Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,204
Wasalaam Wakuu,
Moja kwa moja tujitwike madani.
Kufuatia kufungwa kwa chuo cha Saint Joseph matawi ya Songea na Arusha,iliilazimu bodi ya vyuo vikuu kufanya utaratibu mpya wa kuwatafutia wanafunzi husika vyuo vingine. Wanafunzi wengi walipangiwa Mwenge University na UDOM.
Punde baada ya kuripoti walitakiwa kujisajili na kuanza masomo haraka iwezekanavyo. Kwa taarifa ya kwanza ya Bodi ilidai kwamba wanafunzi wapya (waliotokea Songea na Arusha) walitakiwa kufanya mitihani maalum ili kuweza kuendelea na semester ya pili.
Cha kushangaza ni kwamba,wanafunzi wametakiwa kusoma semester nyingine mpya kabisa kuanzia mwezi wa 7 yaani baada ya kumaliza semester ya pili inayoishia mwishoni mwa mwezi wa 6.
Cha kuhuzunisha zaidi,wanafunzi waliokuwa Mwaka wa tatu wametakiwa kurudia mwaka mmoja mzima. Yaani kurudi na kuwa mwaka wa pili badala ya mwaka wa tatu.Wanafunzi walipotaarifiwa na Vice-Chancelor wa chuo (UDOM) kuwa bodi ndo imetoa ufafanuzi,hawakukubaliana naye hivyo kulazimu Katibu mtendaji wa bodi ya vyuo vikuu (TCU) Prof Yunus Mgaya kuitwa na kutoa ufafanuzi juu ya hilo. Alipoulizwa maswali kwa nini wameamua hivyo,hakuwa na majibu ya kuridhisha na Mara nyingine kusema kuwa kuna maswali ambayo yapo nje ya uwezo wake. Kama katibu wa bodi unashindwa kujibu maswali hayo,je ni nani atayajibu?
Pili,wanafunzi wanaodhaminiwa na bodi ya mikopo HESLB,mwaka huo mzima nani atawalipia Ada pamoja na hela ya kujikimu?
Je,ongezeko la semester nzima ni nani atahusika na gharama zote za wanafunzi wawapo chuoni katika kipindi hicho?
Kwa mini wanafunzi wasifanye mitihani maalum na kuweza kuendelea na masomo kama kawaida? Kwani kipindi hicho cha mwezi wa 7 hadi 10 ni miezi ambayo wanafunzi wanakuwa field?
Kwa hapo mmechemsha sana. Na busara zinahitajika katika kutatua mambo haya. Naomba bodi iangalie upya utaratibu huo.
Karibuni tulijadili.