issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,788
- 5,217
WEDNESDAY, APRIL 27, 2016
Kwa madudu haya, tunahitaji kuwa na ATCL?
Kwa ufupi
CAG amebainisha kuwa kampuni hiyo ya ndege iliingia mkataba na kampuni ya Wallis Trading Co. Limited kukodi ndege aina ya Airbus A320-214 Oktoba 2007 ambao haukufuata taratibu muhimu na rasmi za uendeshaji wa kampuni.
Hali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ni mbaya kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubainisha ufisadi mkubwa.
Mmoja ya ufisadi huo ni hatua ya ndege moja ya kukodi kugharimu zaidi ya Sh90 bilioni huku ikifanya kazi kwa miezi sita tu.
Ripoti ya CAG, Profesa Musa Juma Assad, iliyotolewa juzi, inaeleza kuwa hadi sasa ATCL haina mkakati mahsusi wa kujifufua katika mpango mkakati wake wa 2015 hadi 2020 na kwa zaidi ya miaka tisa, imekuwa ikipata hasara ya mabilioni ya shilingi.

Mkataba huo uliitaka kampuni hiyo ya ndege kuilipa Wallis Dola 370,000 za Marekani kwa mwezi kwa ajili ya malipo ya kukodi chombo hicho cha usafiri chenye uwezo wa kubeba abiria 150.
Wakati mkataba huo ukifanyika, ATCL ilikuwa na miezi michache baada ya Serikali kurudisha asilimia 49 ya hisa zilizokuwa zimeuzwa kwa Shirika la Ndege Afrika Kusini (SAA) kama sehemu ya kutekeleza ubia katika sera za ubinafsishaji.
Shirika hilo la Ndege lilianzishwa mwaka 1977 likiitwa ATC baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Awali, ATC ilikuwa inamilikiwa na Serikali, kabla ya mwaka 2002 kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini lililokuwa likimiliki hisa 49, ingawa mwaka 2006, Serikali inunua hisa zote.
Leo, hakuna anayeweza kutoa maelezo ya kuridhisha kwamba Tanzania imebakiwa na ndege mbili tena moja ikiwa mbovu.
Wakati ATCL ikiwa katika hali hiyo, majirani zetu Rwanda wana ndege nane ambazo zinafanya safari za ndani na nje. Rwanda Air ambayo ilianzishwa miaka 14 tu iliyopita, tayari imeagiza ndege nyingine tatu mpya na mipango ya kuanza safari za kwenda India, China, Ivory Coast, Cameroon, Zimbabwe na Sudan zipo katika hatua za mwisho.
Kuna mfano mwingine wa Shirika la Ndege la Emirates lililoanzishwa mwaka 1985 likiwa na ndege mbili tu huku likifanya safari zake za ndani. Wakati huo, Tanzania tayari ilikuwa na zaidi ya ndege sita ambazo zilikuwa zinafanya safari za ndani na nje ya nchi lakini leo tumerudi nyuma tuna ndege mbili.
Ni linaloumiza kichwa na hasa ukizingatia kuwa mashirika mengine ya nchi jirani kama Kenya Airways (KQ) ambalo linashindana na Fly Emirates na mashirika mengine makubwa ya kimataifa, yanakua na yanapata faida pia.
Fly Emirates inamilikiwa na Serikali ya Dubai na ina zaidi ya ndege 300 ambazo zinasafiri katika nchi 78 katika mabara yote sita duniani. Nini kimewafikisha hapo? Bila shaka ni umakini na ubunifu wa menejimenti yake na kujiendesha kutokana na matakwa ya mahitaji ya wakati husika.
Hata hivyo, tunapaswa kujiuliza maswali kadhaa, kama kwa miaka zaidi ya 40 tumeshindwa kuliweka shirika hili katika ushindani wa kutoa huduma ya usafiri je, tutaweza sasa wakati tayari anga limeshikwa na mashirika ya ndege yenye majina makubwa?
Pia, tunapaswa kujiuliza, hivi Watanzania kipaumbele chetu sasa ni kuwa ndege au kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji binafsi kuanzisha mashiriki ya ndege? Je, tumejiuliza tatizo ni nini kiasi kwamba nchi jirani zinafanikiwa, lakini kwetu imekuwa ni tatizo kiasi kwamba kila ripoti ya CAG inapotoka imekuwa ikigusia uozo wa ATCL.
Kabla ya kufanya uamuzi ama wa kufufua shirika hilo la ndege au kulifuta, ni muhimu kufanya utafiti wa kina kwa kuangalia jinsi wenzetu wanavyojiendesha ili tujue kama kuna tija ya kuwa na shirika hilo au vinginevyo.
Chanzo: Mwananchi