Kwa kiasi kikubwa hili ndilo tatizo la watanzania

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
583
Wakati tukitafali hali ya mambo mbalimbali hapa nchini chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli. Kuna mambo ambayo kama watanzania hatutotaka kuyafanyia kazi basi tutakwama kwenye lindi la umasikini siku hadi siku hata Rais Obama aliyemaliza muda wake wa kutawala huko Marekani akija kuwa Rais wetu nasema hakutakuwa na hatua zozote za kimaendeleo zitakazopigwa kutokana na watu tulio nao kwenye kile tunachokiita wasukuma maendeleo ya nchi nyenzo hii tuliyonayo( watu)kiasi kikubwa ni butu haiwezi hata kutusaidia kupiga hatua.

Watanzania walio wengi leo hii hawafahamu kile kinachoitwa busara ndogo za binadamu yaani uwezo wa kufahamu nini unataka na nini hautaki , kutokana na kutokulifahamu hilo mamilioni ya watanzania hawana mchango katika nchi yao kwani kwa kiasi kikubwa wamebaki kuwa watazamaji wa mambo yanayotokea na kuwa wasilimuliaji.

Tatizo kubwa watanzania ambalo tunalo na mara nyingi limetuletea matatizo ni kuishi na UJINGA yaaani hali ya kutokutaka kujifunza mambo kwa maana ya kupokea elimu ujinga umekuwa sehemu ya maisha yetu , tunapenda hata tuitwe majina yetu kwa ubini wa UJINGA hali hii haitaweza kulikwamua Taifa hili sasa ni muhimu Watanzania tukaacha kuishi na ujinga na tuone kuwa ujinga ndiye adui wetu wa kwanza na si serikali , chadema , CCM, CUF, ACT ,bali ni tabia yetu ya kijinga ya kukumbatia ujinga .
ona mifano ya matukio kama haya

1.Mkulima kulima chakula na kuuuza chote bila kuacha akiba,

2. wafugaji kufuga mifugo mingi yenye kuleta adha kwenye jamii ya kula hata chakula cha mfugaji huyo huyo.

3. Wanasiasa kutumia matatizo ya wanaichi kama mitaji mikubwa ya kisiasa na kwa kiasi chake sasa hata wanaweza kuyatengeza matatizo na kuja kuyatatua na wanainchi hao hao wanawashangilia

4. kufanya maamuzi bila ya kuwa na elimu ya maamuzi kiasi kwamba hupelekea maamuzi hayo kukua / kukufunga

5.Wazazi kupeleka watoto wengi shuleni eti kwa sababu ya ada ya shule kufutwa kwa maana hiyo Rais Jonh asingekuwepo kuna mamilioni ya watoto walikuwa hawapelekwi shule.

6.Sera za nchi kutungwa na wasio tatizo la umuhimu wa sera hiyo na ukiwaita wenye umuhimu wa sera hiyo hawaji wanataka posho.

7. Rais kuwauuliza wananchi wanataka nini na wao wakamjibu wanataka akae nao tu , akawauliza tena nikae nyie kwa muda gani wananchi wanajibu ukae tu, Rais kwa huruma ya kujua hawa hawajui nini wanataka kutoka kwa Rais wao anawaagizia karanga , na ndizi za elfu tano .....hii ni mbaya sana
Haya ni baadhi ya matunda ya KUMILIKI UJINGA KAMA SIRAHA YA KUMUUA ADUI KUMBE INAKUUA WEWE MWENYEWE KABLA HATA YA ADUI KUTAKA KUKUUA.
hqdefault.jpg
 
Back
Top Bottom