Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Nimechoka kila mtu ili aonekane anajua mpira anaona kuiponda simba na yanga ndo kigezo kikubwa. Huu ni ukondefu wa fikra. Huwezi ukawa na akili zenye afya ukadhani soka la tanzania litakua kwa kuiponda simba na yanga au kupendekeza kuwa timu hizi zifutwe. Wewe una fikiri sawa sawa kweli?
Imekuwa ni tabia inayojijenga kwa sasa kila mtu anapokuwa amefadhaishwa na matokeo ya mpira wa simba au yanga anakuja na suluhisho la kuwa hizi timu zifutwe. Huu ni uwezo wa chini sana wa kufikiri.
Hizi timu ni historia katika nchi yetu kwa mwenye uelewa mzuri hawezi kamwe waza jambo kama hilo. Tunafaham asilimia kubwa ya wapenzi wa mpira ni wa simba na yanga theni zinakuja za mikoani ambako mtu anatokea ambako pia huko kuna kuwa kama ilivyo first language na second language. timu mama bado ni simba na yanga. Then mtu ataipenda Mbeya city, majimaji au reli ya Morogoro. Huo ni ukweli kwa kiasi kikubwa kwa wale wenye umri mkubwa kwenye michezo ukiacha watoto wa miaka hii ya 90 na 2000s.
Na kiukweli si kuwa ili uweze onesha una uwezo wa kuchambua michezo basi ni vyema ukatumia mawe timu hizi, tunajua kuna wanaolipwa kwa kuzitupia mawe timu hizi na kuzisifia timu zile au pengine za nje. Lakini kuna wengine ni kwa ulevi na ukosefu wa vitamins katika fikra wanadhani miti ya kutupia mawe ni simba na yanga tu ili waonekane nao wanaweza kurusha mawe.
Azam imekuwa kwenye soka kwa miaka kadhaa sasa. Naipongeza ina mtaji mkubwa kutokana na kumilikiwa na mtu tajiri. Lakini kimataifa tujiulize imeshiriki mara ngapi na imefanya nini ambacho simba na yanga hawajahi? mtasema uwanja. Ni kweli. Hili ni jambo zuri sana na la kupongeza lakini muelewe azam haindeshwi na wanachama. Azam kuna watu wapo kule kimaslah tu illa mioyoni mwao ni wapenzi wa simba na yanga.
Na wengine kwa sababu ya chuki na hasira ndo wanasema wao ni azam lakini kiuhalisia washabiki hasa wenye uchungu na azam hawafiki hata 1000. Huwezi ilinganisha na simba na yanga katika hili. Bado hizi zitabaki kuwa ni timu kongwe na zenye ushawishi mkubwa katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla. hamjajifunza? Angalieni zanzibar baada ya kutetereka kwa small simba na jamhuri na ile nyingine nimeisahau. Ligi ya Zanzibar imekuaje? Ukiweka sababu nyingine pia ni kukosa msisimko. na ndo maana ni ngumu pia kuzifanya simba na yanga zishuke daraja.
Huo mwaka TFF wata experience mapato kidogo kuliko inavyodhaniwa. Usilinganishe ligi ya uingereza na ya Tanzania au Hispania na Tanzania. Angalia ni timu gani zinajaza uwanja wa Taifa. Hata azam ikicheza na timu nyingine ule uwanja haujai.
Tuache kuwaza fyongo kuwa simba na yanga ndo zinaua mpira wa tanzania..tujiulize lini ulikuwa hai na sasa umekufa. Tukubaliane kuna mapungufu lakini solution si kuziua/kuzivunja au kuzishusha daraja. Tuwaze kwa unene kidogo, mtu akipata jeraha kwenye kidole haimaanishi mkono wote ukatwe ....ni dakatar mvivu na mzembe anayeweza kufikiri hivyo.
NIMESEMA SASA KAMA UTAKASIRIKA KASIRIKA TU, SIWEZI UNAFIKI NA MOYO WANGU UMETULIA.