Je, wewe ulitaka aolewe na nani? Ujue Mungu yupo katikati yao, hata bikra maria ilikuwa hvyohvyo kwa yosefu. Linaloshindikana kwa wanadamu kwa Mungu linawezekana. Heri yeye asiye na mashaka juu ya huyo mwanamke
Mi nadhani wewe mleta mada ndo mwenye mimba. Sasa uneleta jamvini tukujadili ili iweje. Hii inaitwa MIMBA SHIRIKISHI
Vp kuhusu mkaka alie mpa mimba maana na yeye anataka kumuoa?
sina shaka wewe unaona wivu, kama aliyempa mimba anataka kumwoa alikuwa wapi siku zote mpaka afikishe miez 7: wewe unamwona kinyaa wenzako wanasema watampata lini na ganda la mua la jana chungu kaona kivuno. Acheni kufuatlia maisha ya watu
Habari ya Jumamosi ndugu.
Kuna dada mmoja amepewa mimba na mpenzi wake (takribani miezi 7 ) Hivi sasa kapata mpenzi mwingine aliyeahidi kumuoa japokuwa ana mimba ya mtu mwingine.
Dada huyu ni mzuri wa kuvutia, ninachojiuliza, je ni kweli huyu kaka anataka kumuoa au anataka kumchezea.
Ushauri wenu wapendwa.