Nyamsusa JB
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 567
- 1,564
Kama tunavyoshuhudia Kasi ya Magufuli katika kudhibiti Ukwepaji wa kodi unaofanywa na Wafanyabiashara Wakubwa na wale wa Kati ni dhahiri kuna baaadhi ya Bidhaa zitapungua Nchini.
Kichochezi kikubwa(Motive) kwa Wafanya Biashara wengi Nchini kilikua ni uwezo wao wa kukwepa kodi na wala sio Faida tu ipatikanayo kwenye Biashara hizo. Biashara ambazo zilionyesha Mianya ya ukwepaji Kodi ndizo zilifavutia zaidi wafanya biashara wengi.
Sasa kutokana na Mh Raisi Pombe kufunga Mianya mingi ya ukwepaji wa kodi kuna uwezekano mkubwa Wafanya Biashara wengi wakajitoa katika biashara hizo kutokana na Ukweli kwamba wao waliingia katika biashara hizo kwa kua wangeweza kukwepa Kodi na kujizalishia Faida mara dufu.
Wafanya Biashara wengi hawapendi kufanya Biashara ambazo haziwezi kukwepa Kodi, wanadai Biashara nzuri ni ile yenye mianya ya kukwepa Kodi.
Kufuatia Ufafanuzi hapo juu Watanzania tujiandae na Upungufu wa Baadhi ya Bidhaa zilizokua zikizalishwa ama kusambazwa na Wafanya Biashara hawa waliotegemea Faida Kubwa ya Kukwepa Kodi.
Bidhaa nyingi zitakazo adimika zaidi ni zile zilizoletwa kutoka nje ya Nchi kwani kwa kiasi kikubwa ndizo zilizokwepa kodi na kuwavutia Wafanya Biashara wengi Nchini.
Kutokana na hili huenda Bei ya Bidhaa hizo husika zikapanda kutokana na Upungufu wa Bidhaa hizo.
Pia watakaodhurika zaidi ni wale watu ambao walitegemea Bidhaa hizo kuendeshea Maisha yao.
Mfano wa Makundi yanayoweza Kudhurika na Mabadiliko haya ya Ulipaji wa Kodi ni pamoja na :-
1. Waendesha BodaBoda ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea Spare zinazoletwa na Wafanya Biashara hawa Wakwepa Kodi
2. Wauza Nguo zitokazo Nje ambazo pia kwa kiasi kikubwa ziliingia Nchini kwa Kukwepa Kodi.
Asanteni.