Habari wana JF !
Nina pendekezo kuhusu watoa huduma za mahospital na sehemu zote za huduma ya afya, kuwe na utaratibu wa kupimwa afya zao ili wagongwa wanapokuwa mahospital wawe na amani na huduma wapatazo kwenye vituo hivyo.
Kuna baadhi ya hospital asilimia kuwa ya wauguzi wa hospital hizo wameugua (wagonjwa wa ukimwi) na inafahamika kabisa, lakini kutwa kuwachoma sindano tu wagonjwa.
Wengine wapo sekta ya kuwazalisha kuna mama, sasa dokta mgonjwa wa ukimwi anakuwa kitengo cha kuwazalisha kina mama na kuwachoma masindano au kuwasafisha vidonga na ameugua, akiwa na roho mbaya ataweza kuwa anawaambukiza wagongwa wengine waliokuja hospital kwaajiri ya kutibiwa ugonjwa tofauti, wakitoka hospital wanatoka na ugonjwa ambao hawakua nao.
Dokta mwenye Uukimwi anajitolea damu anachangaya kwenye dawa nyingne na anamchoma nayo mgonjwa aliekuja kutibiwa kwa ugonjwa mwingne.
Naomba vituo vyote vya afya waiguzi wawe wanapimwa afya zako kila baada ya miezi mitatu, watakaogundulika wameathirika ukimwi wawe wanafukuzwa kazi.
Kwanza kabisa Punguza uoga hakuna mtu mwenye Roho hiyo unayofikiria Maana umefikiria vitu vikubwa sana ambavyo kiuhalisia ni Impossible Hasa kwa kada ya afya uliyotaja..Watu walio na weredi na waliosoma Ethics kwa muda mrefu..
Na ukikuta Wasio na weredi ni 2 kati ya 100..
Na hata hao hawafikii Level ya kusababisha Matatizo makubwa kwa wagonjwa...kwa hiyo hicho ulicho waza ni impossible..
Yaani kifupi vyote haviwezekani..
Umepropose kuhusu Watoa huduma kufanyiwa checkup hiyo ni sheria ya kikanuni kwamba kabla hajaanza kazi lazima afanyiwe check up na Daktari wa Serikali ili kuthibitisha...
Na ipo Chini ya
Standing order of the public services ya mwaka 2009 (KANUNI ZA KUDUMU ZA UTUMISHI WA UMMA 2009) Kipengele au Kanuni D.16
Ila kuendelea kumpima Kwa kigezo cha kupreviw au kut9a majibu ya Afya yake hairuhusiwi kisheria na Ni kinyume kutunga sheria yoyote au Kanuni au Sera Ambayo itabdilisha au kuexpose Privacy and confidentiality yake...
Hii ni kwa mujibu wa
HIV and AIDS (Prevention and Control) ya Mwaka 2008 kifungu cha 28 cha sheria
Lakini kingine Jua kabisa kwamba Hakuna mtu stakaye lazimishwa kisheria kupima HIV kwa sababu ni kinyume cha sheria Hiyo hiyo..
HIV and AIDS (Prevention and Control) ya Mwaka 2008 kifungu cha 15 cha sheria hiyo
Tuseme bhasi amelazimisha na ameruhusiwa na sheria kukupima na amekukuta na HIV pia hairuhusiwi kuachishwa kazi kwa Ajili ya HIV/AIDS
Kwa mujibu wa Kanuni Za Ajira Na mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora) Za mwaka 2007 ambazo zimeandaliwa chini ya sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na zipo kwenye Tangazo la Serikali no 42 la Tarehe 16/02/2007 Kanuni Namba 20
Ila endapo kama atapatwa HIV na akashindwa kuhimili kazi kama kanuni hiyo hiyo kanuni namba 19 inavyosema...
Vinginevyo haiwezekani kwa hicho kitu....
Naomba nikutoe hofu kwamba Hospitali zote kwa ngazi zote..zinatoa huduma Stahiki na kwa Mujibu wa sheria na taratibu huku ikizingatia Sheria na Miongozo iliyowekwa na hakuna atakayeweza kusababisha Matatizo kwa Wagonjwa Hata kama akitaka....