unaweza ukawa na digrii lakini usijue kuitumia, itumie kuleta tija na ufanisi kazini uoneshe tofauti kati yako na mwenye cheti kiutendaji kisha uone matokeo yake!Wanajf tulidai Salary. Vyeo vipande tukaambiwa tukasome Tumeenda University tumepanda Kielimu kurudi kazini hakuna changes huu ni mwaka wa tatu. La ajabu wapo wenye Certifiate za 6months na uzoefu wa kazi ndio Meneja na wana mishahara minono. Haingii akilini mtu hana Digrii serikalini analipwa 3m,4m 5m 6m 7m 8m plus umeme, fuel, vocha na kodi ya nyumba japo anamiliki yake. Nashindwa kuelewa Utumishi wanawezaje kuridhia tofauti hii kwa pesa ya Serikali kuchotewa watu fulan nyingi na Wengine kiduchu. Mfano huu upo TPA. TRA na TanRoads kwa Staili hakuna haja ya kujipatia Digrii huku tukichekwa na Wenye Mishahara minono wasio na Digrii.
Ndo maana wizi unakithiri, thamani ya elimu haipokabisa
Tukitegemea wenye digirii wafikirie zaidi kujiajiri lakini kumbe wanatamani mishahara minono. Hulku wamachinga akianza na bishara kwa mtaji wa sh.10000 na wanafanikiwa! Certificate na digri zinazidiana kulingana na aina ya kazi. Sas kama anahitajika fundi wa umeme yuke mwenye digri ya mambo ya umeme ataachwa kwn atakua hana tija.sa kwa walimu shule za kata wenye vidigrii wataiba nini chaki?
sa kwa walimu shule za kata wenye vidigrii wataiba nini chaki?
Wanajf tulidai Salary. Vyeo vipande tukaambiwa tukasome Tumeenda University tumepanda Kielimu kurudi kazini hakuna changes huu ni mwaka wa tatu. La ajabu wapo wenye Certifiate za 6months na uzoefu wa kazi ndio Meneja na wana mishahara minono. Haingii akilini mtu hana Digrii serikalini analipwa 3m,4m 5m 6m 7m 8m plus umeme, fuel, vocha na kodi ya nyumba japo anamiliki yake. Nashindwa kuelewa Utumishi wanawezaje kuridhia tofauti hii kwa pesa ya Serikali kuchotewa watu fulan nyingi na Wengine kiduchu. Mfano huu upo TPA. TRA na TanRoads kwa Staili hakuna haja ya kujipatia Digrii huku tukichekwa na Wenye Mishahara minono wasio na Digrii.
unaweza ukawa na digrii lakini usijue kuitumia, itumie kuleta tija na ufanisi kazini uoneshe tofauti kati yako na mwenye cheti kiutendaji kisha uone matokeo yake!
sie wenzako huku tuna vidigrii mishahara yetu haizidi sh laki sita kwa mwezi, tumetulia tu ka mazuzu kumbe huko wenzetu wana neema ya ajabu hebe jaribu kuwapangua kwa staili hiyo ikishindikana rudi tena jamvini tuangalie namna ya kuwapandia hukohuko!
Ndiyo maana wenzio tulisoma tukiwa wadogo, hizo za open university na vyuo vingine vyaa ajabu ajabu ni kuboresha elimu yako ya kidato cha sita tuu, maana ulifanya mtihani wa kuchagua majibu na si kukokotoa
Kweli mdau hapo umenena kwani mabadiliko huwa hayaji mara moja, hata hao anaosema wana certificate huwezi kuwaondoa mara moja kwani pamoja na elimu yao walikuwa na mchango kwa hizo taasisi hivyo kinachotakiwa ni kuonyesha performance yako ili udhihirishe uwezo wako wa kazi mwisho wa siku utapanda. Ukisema tu mie nina degree basi hawa niliowakuta wana certificate waondoke mara moja sidhani kama kazi itafanyika maana hata yule mwenye degree anaetaka kuwaondoa hao kabla alikuwa anafanya bila degree.
Kitu cha kwanza ukiwa na elimu kubwa kuliko uliowakuta ni kujitahidi kusoma mazingira pia kujifunza based na uzoefu wao wa kazi hata kama umewazidi elimu kwani tunachosoma chuoni si kile ambacho tunakitumia mara nyingi kwa baadhi ya kazi na ndio maana inahitaji muda kidogo kuzoea mazingira ya kazi kabla ya kuanza kulalamikia vyeo na ndio maana walio sekta binafsi unakuta mkurugenzi ana degree na waliochini yake wamemzidi lakini kwa kuwa kuna sera madhubuti ya namna ya kufanya kazi unakuta malalamiko hakuna kwani kinachokuuza ni CV yako na uwezo wako kiutendaji. (ili upande onyesha kwamba unaweza) Tatizo staff wengi hasa serikalini focus yao ni vyeo na si utendaji na ukiona mtu kaenda kusoma ujue kichwani anawaza kuongezwa cheo na mshahara alafu performance ya kazi inakuja mwishoni kabisa (wakati vinatakiwa viende kwa pamoja)
Tatizo ni kwamba Thamani ya Elimu ya Juu kwa mfanyakazi wa serikali haionekani ikiwa wapo wasiokuwa na Elimu ya juu wanalipwa Vizuri na wana Vyeo Vikubwa . Sikatai kuwa Perfomance zao ni nzuri ila Thamani na Tofauti ya Elimu inaonekana wapi ili na wengine nao Wavutiwe Kujiendeleza?