philosophy
Senior Member
- Nov 11, 2012
- 104
- 42
BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI TZ VINALINUFAISHA NINI TAIFA NA WATANZANIA?
Ni swali ambalo kwa mtu ambaye analitizama kwa juujuu anaweza kuniona sina nachomanisha ila kwa wle wenye jicho lingine la ziada la kuangalia mambo kwa undani wanaweza kukubaliana nami kwa kile nachoongelea. Hili ni wazo ambalo nimelifikiri na nikaona kuwa laweza kuwa bora kuliweka mbele ya watanzania.
Ni baada ya serikali kutangaza kuvifungia baadhi ya vyombo vya habari vitatu hivi karibuni; nimeona serikali walifanya vema kufanya hivyo kwani, vimekuwa vikiendesha baaddhi ya vipindi ambvyo ukweli vingeondoa amani ya nchi hii. Lakini hatoshi serikali yetu imechelewa sana ijapo vyombo hivyo vimefungiwa, kuna baadhi ya vyombo ambavyo kwavyo ukisikiliza baadhi ya vipindi vyao hakika havina manufaa kwa maisha ya sasa ya mtanzania wa leo ambeye kwa wakati mwingine anahitaji msaada wa vyombo hivyo kuweza kupanuka mawazo na kuelimika hata kuelewa yanayoendelea katika nchi hii
.
Mathalani kuna vyombo vya habari ambvyo vipindi vyake utakuta kwa siku kama ni televisheni, wanashinda wanapiga miziki, wanaoneha filamu zisizo na maadili ya kitanzania, vipindi vya mahaba wakisingizia kuwa eti vinaendeshwa usiku, wakishindwa kufikiri na kuelewa kuwa kuna baadhi ya watoto ambao ambao ni wanafunzi wanakuwa wanasoma wengine au pia wanasimu hata kama wakifukuzwa na wazazi wao kulala wanakuwa wanasikiliza peke yao kitandani, pia ndivyo ilivyo kwa wanafunzi wa bweni.
Hii inamaanisha au inaoneha picha gani kwa kizazi cha sasa na kijacho? Kuharibika kwa vizazi hivi, vyombo vya habari baadhi haviepukiki lawama hii.
Sio hilo tu, pia kuna vipindi kama XXL- kipindi ambacho huzungumzia juu ya maisha ya mastaa wa bongo: pia kipindi kama MIKASI ambacho nacho pia huzungumza na baadhi ya wasanii wa bongo na masta wengine; kimsingi mahojiano hayo huwa hayana mantiki yoyote.
Mfano mtu anulizwa na mwandishi au mtangazaji kuwa umeishaoa? Au una mke/mpenzi? Ama ulishwawahi kufanya mapenzi? Mara yako ya mwisho kujamiiana ni lini? hakika vipindi kama hivyo kimsingi haviwasaidii watanzania wa sasa! Ki ukweli serikali itazame kwa jicho la ziada katkia media za namna hii. Kuvunjika kwa maadili kunaanzia huko. Vyombo vya habari uchwala kama hivi vilistahili vifungiwe au vifutiwe usajili mapema. Chombo cha habari chenye uchungu na maendeleo ya nchi yetu hakiwezi kushinda kila mda eti vipindi vyake ni miziki tu, na miziki yenyewe ni ile ya kupotosha kizazi cha sasa.
Zaidi ya hayo, ukifuatilia kwa undani zaidi utagundua kuwa hata waandishi au watangazaji wa media hizo hawana taaluma ya kutosha, wanajifanya ni washauri wakati hawana hata ujuzi wa ushauri. Mwandishi bila aibu anaamua kudiriki kutamka maneno kama kwa taarifa zisizo rasmi kitu fulani kiko hivi na hivi wakiamini kusema hivyo wanajikinga na lawama, sawa nikweli!
Lakini, mwandishi/mtangazaji mwenye taaluma bora sio tu kipaji hawezi kutamka maneno kama hayo, huwezi kusema kwa taarifa zisizo rasmi, hii sio kauli ya kimaadili ya ueledi wa taaluma ya habari. Chukulia umefanya hivyo, jamii inayoenda kupokea taarifa hiyo ni watu wa nama gani kuna makundi yapi ya watu wenye uwezo wa kuitafakari na kuielewa kauli hiyo, mathalani ikileta uchochezi kwa jamii na jamii ikafanya vurugu, sakata kama hilo mwandishi aliyetoa kauli hiyo anaweza kusululisha hilo kama yeye?
Lakini haya yote yanatokana na baadhi ya wakurugenzi watendji wa vyombo hivi vya habari hivi, kutamka kuwa wanatafuta vipaji vya watangazaji. hii sio sahii kwani kipaji tu sio tosha kwa mtu kufanya kazi hii, hapo hakuna kubobea( PROFFESIONAL). Baadhi ya media hazishutuki hata kidogo, kuandika habari za udaku kila siku.
Watanzania wanakufa kwa njaa, wanahangaika na shida mbalimbali,maafa yanatokea lakini unakuta gaziti lnaandka habari kama Kanumba kafa sababu ya freemason, kigogo kakutwa na mke wa mtu, sijui diamond kaachana na nani n.k. Lakini kama haitoshi baadhi ya watangazaji huongea mambo kwa kuegemea mawazo yao wenyewe tu sio ukweli wenyewe, pia waandishi na watangazaji hupotosha umma kutokana na mapenzi yao binafsi kwa mambo wanyoengelea. Hakika vitu kama hivi havipaswi kupewa nafasi katika jamii yetu. Kwani jamii haiwezi kuendelea kwa umbe kama huu. Watanzania tuwe macho sana na vyombo vya habari kama hivi, na serikali iwe makini juu ya vyombo kama hivi,kwani sio vya kuachia nafasi.
Yangu ni hayo tu kwa leo!