KIUNGOMCHEZESHAJI
Senior Member
- Oct 4, 2013
- 120
- 254
Ile misemo mizuri na mitamu kama asali kuhusu ndoa kwangu ni kama hadithi fulani hivi. Wakati naingia kwenye mahusiano ya ndoa nilikuwa very optimistic, sasa hivi nimenywea, sina hamu tena.
Mwaka 2007, mke wangu alikuwa mjamzito kwa mtoto wa kwanza, na wakati huo nikapata kazi ya kuajiriwa mkoa wa mbali na nyumbani. By then hatukuwa na msichana wa kazi. Nikaona kwa situation ile, itabidi tuu niwe na msichana wa kazi. Tuliposhauriana mwenzangu akaniambia nimtafute mimi kama nitampata kwetu. Nilimkosa, ila kulikuwa na mtoto wa kaka hakubahatika kwenda sekondari, kaka akaniambia nimchukue tu kama namhitaji kwa malengo kuwa hapo baadaye nimtafutie hata ufundi veta au shule ili ajiendeleze. sikuona ni tatizo.
Nilipomchukua, ikawa yule binti anakorofoshana na mke wangu. Mke wangu akawa anakuja kumshitaki, huku analia sana. Nilipoona issue itakuja kunivunjia ndoa nikamrudisha yule binti nyumbani ili nimsaidie shule huko huko nyumbani. Nikamwambia mke wangu sasa na yeye amtafute wa huko kwao, ikashindikana. Nilipofika nyumbani, mara dada yangu akaning'ang'ania nimchukue binti yake. Nikamwuliza wife akasema bora nije naye tuu maana hakuna namna. Nilimchukua huku rohoni sina amani. Tulikaa hata mwaka haukuisha mambo yakawa yale yale. Nikamrudisha tena. Nikagoma kumtafuta mwingine, nikamwambia mke wangu kama hataki kumtafuta basi tuache.
Akampata wa huko kwao ndo akamleta. Sasa huyu binti ni mkorofi afadhali hata wale wa ndugu zangu, ila mke hataki kumwondoa, anasema atapambana naye. Nikiona mapungufu au uzembe wowote pale nyumbani, nikimwambia mke wangu anasema yeye hahusiki nimwulize binti.Yanai yeye anaona mimi ndo niwe namuamrisha binti wa kazi, badala ya yeye. Nimegombeza mpaka nimechoka wakati mwingine napata hasira za kushusha mkong'oto. Mathalan, inakuwaje binti wa kazi anaamka saa 12 na nusu wakati mimi saa moja kamili natakiwa kuripoti kazini? Maandalizi ya watoto kwenda shule na kupasha maji ya kuoga yatafanyika saa ngapi? Kila siku ugomvi na dereva anayewapeleka watoto shule kwa sababu ya uzembe. House girl anachelewa kuamka na mke naye anachelewa kuamka, wote wanaviziana nani atangulie. Kazini kwangu siyo mbali na nyumbani kiasi kwamba lunch naenda nyumbani mara nyingi, lakini inakuwaje chakula cha mchana hakijawa tayari mpaka saa tisa mchana? Nikila huko kazini kwenye restaurant hataki, anasema hizo hela unazoteketeza huko si tuboreshe hapa nyumbani, lakini naenda nyumbani alafu narudi sijala? Siku zingine nakuwepo nyumbani mpaka saa mbili asubuhi au saa tatu lakini hata chai haiandaliwi, naondoka empty stomach, wakati mahitaji yote yapo nyumbani. Nikimwuliza mke wangu anasema numwulize housegirl. Siku nyingine nanunua matunda mengi ndani lakini hata yanaweza kuozeana ndani, chakula kikipangwa, nisipouliza matunda hayawekwi, ila baada ya siku mbili utakuta ndizi zimeozeana ndani, parachichi zimeshakuwa rojo, wakati siku mbili zimepita matunda hayajaliwa ndani.
Kuna kipindi nilimnunulia simu kama motisha tuu afaye kazi kwa bidii, kumbe ndo ikawa nimemrahisishia ufuska wake, akawa anawachanganya wanaume. Siku moja nikazipata stori mtaani, nikaja kuifuma simu yake, anadate na wanaume kama wanne hivi. Nikataka nimtimue, mke wangu anamkingia kifua. Nikasema ataondoka, yeye anasema haondoki. Anyway, nina mengi moyoni, mengine hata nashindwa kuandika hapa. Natamani tu niwe nachelewa kurudi nyumbani nikifika nikute wamelala.
What can i do jamani haya maisha gani? Hivi nikipiga si nitashtakiwa.