Kwa kiasi kubwa kelele za huyu jamaa ndio zilimuangusha Sepp Blatter, nasasa kalianzisha kwa Trump

mxyo16

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
1,243
758
john Oliver,
Huyu jamaa kwa kiasi kikubwa aliuweka uwazi ufisadi wa FIFA mpaka kuelekea anguko la Sepp Blatter, alielezea jinsi maofisa wake wakuu wanavyopiga fedha kutoka makampuni ya matangazo, ununuaji wa kura kutoka vyama kutoka nchi masikini, kurithishana vyeo ndani ya FIFA kuendeleza upigaji, kupokea rushwa upangaji wa nchi waandaaji mashindano makubwa kama world cup nk.

Leo amemuongelea Donald Trump, upande ambao wengi nadhani hatujausikia kimpangilio huu...Kwamba ingawa Trump anasema utajiri wake upo kwenye dola bilioni 10, wataalamu wanasema yupo kwenye dola milioni 250 - 300.
Anavyojitapa ni successful business man, hapana kuna maeneo mengi sana kapata hasara, na kwamba alirithi millions kutoka kwa baba yake kwahiyo sio mpiganaji kama anavyojinadi.

jamaa kataja vitu vinavyowavutia wafuasi wengi wa Donald wanachompendea na kuelezea ukweli kuhusu kila anachopendewa kwamba si sahihi kwa facts alizokusanya.

Nimecheka lingine kwamba jina lao la ukoo Trump lilibadilishwa ku sound good tu, kutoka jina lao halisi kiukoo Drumpf....hili limesemwa kwani kinachoonekana anauza zaidi katika kampeni ni sound ya jina (brand) tu lakini sio policies,
Jamaa pia katoa maeneo mengi ambayo Trump kawa kigeu kigeu kimsimamo; Kuhusu wahamiaji, guns control, uzazi wa mpango....
Jamaa ni kichwa fulani hivi katika comedy msikie...

 
Hahahahhahhhahha yaani sichokagi kuangali
Hii show. John Oliver one of the kind.

Kamvaa Trump kweli kweli .
 
Sure, nadhani inajulikana kwamba the coming super Tuesday akishinda tu ndio basi tena kaukwaa u-nominee na probably urais pia.
mkuu hivi kweli Trump anaweza kuwa rais wa Marekan kweli. Dah hii maqi2 inantisha sana
 
mkuu hivi kweli Trump anaweza kuwa rais wa Marekan kweli. Dah hii maqi2 inantisha sana
Wakiweza kumuanika kwamba ni msemaji tu nasio mtendaji kama ukiicheki hii attached video vizuri..anaweza apate nomination lakini aisiwe president....mpaka sasa anavutia wengi kwa kujionesha yeye ni best na successful sales man katika kundi...Majuzi haku fair well kwa Rubio.......
Pia tatizo kubwa hao wanaomfatia kwenye polls Rubio na Cruz bado hawa appeal kwa wengi hawajaweza ku throw power punches kuvutia wengi....record zao za kumpinga Obama nadhani zinawatafuna.
huyu jamaa alivyolianzisha hivi, nadhani itamuumiza trump kwenye general election na kushindwa iwapo atakua nominee
 
Jamaa kamchana mnooo hatare
na ndivyo alivyoichana FIFA kwa style hii segment tatu, ndio tukasikia FBI, na yule AG wasasa wakavamia wahusika walio US, then Swiss na mpaka sasa tuna rais mpya FIFA
 
Hivi hizi calculation za utajiri wa trump mbona zinachanganya,kama anamiliki tower yenye thamani ya karibia 1b inakuaje awe na net worth ya 200m?
 
Kilichofanyika ni set up tu
ili Hillary awe Rais...

Wale Republicans die hard kwa pesa na mbinu Hillary asingeshinda
sasa 'wale watu behind powers' walichofanya kwa kupitia media ni kuinfluence tu ili Trump awe nominee wa Republican..
halafu waanze kumpasua vipande vipande Hillary ashinde kiurahisi
hii ndo imeanza sasa...taratiibu
 
Hivi hizi calculation za utajiri wa trump mbona zinachanganya,kama anamiliki tower yenye thamani ya karibia 1b inakuaje awe na net worth ya 200m?
Kama nimemuelewa vizuri jamaa kwenye video anasema kuna mradi wa ujenzi wa magorofa uli-fail zimeonyeshwa sites na plans na alikua kachangisha watu, sasa inawezekana jamaa ni mzuri kwa upatu pia....
Ngoja tusubiri aisee hizi ni shutuma kubwa na ni kwenye tv ya kitaifa, kuna mengi yataibuka...kama the boss hapo juu anasema hii ni set up na muda umefika wanaanza kumkaanga kumnyooshea barabara ya urais madam clinton...

Majuzi walimuuliza mbona huoenyeshi tax returns zako! akajibu bado IRS wanamu-audit....IRS nasikia wakaguna...sasa limeibuka hili...tutasikia mengi aisee
 
Kilichofanyika ni set up tu
ili Hillary awe Rais...

Wale Republicans die hard kwa pesa na mbinu Hillary asingeshinda
sasa 'wale watu behind powers' walichofanya kwa kupitia media ni kuinfluence tu ili Trump awe nominee wa Republican..
halafu waanze kumpasua vipande vipande Hillary ashinde kiurahisi
hii ndo imeanza sasa...taratiibu
dah! fitina hizi aisee...kweli dunia hii inawenyewe.....au na trump yumo kwenye set up, ni kweli asilijue hili zengwe, sababu kwenye analysis ya kwenye video Trump kasema katumia $24millions kwa kampeni, na kumbe ameikopesha team inamana atakuja kuzidai kwa election commission , pia donors wamechanga $7m....meaning haja spend that much money kama anavyojitapa na kupata ujiko kwamba anatumia hela yake....kachanwa kweli hapa....
 
Back
Top Bottom