomkosoa Magufuli Ni Kama vile wanamkubali kimya kimya moyoni unakuta mtu anasema Magufuli kabana Ila ndo vizuri heshima ya pesa imerudi
3.watu wameshagundua kwamba Magufuli hatawaletea chakula au hela Kama wasipojishughulisha.. watanzania wameacha kujipotosha au kupotoshwa kwamba Rais atakuletea pesa mlangoni Ni lazima uchape kazi na ndo maana mitaani huku biashara zinazidi kushamiri watu wanatembeza vitu na wanauza.
4.magufuli anafurahisha na kuchekesha.hotuba zake hata kama ulikuwa umenuna utajikuta umecheka kwa hiyo anapendwa Sana watu hawawezi kwenda kuandamana na Kama mpo hamfiki hata million 2 Tanzania yote
 
Back
Top Bottom