Kuuzwa nyumba ya sanaa; kuna siku Ikulu itauzwa pia!

Mkerio

Member
Mar 12, 2006
35
0
Ndugu wana JF,
Nimesikitishwa sana na habari kuwa jumba la sanaa limehamishwa ili kupisha ujenzi wa gorofa ya kigogo mmoja ambaye alishawahi kuwa waziri mkuu. Jumba hili ni la muhimu sana na lipo tangia wakati wa mwalimu.

Inasikitisha kuona nchi inakwenda kishkaji kwa kufanya mambio kwa manufaa ya watu wachache. Wakati wa Mzee ruksa waliuza sana viwanja vya wazi nakumbuka hapo mnazi mmoja watu walivamia kuchukua mabati na matofali.

Tuwe shupavu pia kama serikali inauza mali ya umma kama hivi kuna siku watauza ikulu. Tungekataa na hata wakilazimisha tukavunje uzio pale. Nchi hii imefika mahali tutumie nguvu ya umma kidogo kupambana na wahuni wachache wanataka kujiuzia kila kitu.

Tanzania ipo mikononi kwetu tuilinde hata kama tutalipa gharama kidogo
 
Mkuu,

Naona litakuwa jambo jema sana kama tukiuza ikulu hakutakuwa na mwenye uchu wa kukimbilia pale. Kama wananchi wamelala basi wataendelea tu kuiba na sisi tutaendelea kulalama tu.

Hii ndiyo Tanzania.
 
Tumechoka na majungu. Bora tumlilie Remmy tu

Labda husomi magazeti kujua nyumba ya sanaa imeuzwa. Swala la majungu halipo na sina muda wa majungu. Magazeti sikumbuki ya lini ila kwa mfano soma The Citizen Friday, 10 December, 2010 page 9 utakuta mchambuzi Freddy Macha alivyochambua umuhimu wa Nyumba ya Sanaa na hatari za kuhamishwa kwake. Kwa hiyo uamuzi ulishafanywa sijui wewe unakaa wapi. Aya ya mwisho anasema hivi
" Closing down Nyumba ya Sanaa for whatever financial or political reasons is a typical example of how we black people run our businesses: short sighted, short term, clueless?"
 
Back
Top Bottom