Kwa biashara hii natakiwa kuwalipa TRA kiasi gani cha kodi?

swamy

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
252
143
Mtaji wangu ni kati ya 7.5M - 10M nimewekeza kwenye duka la chakula,sabuni spices nk... reja reja ILALA DAR, wakuu wataalamu wa TRA nawaomba munijuze hapa kiasi gani yafaa nilipe TRA kwa mwaka, kwani nashindwa kujua hesabu zao wanapiga vipi katika makadirio yao.

Mwaka jana wamenitandika 1M kwa Mtaji niliokuwanao wa 5M na mauzo ya kila siku ni kati ya 30alfu - 80alfu siku za sikukuu inapanda Wakati mwingine mpaka laki 2.

Lakini hii biashara inanikondesha moyo sabbu mimi pia ni mkulima wa mpunga hivyo kila nikiuza mazao pesa nawekeza hapa dukani, ni mwaka sasa naona ile 1M niliotoa TRA ndio faida yangu, Ndio nataka nitinge tena huko TRA nikiwa nimeongeza Mtaji wa duka kufikia kiwango nilichoandika hapo juu.

Duh nawaza sijui wataniambia shilingi ngapi..... wakuu nawaomba munijuze kiwango na namna ya kuwakinaisha wale jamaa ili wasinipige kwa kunikomoa.... shukran.
 
Nasikia ukitumia EFD unakuwa na rekodi nzuri za mauzo na hivyo unaepuka kukadiriwa
 
Swamy ukitaka ujue na wasikupige kama ulivyosema dawa yao wewe weka hesabu zako vizuri za manunuzi,matumizi kwa ajili ya biashsra na mauzo.mm TRA waje tu tena nimeingia tovuti yao ile www.tra.go.tz siku hizi naona wameweka na lugha yetu ya kiswahili naona weelezea sijui ukiuza kwa mwaka milioni 4 mpaka saba na nusu tutalipa 150,000 kodi ya mwaka ika kama tukiwa na kumbukumbu tumezitunza wanapiga asilimia tatu ya kilichozidi milioni 4 kwa mwaka mzima.ngoja nifungue nikutumie na wewe
 
Mauzo ya Mwaka

Kodi inayolipwa endapo kumbukumbu za biashara haziridhishi

Kodi inayolipwa endapo kumbukumbu za biashara zinaridhisha

Ikiwa mauzo hayazidi ShT. 4,000,000

Hakuna

Hakuna

Ikiwa mauzo yanazidi ShT. 4,000,000 lakini hayazidi ShT. 7,500,000

ShT. 150,000

3% ya mauzo yanayozidi ShT. 4,000,000

Ikiwa mauzo yanazidi ShT. 7,500,000 lakini hayazidi ShT 11,500,000

ShT. 318,000

ShT. 135,000+3.8% ya mauzo yanayozidi SHT. 7,500,000

Ikiwa mauzo yanazidi ShT 11,500,000 lakini hayazidi ShT 16,000,000

ShT. 546,000

ShT. 285,000+4.5% ya mauzo yanayozidi ShT. 11,500,000

Ikiwa mauzo yanazidi ShT 16,000,000 lakini hayazidi ShT. 20,000,000

ShT. 862,500

ShT. 487,000+5.3% ya mauzo yanayozidi ShT. 16,000,000

Hiyo kamanda hope itakusaidia kuelewa usije danganywa
 
Hiyo laki na nusu ni ukiwa umepata faida ya milioni 4 au ni vipi hapo kaka nifafanulie.
 
Dah ndugu Zulu nimekuelewa sana AHSANTEE, ila hawa jamaa wakinikatalia wakitaka milioni kama ya mwaka jana nifate nidhamu ipi ndugu.
 
kwa mauzo ya 32,897,000 napaswa kulipa kodi bei gani Wanabodi?
 
Kitu kibaya katika kodi ni kulipa kulingana na mauzo. Hapa ndio tatizo, migogoro inapoanza kati ya TRA na mfanyabiashara. Endapo ingekuwa kwa kutokana na faida ya mauzo. Mfano mauzo ni mln 13,000,000/= mtaji ni milioni 2,200,000. Ingetoa
-mtaji
-fire extigwisher
-umeme,
-ghalama za usafi/taka
-ghalama za ulinzi
-vibalua
-ghalama za leseni
-michango ya mwenge
-luch za waendeshaji na vibarua.
-kodi ya pango, malekebisho ya pango mfano rangi.
- mshahala wa mwendeshaji.
-ghalama zinginezo za uendeshaji. Sasa faida inayobaki ndio wafanye makadilio. Ila hili halifanyiki kwa mfanyabiashala mdogo mwenye flemu ya kawaida. Kumkadilia kutokana na mauzo bado ni tatizo ukizingatia anaghalimika ghalama hizo na nyingine kila mwezi!.
-

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona hapo mkuu ametoa maelezo mazuri. Nami nimepitia kwenye tovuti nimeona kwamba kodi inalipwa kwenye faida. Faida inapatikana kama utatengeneza vitabu vya hesabu na kutoa hizo gharama. Sheria yao inasema kwamba ambao hawalazimishwi kutengeneza vitabu ni wale ambao wana mauzo kati ya Million 4 na Million 20. Ukiwa na mauzo zaidi ya Million 20 unatakiwa kutengeneza vitabu vya hesabu na hivyo kuonyesha faida ili wakate kodi. Wale wenye mauzo kati ya million 4 hadi 20 wana option ya kutengeneza vitabu ama la. Kama hajatengeneza basi kodi yao ni kati ya Shs 150,000.00 hadi Shs. 862,500.00 kwa mwaka kutegemeana na ukubwa wa mauzo.

Inabidi tujisomee sana na hao TRA watoe elimu ya kodi ili watu wafahamu haki zao. Suala kama hili linatakiwa kuwa wazi kwa kila mtu anayefanya biashara na hata huyu aliyeuliza angekuwa ameambiwa ama kufundishwa wakati anachukua leseni ama TIN ya biashara. Nilisikia TRA wanasema watakuwa na mafunzo kwa watu wanaoanza biashara. Hii ni muhimu sana
 
Hiyo laki na nusu ni ukiwa umepata faida ya milioni 4 au ni vipi hapo kaka nifafanulie.
Mkuu hapo si faida. Hiyo Shs 150,000.00 ni kodi ya mwaka kama una mauzo kati ya Shs. Million 4 hadi Million 7.5 na hutengenezi vitabu.
 
kwa mauzo ya 32,897,000 napaswa kulipa kodi bei gani Wanabodi?
Kwa jinsi nilivyosoma, kwa hayo mauzo unatakiwa kutengeneza vitabu vya hesabu ili ulipe kodi kutokana na faida unayopata na kama hupati faida basi hutalipa kodi!
 
Mkuu sio duka, yaani nimeuza vifaa kwa mtu vyenye thamani ya pesa hiyo, kwa mara moja tu. Nimefanya biashara ya siku moja tu, Kodi natakiwa nilipe kiasi gani hapo?
 
Kwa kuzingatia mchanganuo wa Otega inaonekana kwa mauzo yako unakimbilia humo kwenye milioni

TRA wanachoangalia ni Turn Over na so faida kama wengi wanavyodhani

Kama unataka haki tafuta mashine ya EFD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuzingatia mchanganuo wa Otega inaonekana kwa mauzo yako unakimbilia humo kwenye milioni

TRA wanachoangalia ni Turn Over na so faida kama wengi wanavyodhani

Kama unataka haki tafuta mashine ya EFD

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, mimi nafanya biashara ya mara chache sana, sasa nimemuuzia mtu mzigo wa hiyo pesa tajwa ndio nahitaji kufahamu kodi ni kiasi gani hapo, kwanini hakuna mipangilio ya kueleweka kwenye masuala ya kodi. Sisi wengine hatufanyi biashara za kila siku ama duka.
 
Kwann unateseka isee....pitia shortcut haya maisha ni kusaidiana ukijifanya unafuata Sana sheria ndo maana ulipigwa hiyo hela, kamata mfanyakazi wa TRA unampoza ela kidogo then unamwambia akukadirie kiasi unachoona kwako ni afadhali. Point ni kutokukwepa kodi haijalishi utachangia kidogo au LA cha msingi umechangia pato taifa, kuna wengine wanaishi kwa kula tu kodi za watanzania bure so ukisema hii njia sio fair na hao ambao hawalipi tunawafanyaje?
 
Back
Top Bottom