thesym
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 3,825
- 4,754
Mgombea anayeongoza katika mbio za kuwania uraisi kupitia chama cha Republican Donald Trump amesema ataendeleza Sera za "marekani kwanza".
Ameita Sera za nje za utawala wa raisi Barack Obama "kwa ujumla ni janga lililo kubwa".
Jumanne, Mr Trump alijiita yeye ndiye mteule rasmi wa kugombea kiti cha uraisi kupitia republican baada ya kushinda majimbo yote matano.
Kabla ya hotuba Trump aliwahi ahidi kuwa Sera zake hazitokuwa "MSIMAMO WA TRUMP" ila atakuwa mtu wa kubadilika yaani flexible katika baadhi ya mambo pindi atakapochaguliwa.
Sehemu kubwa ya hotuba yake ilikuwa ikielezea kile alichokiita "udhaifu, mkanganyiko na kutokuwa na mipango madhubuti" kwa utawala wa Obama na matumaini yake ya kubadili hali ya mambo.
KUHUSU DOLA LA KIISLAMU(Islamic State).
Katika utawala wake Mr trump amesema "siku zao zinahesabika sitowaambia ni lini na kwa namna gani"
Kabla alishawahi kusema atalidhoofisha kundi la dola la kiislamu kwa kukata mirija yote inayowawezesha kupata mafuta, kuongeza ulinzi wa majini na pia njia nyingine Kali za mateso kwa washukiwa wote. Lakini kwa siku ya jumanne hakuyazungumzia hayo.
"Udhibiti wa kuenea kwa waislamu wenye itikadi Kali inapaswa iwe ni lengo kuu kwa Sera za nje za marekani" alisema siku hiyo ya jumanne pia aliongeza kuwa atafanya kazi kwa karibu na washirika wa marekani mashariki ya Kati ili kupambana na kuenea kwa itikadi Kali.
KUHUSU MPANGO WA NYUKLIA WA IRANI.
Trump alisisitiza kupinga kwake juu ya mkataba wa nyuklia na Iran ulioafikiwa mwaka Jana na nchi sita ikiongozwa na marekani ambao uliifutia vikwazo vya kiuchumi kwa kuifanya irani ipunguze urutubishwaji wa nyuklia.
Mr trump amemshutumu Obama kwa kuipuuza kile alichokiita rafiki mkubwa wa marekani yaani Israel na kuichukulia Iran "upendo na umakini mkubwa".
"Yeye (Obama) ameafikiana makubaliano na mpango ambao ni hatari na Iran, halafu sisi tunawaangalia wakipuuza masharti ya hayo makubaliano hata kabla ya wino haujakauka. Iran haiwezi kuruhusiwa kuwa na siraha za nyuklia", alisema.
Katika hotuba yake mwezi uliopita alisema atauvunja Hui mkataba pindi atakapochaguliwa.
KUHUSU NATO NA NGUVU ZINGINE(NCHI).
"Mazungumzo mapya yatachukuwa nafasi na washirika wa marekani wa transatlantic alliance,NATO" mr trump alisema atajaribu kuupa muundo mwengine mpya hilo shirika na pia kuwa na ulingano(balance) kwa marekani katika kugharamia shilika.
Mr trump amesema atalenga kufanya mazungumzo na URUSI ili kuwa na malengo yanayoendana katika baadhi ya mambo, ikiwezekana juu ya waislamu wenye itikadi Kali.
"Wengine wanasema urusi haiwezi kuwa ni mantiki", alisema . "nimelenga kuwa nayo".
China,"heshima nguvu, kuwaacha wachukuwe umuhimu wetu kiuchumi Kama wafanyavyo sasa, tunapoteza heshima yetu kwao". amesema atatafuta njia ya "kurekebisha mahusiano na china" lakini hakufafanua kwa namna gani.
KWA WASHIRIKA WA MAREKANI.
" Nchi tunazozilinda lazima zilipe gharama za huu ulinzi", alisema " Kama haiwezekani US iziache hizo nchi zijilinde zenyewe, hatuna namna".
Akiongea na New York Times mwezi uliopita kuhusu uhusiano wa US na Japan alisema: "Kama sisi tukishambuliwa wao hawana haja ya kuja huku kwa ajili ya ulinzi wetu, ila Kama wao wakishambuliwa sisi moja kwa moja tunapaswa kwenda kwao kwa ajili ya ulinzi wao, Na hilo, na hilo kiuhalisia ni tatizo".
Chanzo: BBC
My take.
Hivi akiacha Korea kusini ijilinde yenyewe, Kim Jung un wa Korea kaskazini hawezi akarusha nyuklia zake kule kusini. Nadhani huyu jamaa atakuwa na matatizo Sana kwenye Sera za nje hasa juu ya maswala ya kiusalama kwa mtazamo wangu naona trump hastahili kuwa raisi na Kama akiwa na akafuata hizi Sera Kama anavyodai basi itakuwa ni tatizo hata kwa US yenyewe.