Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Wakati natazama taarifa ya habari jana kilingeni gafla mayowe yalipigwa hii ni baada tu ya Mhe.Edward Ngoyai Lowassa ambaye pia alikuwa mgombea Urais wa CHADEMA kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kusimama na kuzungumza akiwashukuru Watanzania waliomuunga mkono na kutanabaisha hatua zake za kitaifa katika kuhimiza amani na utulivu katika nchi.
Pamoja na mambo mengine, Mhe.Lowassa alidai kuwa alikuwa akipigiwa simu na vijana, marafiki na watu mbalimbali huku wengine wakidai kuwa tayari kuingia barabarani lakini alitumia utashi wa kisiasa kutuliza hisia za wafuasi. Kauli ya Mhe.Lowassa imepokelewa vyema na kwa mara nyingine leo nimejaribu kuchunguza na kugundua kwamba watu wengi bado wanamuona Mhe. Lowassa kuwa tunu kubwa kwa amani na utulivu wa nchi.
Hii ni kwasababu kwa ushawishi alionao angeweza kuitumia vibaya nafasi yake lakini badala yake alijitambua kwamba ana dhamana kubwa ya maisha ya vijana na amani ya nchi kwa ujumla. Huu ni uzalendo wa hali ya juu kuwahi kuonyeshwa na kiongozi wa upinzani barani Afrika. Naamini kwamba nafasi na ushawishi wa Mhe.Lowassa ungeangukia katika mikono kama ya Dr.Slaa bila shaka damu za vijana wengi zingemwagika barabarani. Rejea baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 na kauli za 'Nchi haitatawalika mpaka kieleweke.'
Wakati huo huo wanamkakati wa chama tawala wanapambana kuhakikisha wanampoteza kabisa Mhe.Lowassa awe kama mtu mbaya na aliyelididimiza taifa kwa asilimia kubwa jambo ambalo si kweli au ukweli wake unapindishwa zaidi.
Kizuri ni kwamba tayari Mhe.Rais Magufuli ameanza kutumbua majipu, tunaomba basi hatua stahiki zichukuliwe kuchunguza mali za Mhe.Lowassa na uhalali wake lakini hili lifanyike baada ya mchukua hatua pia kutangaza mali zake maana mpaka sasa hatujui Mkuu wa nchi ameingia na nini na atatoka na nini.
Ikibainika kwamba ni fisadi basi atumbuliwe jipu lakini vinginevyo nawahakikishia kwamba Chama Cha Mapinduzi kitapata wakati mgumu mbeleni. Ikumbukwe kwamba kuna wakongwe walioweka misimamo toka zamani kwamba Mhe.Magufuli hastahili kukabidhiwa Uenyekiti wa chama akiwemo Prof.Mark Mwandosya. Mpaka sasa mpasuko ndani ya chama unaendelea maana wapo wana CCM walioumia na kuumizwa baada ya Mhe. Lowassa kuhama.
Je, kuna mbinu mbadala ya kufifisha harakati za upinzani mpaka sasa?