Kwa hili Mwigulu Nchemba anastahili pongezi

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Kwa mara nyingi kumekuwepo kauli za kuwa CCM ijiandae kisaikolojia kuwa Chama cha Upinzani, katika hili Mwigulu ameonesha kwa vitendo kwa vile kila akijichangia katika vikao vya bajeti amekuwa akichukua maoni ya kambi rasmi ya Upinzani na kuanza kuipinga, kwangu mimi huko ni kujiandaa kisakolojia kuwa chama cha upinzani, kwani Mwaigulu anajua hili kuwa 2015 si mbali hivyo ameona aanze kuzoea kazi ya upinzani.

kwa hapa sidhani kama Mwigulu anapaswa kuchukiwa au kuonekana mbaya katika hili zuri analofanya, kwani si vibaya kama kujiandaa kisaikolojia kuwa chama Cha upinzani kama anavyofanya kwasababu CCM kwasasa ni Kama UKIMWI ambao hauna KINGA WALA TIBA itayofanya ishinde 2015.
 
Ni kweli mkuu kwani kazi ya mbunge ni kuikosoa serkali, kuishauri serkali nk. Ndicho anachokifanya Nchemba kwa hiyo tunashukuru kwa kuikosoa serkali tarajiwa.
 
Nakumbuka miaka ile 1980 siku tunafanya mtihani wa darasa la 7, kuku wa mwalimu mkuu aliyekuwa kaatamia mayai yake kwenye kona moja nyuma ya darasa alitotoa vifaranga 13.

Baada ya kumaliza mtihani na kuhitimu darasa la 7 mida ya saa kumi jioni kuku yule na vifaranga wake naami nao walikuwa wame hitimu darasa la 7.

Si kila aliyepo darasani yuko masomoni, wengine wameatamia mayai ya vizazi vya ujinga wao.

Naamini MH Mwigulu alikuwepo darasani lakini sina uhakika kama elimu iliyo tolewa na professor wake alifanikiwa kutoka nayo walau mita mbili kutoka uswa wa mlango wa darasa.
 
Ebwana kweli,chemba imesoma alama za nyakati.hivyo inapiga matizi kuwa mbunge wa upinzani kupitia ccm,2015.
 
CDM Take care with him. Anazidiwa busara hata na yule mtuhumiwa wa uzinzi lion-chapekeyake?

sidhani kama kuna haja yakumweka katika tahadhari kwani jinsi anavyoongea ndivyo huku mitaani watu wanapoichukia CCM zaidi naona aendelee tuu kuweka ujinga wake hadharani hakuna haja ya kumchunga
 
Kajipange Upya Bidhaa(Dhaifu na Kama Mbaya iwe mbaya) zimeshafika mitaani kama unataka jipatie upendeze! Plz ushauri zaidi my signature inahusika.
 
Nakumbuka miaka ile 1980 siku tunafanya mtihani wa darasa la 7, kuku wa mwalimu mkuu aliyekuwa kaatamia mayai yake kwenye kona moja nyuma ya darasa alitotoa vifaranga 13.

Baada ya kumaliza mtihani na kuhitimu darasa la 7 mida ya saa kumi jioni kuku yule na vifaranga wake naami nao walikuwa wame hitimu darasa la 7.

Si kila aliyepo darasani yuko masomoni, wengine wameatamia mayai ya vizazi vya ujinga wao.

Naamini MH Mwigulu alikuwepo darasani lakini sina uhakika kama elimu iliyo tolewa na professor wake alifanikiwa kutoka nayo walau mita mbili kutoka uswa wa mlango wa darasa.
Nakuunga mkono asilimia mia mbili, Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeessssssssssssss!!
 
ushabiki wa vyama ndio unatufanya tuwe mambumbumbu. utaifa kwanza there is nothing special with chadema or ccm
 
huyu jamaa anatumika! Tangu Day one akinyanyuka anajadili hotuba ya kambi ya upinzani,mpaka kuna wakati alirusha kitabu mbali! hii ni trick ya kuwateka wapinzani nao badala ya kujadili na kuconcetrate na bajeti ya serikali,wanaconcetrate kwenye bajeti yao wenyewe....na ile ya serikali inakosa upinzani na kupita kiraini! just tricks!!!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom