Nakumbuka miaka ile 1980 siku tunafanya mtihani wa darasa la 7, kuku wa mwalimu mkuu aliyekuwa kaatamia mayai yake kwenye kona moja nyuma ya darasa alitotoa vifaranga 13.
Baada ya kumaliza mtihani na kuhitimu darasa la 7 mida ya saa kumi jioni kuku yule na vifaranga wake naami nao walikuwa wame hitimu darasa la 7.
Si kila aliyepo darasani yuko masomoni, wengine wameatamia mayai ya vizazi vya ujinga wao.
Naamini MH Mwigulu alikuwepo darasani lakini sina uhakika kama elimu iliyo tolewa na professor wake alifanikiwa kutoka nayo walau mita mbili kutoka uswa wa mlango wa darasa.