tamimusalim
JF-Expert Member
- Jun 17, 2014
- 1,822
- 501
- Thread starter
-
- #21
1. Kuna scholarship za kumwaga. Omba ubalozi wa Japan. Ukifaulu, unaweza kuishi Japan baada ya masomo yako. Wanahitaji watu, raia hawazai.
2. Funga ndoa na Mjapani. Viza ya ndoa inakuruhusu kufanya kazi yoyote. Baada ya miaka 5, unapata "green card" ya Kijapani. Ukifaulu mtihani wa Uraia ( kwa kijapani) unapata pasipoti yao ukipenda.
3. Kazi za BOX zipo nyingi. Inahitaji elimu ya Kijapani. Wananchi wengi hawajui Kiingereza.
Wageni wachache sana, ila lugha ndiyo matatizo. Kuandika Kijapani ni balaa tupu lakini kuongea siyo tabu sana. Unaweza kujifunza mwenyewe katika mtandao.
4. Kodi hukatwi ndani ya kiasi hicho kama una watoto tu au umekopa kununua nyumba.
Kila la heri.
Duuuu nimefulahi sana kuja jamvini mtu kama wewe umetukaza akili ujue wabongo wengi hapa wangedanganywa na wanaojifanya wanajua, vp mkuu unamwaga point tokea wapi uko tokyo au bongo chafu

Shukrani nitakutafuta zaidi kupata maelezo,nimefanya kazi bongo miaka karibia 8 lakini bado si yanga wala si simba.
Wakati wewe mwenyewe huna uhakika "pumba" gani nimeandika wala kushindwa kunisoma, ila "unahisi" tu, huoni kwamba wewe ndio unaleta upumba hapa?
Katika mada, lazima utoe sababu za msingi unazozipinga, siyo hisia. Hisia hazina nafasi katika hoja, labda kwenye vijiwe vya kahawa.
Jipange upya ili unielimishe.
Basi utakuwa polisi ya morogoro wewe
kwahiyo kama nimekusoma vizuri inamaanisha kuwait wanaexport sana kuliko wanavyoimport?! so wanaexport kuliko japan, usa, china, russia etc?
"wanaexport sana kuliko wanavyoimport" ina maanisha exports revenues zao ni kubwa kuliko imports payments zao, haimaaninishi kuwa wana exports zaidi ya nchi nyingine. Kuna nchi wana exports kuliko Kuwait ila na wana imports sana ndio panapotofautiana...kumbuka tunaongelea revenues (payments) sio units (quantity)...
Kwa mfano kwa mwaka 2013 Current account balance (% of GDP) ya Kuwait ni 39.7%, ya Japan ni 0.7% ya USA ni negative 2.4% ya China ni 2.0%...
Current Account ni sawa na Export kutoa Import +...+... (nikiandika yatakuwa mengi)
Duuuu nimefulahi sana kuja jamvini mtu kama wewe umetukaza akili ujue wabongo wengi hapa wangedanganywa na wanaojifanya wanajua, vp mkuu unamwaga point tokea wapi uko tokyo au bongo chafu
Shukrani nitakutafuta zaidi kupata maelezo,nimefanya kazi bongo miaka karibia 8 lakini bado si yanga wala si simba.
Namna ya kuuza/ kununua bidhaa
1. Importer.tradekey.com
Hapa unaweza kupata wateja wanaotaka juice ya matunda mbalimbali pamoja na vitu vingine.
2. Alibaba.com
Hapa unaweza kupata contact moja kwa moja na wenye viwanda wa kila kitu China. Ni sehemu nzuri ya kununua bidhaa kwa wingi na bei nzuri. Hamna mtu wa kati, bidhaa inakuja moja kwa moja kutoka kiwandani.
3. Tripadvisor.com
Lonelyplanet.com
Fodors.com
Forum.vitualtourist.com
Hii ni sehemu nzuri ya kujitangazia biashara yako ya hoteli, kujibu maswala ya watalii na kupata mteja.
4. Ofisi za Ubalozi wa nchi za nje.
Mara nyingi kuna afisa anayehusika na biashara atayekusaidia kukupa contact za wafanyabiashara wa kwao au kukusaidia kujua sheria zao za biashara na fomu za kujaza kuridhisha sheria zao wakati wa kusafirisha.
5. T.justdial.com
Wanauza perfume kutoka India kwa bei ya jumla kutoka kiwandani. Kuna contact za wauzaji tofauti.
6. Bestvaluewineguide.com
Hapa unaweza kununua chupa moja ya mvinyo wa Afrika Kusini kwa $2.00.
Shukran. Kama ukiwa na maswali mengine kuhusu Japan, nitajitahidi kujibu hapa kadri ya uwezo wangu.
Nafanya biashara hasa maeneo ya Asia lakini naenda pia Tanzania na nchi nyingine za Afrika kwa kazi na likizo.
Mkuu Tokyo hivi wewe ndo mwanamziki wa tz huko? {fresh Jumbe}. Nazingua tuu mkuu ila una sehemu muhimu sana ya shukrani zangu ndano ya moyo wangu kwa mchango wako jengefu humu.
Naomba unisaidie ia taarifa ya soko la sungura na kuku waliofugwa in organic ways huko please kama unazo. Ufugaji ndo njia niliyoichagua mdoo wako
Namna ya kuuza/ kununua bidhaa
1. Importer.tradekey.com
Hapa unaweza kupata wateja wanaotaka juice ya matunda mbalimbali pamoja na vitu vingine.
2. Alibaba.com
Hapa unaweza kupata contact moja kwa moja na wenye viwanda wa kila kitu China. Ni sehemu nzuri ya kununua bidhaa kwa wingi na bei nzuri. Hamna mtu wa kati, bidhaa inakuja moja kwa moja kutoka kiwandani.
3. Tripadvisor.com
Lonelyplanet.com
Fodors.com
Forum.vitualtourist.com
Hii ni sehemu nzuri ya kujitangazia biashara yako ya hoteli, kujibu maswala ya watalii na kupata mteja.
4. Ofisi za Ubalozi wa nchi za nje.
Mara nyingi kuna afisa anayehusika na biashara atayekusaidia kukupa contact za wafanyabiashara wa kwao au kukusaidia kujua sheria zao za biashara na fomu za kujaza kuridhisha sheria zao wakati wa kusafirisha.
5. T.justdial.com
Wanauza perfume kutoka India kwa bei ya jumla kutoka kiwandani. Kuna contact za wauzaji tofauti.
6. Bestvaluewineguide.com
Hapa unaweza kununua chupa moja ya mvinyo wa Afrika Kusini kwa $2.00.
Tokyo40 nataka kuku-like alaf kutufe cha ku-like sikioni ila ntajitahidi. Napenda sana taarifa kama hiz, big up.
Mungu akubariki zaidi na zaidi.
Siyo rahisi kabisa.
Jitahidi kuelewa maswala ya uchumi.
Kwanza, hatuna mafuta ya kuchimba.
Tanzania kuna gesi (LNG) nyingi na hata hivyo, serikali imetangaza mapato ya baadae ya kama $3 Bilioni kwa mwaka watapomaliza ujenzi baina ya 2017 na 2022.
Pia, bei huenda ikipanda au kushuka katika miaka 25- 30 ya Uzalishaji mpaka kisima kukauka.
Kupanda kwa thamani ya fedha ya nchi inahitaji uwe mzalishaji wa vitu mbalimbali vinavyotumiwa duniani, siyo tu gesi.
Kufika katika Maendeleo ya nchi kama Malaysia au Afrika Kusini, tunahitaji uzalishaji wa $300 bilioni. Sasa tunazalisha kama $40 bilioni. Tutafika tukijipanga vizuri, lakini safari ni ndefu.
Kumbuka, Japan hana gesi wala mafuta. Ni uzalishaji tu wa vitu kila kona ya dunia wanavitumia.