Kwa gharama kubwa za original spares acha mchina aendelee kupeta

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
10,425
15,981
Hope wote mnaendelea vema na majukumu,

Ebana eeh, kababy walker kangu kalizingua front wheel bearings nikiwa mkoani. Sasa jamaa wa garage akashauri tuagize kutoka Dar, kuuliza bei nikaambiwa kwa bearing moja ni Tsh. 55,000-70,000 nikaona kusubiri spare napoteza muda. Nikanunua moja mtaani ya Tsh. 25,000/- nimaweka kwenye gari nikaendelea na safari.

Kilometer kama 5 mbele gari ikaanza kuunguruma nikajua yes kitu fake kimeshaanga mashindano, ikabidi nijikongoje hadi maskani nikapaki nisubiri muarobaini wa tatizo.

Sasa leo nikasafiri kuja Dar nikaone mambo yasiwe mengi wacha niende straight kwa Toyota dealers pake K/koo nikamueleza nataka front wheel bearing za Allex. Laaahaula, jamaa kasearch kwenye system akaniambia moja ni Tsh. 175,000/- yaani ni mara 6 ya ile niliyoweka na mara 3 ya ambazo jamaa walitaka niagize town.

Nikauliza break pad akanjambia ni Tsh. 215,000/- 🥹🥹 wakati Mchina anatuuzia kwa Tsh. 15,000/-.

Nikaona kwani Tsh. 350,000/- kitu gani wakati nachukua kitu original? Ndio hivyo wakuu nimekwanguliwa Tsh. 350,000/- kwa pair ya bearing.

NB: Remember cheap is expensive, ni afadhari ukachukua kitu og kitacholast kuliko fake utayotumia kwa muda mfupi.
 
Mchina kaweza sana kutengeneza vitu vya bei rahisi ila kwenye spare za vyombo vya usafiri kakwama
 
Spare parts za kuchunga zipo Kwa Toyota Tu.
Magari tofauti na Toyota ni ngumu Sana kukuta wanauza vitu fake
 
Hapo Toyota Msimbazi Street niliwahi kununua spark plugs za 1ZZ-FE kwa sh 180,000/-. Plug 1 ilikuwa sh 45,000/-.
Ni sahihi mm pia nikishawahi kununua kwa hiyo bei.... ukija kitaa mchina kafyatua kitu anauza kwa 15k.... mchina kajua kucheza na fursa
 
Hapo walikupiga maana feki ni 35000 hadi 45000 original ni 100000 hiyo ni front ukitajiwa ya nyuma si ndio utapaki gari kabisa na uzuri wa hizo bearing zinaingiliana na za gari nyingi
 
Back
Top Bottom