Mkuu hii mada imewahi kuja humu jukwaani watu wakaichangia but I guess you were not around.
Mimi mchango wangu ulikuwa ni kwamba kimsingi tatizo hakuna..unaweza kumuoa na mkaishi maisha mazuri tu. ila nilijitahidi kulist negative sides za ndoa kama hiyo kama ifuatavyo:
Life expectance
Nilifafanua kuwa kama mtakuwa mmezidiana sana linakuwa jambo la mashaka kwamba for how long you shall be together in this life. Chukulia una miaka 25 then unaoa mwanamke ambaye ni 45...chukulia wastani wa kuishi wa mtanzania kwa sasa labda ni miaka 60..hii itamaanisha kuwa wakati wewe unaexpect kuishi miaka mingine 35, wife wako atakuwa anadai miaka 15..so kimahesabu uwe tayari kuishi mghane kwa miaka 20
Interests
Mara nyingi interests za mtu huenda hand in gloves na age yake...kwa gap kubwa ya umri inamaanisha totally different interests. Sasa kama wana ndoa mna very few things in common inakuwa shida..unataka ukamate station ya movie..ye anataka muangalie "wanawake na maendeleo"...unataka kwenda disco ye anataka mwende mkesha church...unataka mapenzi ya kubinjuana, ye anataka conventional style...ni shida kidogo
Keeping each other company
Hii inaendana kidogo na hapo juu...any successful marriage utakuta mtu na mke wake ni good companions...sasa watu mna interests tofauti..marafiki zake are not your style and vice versa...mtajikuta kila mtu anaspend muda kivyake na hapo cement fulani ya ndoa nzuri inamomomnyoka.
Mtazamo jinsi ya kulea watoto
wazazi hutreat watoto wao kutokana na umri wao (wazazi). Nikivuta kumbukumbu yangu, babangu alikuwa anaamini maisha ya mtoto yamecenter katika vitu viwili...kanisa na shule. niliwahi kupigwa kama mwizi kwa sababu niliacha kwenda tution nikaenda kucheza mpira..kwake yeye michezo was a wastage of time..I am not saying he was wrong but a balance is needed...lakini ajabu juzi eti kataka kumtoa macho sister kwa kukataa kumnunulia mtoto (mjukuu wake baba) mpira!! so with age we treat kids differently...hapo nachelea msije mkakinzana na mkeo jinsi ya kuwalea wanenu.
zipo nyingine lakini nachelea nitakuchosha na maelezo mengi