TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,810
Kumemkuwepo na Misuguano ya Kisiasa nchini Tanzania, Kadhalika Mijadala Mikali ambayo imekuwa Ikitetea hasa Utawala Bora, Uwajibikaji, Haki na Demokrasia Nchini. Inasikitisha sana kwamba Kumekuwepo na Jitihada Kubwa sana za Kijidanganya Binafsi Kuwa Kwa Kuua Upinzani, CCM itaweza Kuongoza na Kutawala Nchi Vizuri.
Mimi Binafsi kwa Nafsi Ilioshawishika Kabisa, Kiongozi yeyote wa juu, ambaye kwa Makusudi Kabisa hatajenga Uhuru, Demokrasia, na Akajali zaidi Katika Kujenga Uchumi, Na Huduma za Jamii Peke yake, Atapata Sifa sana kwa Kitambo, Lakini itakuwa ni sawa na Mjenzi aliyejenga Jengo refu sana na Maridhawa, wakati wa Kipupwe lakini, kwa Kutumia Matofali ya Barafu, Watu wakalistaajabia, "Jengo zuri lililoje!" Na Lo mara Kiangazi chaja Na jengo likaangamia wala asijue mtu kuwa, liliwahi Kuwepo.
Mifano:-
1) Iraq ilikuwa Miaka ya 90, Ni Namba nne Duniani Kwa Nguvu za Kijeshi? Lakini Kwa Utawala Mbaya, Leo hii Taifa hili limeangamia na watu zaidi ya Milioni 4 wamepoteza maisha, Mwaka 2003 Nilikuwa Nikiongea na watu Nikiwa na Hasira sana Juu ya Vita ambavyo Havikuwa na sababu, Nikaropoka, "Look Iraq is doomed forever" Inatia huruma! Na ikumbukwe Iraq raia walikuwa wakipewa Mafuta ya Kupikia bure, Mchele bure, Makazi Bure, Afya Bure, Elimu bure nk, Lakini Tanzania ya CCM inajidanganya Kuwa Hitaji pekee la Taifa ni Huduma za Jamii na Uchumi, (Mimi nasema ni Mambo Mazuri but those items are not substitute for freedom and human rights)
2) Libya ilikuwa hali Kadhalika, Taifa Pekee Afrika lilokuwa na Nguvu ya Uchumi Afrika Kiasi cha Kuanzisha Benki ya Afrika ya Misaada. Qadaffi alikuwa Kiongozi aliyesaidia sana Wananchi wake, a)Elimu Bure, b)Makazi Bure, (3) Huduma za Afya Bure (4) Umeme, Maji etc bure, Hata Kijana akioa Qadaffi alikuwa akiwapa Waliooana Kianzio cha Maisha, Lakini Kutojali Kwake Uhuru na Demokrasia Kukatoa Mwanya Kwa Wahuni tu waliotaka shortcut za Madaraka Kuifikisha Libya Ilipo leo Failed State na Qadaffi Kufa Kifo cha huzuni sana, sanaa!
3) Syria Mambo Ni hayo hayo. Kila wakati Uhuru na haki zinapopuuzwa zinafikisha nchi mahali ambapo Mataifa yenye Nia ya Uovu yatatumia Mwanya Kushawishi wananchi Kuanza Kuchallenge utawala kwa Njia ambayo haitamaniki.
Labda Nitoe Utabiri wa Kisayansi Jamii Tu, Niseme Tanzania Itajifunza Kwa yatakayotokea Uganda within the next 3 to 4 years, Museven naye anajitahidi na Uchumi na Huduma za Jamii, Muda Mfupi sana kama hatafanya U turn, Uganda itarudi Kuwa ile nchi ya Miaka ya 1978-85 tuliyokuwa tunaililia. Amepewa fursa na Mungu, ameidharau na Kufikiri yu Mungu! Nisieleweke Vibaya, Namheshimu sana Rais Museveni, Lakini Ukweli Unabaki Ukweli, Asipotengeneza njia nzuri ya Utawala Uganda, Anakaribisha Uharibifu wa Kila alichotolea jasho au akiwa bado angalipo, Lakini Ni Uhakika kabisa Mungu amlinde, Lakini itokee aondoke Duniani Leo Kutazuka shida Kubwa Uganda!
Sina Haja ya Kutoa Mifano Mingi zaidi, inajulikana, Ila Swali langu Ni Kwamba, Kuna Tatizo Gani Kukawepo na, (1) Katiba Clean ya Utaifa Bila Kujali Maslahi ya Chama au Mtu Yeyote, (2) Tume Huru ya Uchaguzi (3) Vyombo vya Ulinzi Vinavyoheshimu Utu wa Mtanzania na Haki za Binaadamu, (4) Uchumi Mzuri (5) Huduma Bora za Jamii.
Kama Tukichagua Moja au Mawili Kati ya haya, Rais Yeyote Kutoka chama chochote hatapata Mafanikio yatakayodumu.
Finally may I say A great Leader does not cherish in appreciations and praises for what he do, but if his leadership, Ideas and the things he build will endure for generations!