Kwa maamuzi haya ya tume kwanini mkurugenzi wa Kyerwa asiwajibishwe kuonesha utawala?

jeremiahy

Member
Oct 7, 2015
42
23
Habari za jioni wakuu,

Mkurugenzi halimashuri ya Kyerwa kwa kuufahamu ukweli pamoja na kuaminiwa na chama CCM alilazimisha kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa mshindi ambapo ni dhahiri hakushinda na kumpokonya mshindi wa kweli Benedict Mtungireh.

Huyu huyu alituma matokeo ya udiwani tume ya uchaguzi kuwa CCM imeshinda kata 13 na CHADEMA kata 11, na ukweli ni kuwa CHADEMA ndiyo walioshinda kata 13 na CCM 11. Hili amekiri mwenyewe kuwa alisahau.

Hivi huyu kiongozi kwanini asiwajibishwe kukidhi haja ya utawala bora na kurejesha amani inayotoweka kwa kasi kwa wakazi wa Kyerwa?

Baada yakufanya masudu yote alijipa likizo na kuna tetesi kubwa kuwa anatumiwa na wakwepa kodi wa huko waliojivika miamvuli wa viongozi wa chama tawala.
 

Attachments

  • Screenshot_2015-12-24-19-20-17.png
    Screenshot_2015-12-24-19-20-17.png
    48.1 KB · Views: 191
Alikuwa anaamini kuwa zama za 'maisha bora kwa kila mtz' zingeliendelea, hadi sasa atakuwa keshajua kuwa #hapakazitu!
 
na limeathiri matokeo ya uchaguzi wa mwenywekt wa halimashauri.na je kuna uwezekano wa kupinga uchaguzi huo mahakaman? kwa wabobezi wa sheria naomba ufafanuzi,
 
Back
Top Bottom