Capital
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,457
- 1,052
Wanabodi, hivi karibuni serikali imepiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma, wakiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma. Hali hii inasikitisha sana kwa sababu
1. Vyuo vikuu vina miradi ya utafiti wa masuala mbali mbali yenye maslahi kwa nchi na dunia nzima na katika tafiti hizi, watu mbali mbali wa nchi, ikiwemo wafadhili na watafiti wa kimataifa huhusika. Kusafiri nje ya nchi huwa ni kwa malengo mahsusi na si kwenda kufanya shopping kama serikali inavyotaka kuaminisha wananchi
2. Serikali katika miaka ya hivi karibuni haijawahi toka pesa kwa ajili ya kuendesha tafiti za kisayansi katika vyuo vikuu vya umma. Haitoi kwa kisingizio cha kukosa pesa. Wahadhiri hawajawahi kulalamikia hali hii kwani wanafaham duniani kote, lazima wafanye tafiti, hivyo kama serikali haina bajeti, lazima waandike miradi ili kupata pesa, ambazo mara nyingi ni za wafadhili wa kimataifa ili kufanya tafiti. Faida za miradi hii ni nyingi kwani hukatwa asilimia 5-10 ambayo huingia katika fuko la chuo husika na kuwa chanzo cha mapato. Miradi hii huchangia manunuzi ya vifaa mbali mbali zikiwemo kemikali kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wa vyuo. Pia zana mbali mbali za kufundishia hutolewa na miradi ya tafiti mbali mbali.
3. Wahadhiri kupitia miradi hii huweza kutoa machapisho ya matokeo ya tafiti mbali mbali kwa ajili ya watafiti wengine pamoja na watu wa kawaida, wa nchini na kimataifa. Machapisho haya huwapandisha vyeo wahadhiri hadi kuwa maprofesa.
Faida za miradi hii ziko nyingi ila nawezaishia hapa kwa leo.
Endapo zuio la kutosafiri nje wahadhiri halitaondolewa mara moja, hasara zifuatazo zitajitokeza
1. Kupungua kwa mapato kwa vyuo. Ifahamike serikali hutoa pesa kidogo sana kwa ajili ya uendeshaji wa vyuo.. hata wakati mwingine hata pesa ya chaki hukosekana.
2. Watafiti wa kitanzania watakosa kushirikishwa katika miradi/ tafiti mbali mbali kwa kigezo cha kunyimwa ruhusa ya kusafiri nje ya nchi
3. Kwa vile serikali imeshajitoa katika utoaji wa pesa ya utafiti, hili ndo litakuwa kaburi la sayansi hapa nchini.
Ushauri
Nawashauri washauri wa rais msiwe wanafiki kwa kushindwa kumweleza rais ukweli huu. Nafahamu hamuwezi kufahamu mambo haya kwa sababu mna roho za kukomoana. Cha zaidi serikali haijawahi kumlipia mhadhiri pesa ya nauli au pesa ya kujikimu akiwa nje ya nchi, na wahadhiri hawaendi huko nje kwa ajili ya starehe, kwa nini wazuiliwe?
Tufike mahali tuache siasa katika vitu visivyo na manufaa kwa nchi. Aidha, ikiwa rais itapata wasaa wa kupita hapa, fikiria vizuri maamuzi yako. Kuna makundi ya watumishi wa umma ambayo ni haki kuzuiwa lakini hili la wahadhiri, nadhani busara za kisomi zichukuwe mkondo wake
Nawasilisha