herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,364
Afrika Mashariki nchi hizi zote kuna mambo mengi ya hovyo yanayofanywa na watawala sababu hii inafanya raia wengi kuzidi kuzama kwenye lindi la umaskini wa kunuka.
Lakini Kenya mazuri yapo hasa kwenye mifumo yao kutoingiliana kiutendaji serikalini na raia kupigania haki zao za msingi.
Kenya baada ya madaktari kudai waongezewe mishahara serikali ikatishia kuajiri madkatari kutoka Tanzania, kwa Tanzania ilishakubali kuwapa Kenya madaktari japo Tanzania kuna upungufu wa idadi kubwa na uhitaji wa madaktariu huko kwenye vituo vya afya lakini mahakama nchini Kenya ikatoa zuio kwa kutoa hoja nzito ya madaktari wengi waliopo Kenya wanaosubiri ajira hivyo serikali ya Kenya ikaona hakuna namna hivyo kuamua kuwaskiliza tu madaktari ili wasitishe mgomo na kurejea kazini kwa kuwatimizia mahitaji yao.
Huu ni mfano mmoja lakini yapo mengi Kenya yanayofanyika na mahakama inakuwa suluhisho la kutoa haki tofauti na Tanzania kimsingi Kenya mahakama inaamua kwa uhuru zaidi ya Tanzania.
Sasa kuna hili zuio la harakati za kisiasa na maandamano Tanzania hadi mkuu wa nchi hiyo atakapoamua tu yeye kuruhusu tena, kwa Kenya hatua kali za kisheria zingeshachukuliwa kupinga zuio la mtindo huu linalovunja katiba ya nchi.
Hata mahakama kwa Kenya ingeshalifutilia mbali zuio la namna hii achilia mbali raia kuandamana kila wiki hadi pale wapate haki yao ya msingi.
Watanzania wamelala usingizi mzito kwenye lindi la umaskini unaozidi kutamalaki na kutoa nafasi kwa watawala madhalimu kufanya watakalo kwa maslahi yao hali Wakenya wanapiga hatua tu kila kukicha na hawako tayari kuwaacha watawala waamue hovyohovyo.
NB:
SHAMBULIA HOJA USISHAMBULIE MTU YOYOTE AU MTOA MADA.