marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa UKAWA chini ya CHADEMA imepwaya.
Kuna faida ambayo CHADEMA imeipata kupitia CHADEMA ila baada ya hapo imepoteza mwelekeo ambao ndiyo ilikuwa hamasa ya wananchama.
Wanachama walipenda kuona chama pamoja na viongozi wakiwa mstari wa mbele kuwasemea wananchi na kuwatetea pale ambapo serikali haikuwa sahihi.
Pamoja na kwamba Lowassa anasema hafuati njia ya uanaharakati ila bado njia aliyoitumia inachangamoto lukuki kwani haki itaendelea kukanywaga kwa muda mrefu.
Pamoja na yote yaliyotokea bado namheshimu sana Slaa kwa kuiongoza CHADEMA katika njia ambayo iliwapa hamasa na kuwafanya wawe na matumaini ya kimaendeleo hapo mbeleni.
Timu iliyokuwa chini ya slaa ilijinasibu sana kwa ajili ya wananchi na taifa. Mfano ;- Zitto,Mnyika,Lissu,Mdee,Lema,Sugu n.k ambapo waliwapa motisha na wa vyama vingine vya upinzani.
Leo yamebaki matamko yasiyo na tija. Siwezi kushangaa chama kinachojinasibu kuwa kikuu cha upinzani kupata upinzani ndani ya wapinzani wenyewe.
CHADEMA inatakiwa kuwa na viongozi wenye kwenda na wakati. Wajifunze kwenye makapuni ya simu na magari kila baada ya muda fulani wanaleta toleo jipya.
Hivyo kama viongozi mbinu zimeisha waache kupoteza muda wa wananchi ili wenye mbinu mbadala washike hatamu. Lowassa na sumaye hawawezi kuleta mbinu mpya maana wao mfumo wao ni wakizamani ambao ni wa kimakundi zaidi kama ulivyo kwenye CCM.
Demokrasia ianzie nyumbani ndiyo itoke nje.