BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,738
- 3,198
Salaam wadau,
Ni kawaida katika mahusiano ya mapenzi baina ya mwanaume au mwanamke mmoja anaweza kuamua kusitisha uhusiano kwasababu fulani au hata bila kutoa sababu maamuzi ya mtuyanapaswa kuheshimiwa mapenzi ni hiari na hiari yashinda utumwa.
Kuna baadhi ya wanaume/wanawake huwa ni ving'ang'anizi hawakubali kuachwa!Wapo radhi kuleta vurugu/mtiti,kukudhuru au kujidhuru wenyewe!Ili kuendeleza mapenzi ambayo mmoja wao hayataki hii hali vizuri uisikie kama hadithi usiombe ikakupata.
Siku za nyuma niliwahi kujuana na Dada mmoja cute toka Mbezi ya Tangibovu anaitwa Juliana mwanzoni nilimuona kama msichana descent tukawa marafiki katika uhusiano wa bae&boo.Nilishtuka siku moja alipanda kwenye gari langu alikuta seat ya mbele ya abiria imelazwa(unaweza fikiria kuwa aliyeikalia aliamua kujilaza) nikainyenyua ile seat ili akae.
Mda uleule akaanza kunilaumu na kuangua kilio kuwa sikuwa mwaminifu pale kulikuwa na msichana nilikuwa naye kwenye gari alilala pale! Nikamwelewesha hakunielewa,akaniboa,nikajumlisha na makosa mengine ya nyuma nikamfutia usajiri(nikamwambia tuachane sitaki makuzi).
Juliana hakukubaliana na uamuzi wangu,akatumia njia za kidiplomasia kunishawishi na kuwashirikisha best zake niligoma kumrudia kimbembe kikaanza kusumbuliwa!Napigiwa simu nizisozijua masaa tofauti mda wa mwaka na nusu nilijaribu kublock,kwenda voda na Tigo/polisi sikupata ufumbuzi,nilipata usumbufu ambao sitaweza kusahau kwakuwa hata nilivyobadili namba za simu haikusaidia aliweza kupata na kunipigia kwa namba tofauti unaweza kufikiria ni namna gani unavyoharibiwa pozi na pia kwa kazi zangu siwezi kukwepa kupokea namba ngeni ya simu.
Hatimae alikuja kuacha baada ya kunipa kibano kile sijui aliko nilijifunza kuwa vizuri kuwa makini na mioyo ya watu tunaoanzisha nao mahusiano wengine wanaweza kukuletea fadhaa badala ya furaha pia jamani ukiachwa
maisha yapo! Usiendelee kukomaa na mwenzio mpaka unamharibia kwa mwanamke/mwanaume mwingine aliyempata baada ya kukuacha.
Karibuni kama umewahi pigwa/piga kibuti kikakutokea puani.