Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je, ni tatizo gani hili?

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,145
5,553

Kuna mshkaji wangu tunafanya naye kazi jana amekuja analalamika kuwa wakati akijisaidia haja kubwa anatokwa na damu. Sasa ameanza kupata wasiwasi kuwa anaweza kuwa na kansa ya njia ya haja kubwa.

Mimi kama mdau wa hapa ninapopaaminia naomba tumshauri huyu mshkaji wangu ili aepukane na janga hili. Yuko kwenye tension kwa kweli

Big Up Jf members kwa ushirikiano wenu

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
---
---
 
ICU,
HANA VIDONDA VYA TUMBO?
DAMU INAMTOKA KIVIPI? YAANI BAADA YA HAJA INAENDELEA KUTOKA INAKUWA KAMA HAJA NDIO IMEIFUNGUA ?AU IPO SAMBAMBA NA CHOO?
MHh HEMBU MUWAHISHE HOSPITALI.

LABDA Hemorrhoids ,au chochote cha kufikirika Aende Muhimbili kwanza au hospitali yoyote ya rufaa,.upesi hiyo sio dalili njema.
hima.


.
 
Sio LABDA Hemorrhoids, Hizo ni haemorroids asilimia kubwa sana ya watu wanazo hizo lakini huwa hawasemi hilo, huyo mshikaji wako ni mtu jasiri sana, aende Hospitali tu.
 
Asanteni Wakuu naomba kujua hii Hemorrhoids ni nini?

Hemorrhoids (also known as piles[1]) are part of the normal human anatomy of the anal canal. They become pathological when swollen or inflamed. In their physiological state they act as cushions composed of arterio-venous channels and connective tissue that aid the passage of stool.

The symptoms of pathological hemorrhoids depends on the type present. Internal hemorrhoids usually present with painless rectal bleeding while external hemorrhoids present with pain in the area of the anus.

Recommended treatment consists of increasing fiber intake, oral fluids to maintain hydration, NSAID analgesics, sitz baths, and rest. Surgery is reserved for those who fail to improve following these measures.
 
Asante Wenger

Naomba kujua kuna ukweli wowote baina ya hali hii na kupata kansa ya njia ya haja kubwa? manake ndio wasiwasi mkubwa wa mshkaji. Na kuna uhusiano gani na matatizo ya figo?
 
Asante sana Mkuu Clay, na wengine kwa michango yenu.............ila bado napokea ushauri zaidi wadau
 
Lakini hujasema kuwa hiyo damu inasababishwa na nini. Je tatizo lako ni kuwa una choo kigumu? (constipation) kiasi kwamba ukienda choonimpaka utoe machozi? kama jibu ni ndiyo basi kabla hujapata madhara zaidi ni bora ubadilishe aina ya hakula unachokula jaribu kula vyakula vya nafaka zizokobolewa kama ngano mtama, dona n.k. epuka vyakula vyenye mafuta mengi.

pia usizoee kula mila ya usiku sana, vile vile uwe unakunywa maji mengi kwa siku at least glass 8. kula matunda kwa wingi na pia usipendelee kuchanganya matunda na mboga za majani. ni vizuri matunda yawe na muda wake kabla ya mlo.

kwa kuanzia kutibu kabla ya kwenda hospitali kama tatizo ni choo kigumu tumia juisi ya Ukwaju nzito glass moja x 3 kwa siku. kama una vidonda vya tumbo basi tumia bamia mchemso au supu ya bamia kbala hujala chochote utaona mabadililiko. usipobadilisha mlo wako na pengine wa familia yako basi jiandae kufanyiwa operation za kukatwa nyamanyama zitakazokuwa zinaota huko chini kwa ajili ya hiyo shida.

By the way pole sana ndugu yangu.
 
Inategemea wengine inatokana na constipation imagine ana kama week hajapata haja kubwa as a result akina pata panakuwa hapatoshi .
Ilimpataga mdogo wangu diet ikawa ndo soln mapapai nk.
 
Inategemea wengine inatokana na constipation imagine ana kama week hajapata haja kubwa as a result akina pata panakuwa hapatoshi .
Ilimpataga mdogo wangu diet ikawa ndo soln mapapai nk.
Thanks Njowepo, nimeuchukua ushauri kama ulivyo na nitaupeleka
 
Hii bana ni case ya hospitali tu....
Ndicho kilichofanyika De Novo, jamaa kaenda hospital kapata dawa na anaendelea kutumia na ameanza kupata nafuu kubwa.

Ila kumbuka kitu kimoja hospitali pasipo kuwa na imani ya kupona ni sawa na bure na imani hiyo inapatikana kwa Mungu pekee katika Yesu Kristo
 
Maradhi ya kutokwa na Damu wakati wa kujisaidia haja kubwa kwa lugha ya utibabu inaitwa Hemorrhoids au kwa lugha ya kiswahili inaitwa (Bawasiri) atumie dawa hii huenda ikamsaidia sana apate Tangawizi mbichi au kavu kama gramu 25 achimshe na maziwa safi ya Ng'ombe glasi 2 na atie maji ya kawaida ndani ya hiyo dawa glasi moja achemshe pamoja ichemke mpaka ibaki glsai moja anywe hiyo dawa na afanye hiyo dawa kwa muda wa siku 7 .Na asipopona itabidi aende kwa doctor kufanya Operesheni ya upasuaji kwenye sehemu ya siri.

Na Maradhi ya
Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa yanatokana na ugonjwa wa kufunga choo kwa lugha ya kiingereza
Constipation Constipation also known as costiveness[1], dyschezia,[2] and dyssynergic defaecation[2] is a symptom[2] of infrequent hard to pass bowel movements.[2] Defecation may be painful, and in severe cases (fecal impaction) may lead to symptoms of bowel obstruction. The term obstipation describes severe constipation which prevents passage of both stool and gas. Causes of constipation can be dietary, hormonal, anatomical, side effects of medications (e.g., some opiates), and poisoning by heavy metals. Treatments may include changes in dietary

Source: Constipation - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Tuko field porini, rafiki yangu anatokwa na damu wakati wa kukojoa na wakati wa haja kubwa. Tumekwenda kwenye kituo cha afya wamechukua sample ya damu na wanasema majibu mpaka saa 12 jioni, na amechomwa sindano ya kutuliza maumivu. Naogopa kwa sababu kadiri muda unavyokwenda ndivyo jamaa yangu anazidi kunyong'onyea hasa wakati wa kwenda haja ndogo anaishiwa nguvu na anajisikia kama mwili wote unawaka moto. Kwa sasa tunafanya mawasiliano ili apelekwe kwenye hospitali kubwa. Naomba ushauri tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…