Naomba wajuzi wa mambo mnisaidie kkufahamu hili, nilikuwa nasoma TANZANIA ROAD DISTANCE CHART IN KM - JUNE 2012 ambayo kwa bahati mbaya nimeshindwa kuattach kutokana na changamoto ya mtandao, nikakutana na kitu ambacho sijaelewa, naomba kuelekezwa;
- Nimetazama umbali wa Moshi hadi Morogoro ni Km 541, Umbali wa kutoka Morogoro hadi Mbeya ni Km 630 na Umbali wa kutoka Moshi hadi Mbeya ni Km 1100
- Nimetazama umbali wa Moshi hadi Iringa ni Km 769, Umbali wa kutoka Iringa hadi Songea ni Km 455 na Umbali wa kutoka Moshi hadi Songea ni Km 1224
Swali langu ni hapo namba 1 nilitegemea umbali wa kutoka Moshi hadi Mbeya ungekuwa 541+630=1171 na siyo 1100, na wengine mnaweza kutazama mikoa mingine.
Nawasilisha kwa msaada zaidi