Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je ni tatizo gani hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je ni tatizo gani hili?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mokoyo, May 7, 2010.

 1. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kuna mshkaji wangu tunafanya naye kazi jana amekuja analalamika kuwa wakati akijisaidia haja kubwa anatokwa na damu. Sasa ameanza kupata wasiwasi kuwa anaweza kuwa na kansa ya njia ya haja kubwa.

  Mimi kama mdau wa hapa ninapopaaminia naomba tumshauri huyu mshkaji wangu ili aepukane na janga hili. Yuko kwenye tension kwa kweli

  Big Up Jf members kwa ushirikiano wenu
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  AWE ANAKULA MAPAPI KWA WINGI APATe CHOO LAINI
   
 3. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  HANA VIDONDA VYA TUMBO?
  DAMU INAMTOKA KIVIPI? YAANI BAADA YA HAJA INAENDELEA KUTOKA INAKUWA KAMA HAJA NDIO IMEIFUNGUA ?AU IPO SAMBAMBA NA CHOO?
  MHh HEMBU MUWAHISHE HOSPITALI.

  LABDA Hemorrhoids ,au chochote cha kufikirika Aende Muhimbili kwanza au hospitali yoyote ya rufaa,.upesi hiyo sio dalili njema.
  hima.


  .
   
 4. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #4
  May 7, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio LABDA Hemorrhoids, Hizo ni haemorroids asilimia kubwa sana ya watu wanazo hizo lakini huwa hawasemi hilo, huyo mshikaji wako ni mtu jasiri sana,aende Hospitali tu
   
 5. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Asanteni Wakuu naomba kujua hii Hemorrhoids ni nini?
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hemorrhoids (also known as piles[1]) are part of the normal human anatomy of the anal canal. They become pathological when swollen or inflamed. In their physiological state they act as cushions composed of arterio-venous channels and connective tissue that aid the passage of stool. The symptoms of pathological hemorrhoids depends on the type present. Internal hemorrhoids usually present with painless rectal bleeding while external hemorrhoids present with pain in the area of the anus.
  Recommended treatment consists of increasing fiber intake, oral fluids to maintain hydration, NSAID analgesics, sitz baths, and rest. Surgery is reserved for those who fail to improve following these measures.
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Asante Fidel
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Akamuone daktari apate vipimo zaidi hili hawe kwenye usalama zaidi wa afya yake.
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Asante Wenger

  Naomba kujua kuna ukweli wowote baina ya hali hii na kupata kansa ya njia ya haja kubwa? manake ndio wasiwasi mkubwa wa mshkaji. Na kuna uhusiano gani na matatizo ya figo?
   
 10. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna uhusiano wowote na kansa ya haja kubwa ni vitu tofauti kabisa kabisa,ingawa kansa ya njia hiyo INAWEZA kuja na dalili kama hiyo ,lakini hiyo sio kansa,kula bia yako
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu Clay, na wengine kwa michango yenu.............ila bado napokea ushauri zaidi wadau
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Haya ndugu Kituko, senks mhe
   
 13. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Lakini hujasema kuwa hiyo damu inasababishwa na nini. Je tatizo lako ni kuwa una choo kigumu? (constipation) kiasi kwamba ukienda choonimpaka utoe machozi? kama jibu ni ndiyo basi kabla hujapata madhara zaidi ni bora ubadilishe aina ya hakula unachokula jaribu kula vyakula vya nafaka zizokobolewa kama ngano mtama, dona n.k. epuka vyakula vyenye mafuta mengi.

  pia usizoee kula mila ya usiku sana, vile vile uwe unakunywa maji mengi kwa siku at least glass 8. kula matunda kwa wingi na pia usipendelee kuchanganya matunda na mboga za majani. ni vizuri matunda yawe na muda wake kabla ya mlo.

  kwa kuanzia kutibu kabla ya kwenda hospitali kama tatizo ni choo kigumu tumia juisi ya Ukwaju nzito glass moja x 3 kwa siku. kama una vidonda vya tumbo basi tumia bamia mchemso au supu ya bamia kbala hujala chochote utaona mabadililiko. usipobadilisha mlo wako na pengine wa familia yako basi jiandae kufanyiwa operation za kukatwa nyamanyama zitakazokuwa zinaota huko chini kwa ajili ya hiyo shida.

  By the way pole sana ndugu yangu.
   
 14. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Nimekupata CKABULA. Asante sana
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Inategemea wengine inatokana na constipation imagine ana kama week hajapata haja kubwa as a result akina pata panakuwa hapatoshi .
  Ilimpataga mdogo wangu diet ikawa ndo soln mapapai nk.
   
 16. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Thanks Njowepo, nimeuchukua ushauri kama ulivyo na nitaupeleka
   
 17. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  (haya ni maneno ya mshikaji wangu aliyenielezaga tatizo lake name kulifikisha hapa jukwaani na kumpatia ushauri, nimewasilisha tu)


  Salaam na Asante kwa JF Members
  Kwanza nianze kwa kumtukuza na kumwabudu Bwana Mungu katika jina takatifu la mwanaye Yesu Kristo aliye hai. Sina cha kumtolea Bwana zaidi ya kumshukuru yeye pekee kwa uweza wake ambao nimezidi kuuona katika maisha yangu siku hadi siku. Namshukuru Mungu pia kwa uwepo wenu kwani yeye ndiye aliyewaumba na kuwape akili, hekima na busara ambazo ndizo leo zimechangia kuandika haya niyaandikayo.
  Pili niwashukuru wale wote walionishauri katika kupata ufumbuzi wa ugonjwa ambao ulinisumbua kwa muda mrefu katika maisha yangu pasipo mie mwenyewe kutambua. Hakika nilivyoomba ushauri kwa rafiki yangu ambaye yeye ni Member wa jukwaa lenu ambalo mimi binafsi sio member alikuja na ushauri mkubwa sana na hakusita kuniambia kuwa ushauri huu umetoka Jamiiforums. Hakika nilishangaa sana na nilipoufatilia ndipo leo ninaweza kuandika kwa ujasiri kuwa nimepata matibabu ambayo kwakweli yananipa majibu ya kuridhisha sana ingawa bado sijamaliza lakini nimesema nimwambie rafiki yangu alete hizi salama za shukrani za awali maana mwenye nashangaa sana.
  Nisiwachoshe kwa maneno mengi maana najua nyie ni watu makini sana wenye kufikiri kwa dhati katika kuwasaidia wale wenye shida.
  Nawaomba wale ambao ni Wakristo kuimba nami wimbo huu "Mungu amenihurumia jambo hili"
  Asanteni sana
   
 18. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,822
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  (haya ni maneno ya mshikaji wangu aliyenielezaga tatizo lake name kulifikisha hapa jukwaani na kumpatia ushauri, nimewasilisha tu)


  Salaam na Asante kwa JF Members
  Kwanza nianze kwa kumtukuza na kumwabudu Bwana Mungu katika jina takatifu la mwanaye Yesu Kristo aliye hai. Sina cha kumtolea Bwana zaidi ya kumshukuru yeye pekee kwa uweza wake ambao nimezidi kuuona katika maisha yangu siku hadi siku. Namshukuru Mungu pia kwa uwepo wenu kwani yeye ndiye aliyewaumba na kuwape akili, hekima na busara ambazo ndizo leo zimechangia kuandika haya niyaandikayo.
  Pili niwashukuru wale wote walionishauri katika kupata ufumbuzi wa ugonjwa ambao ulinisumbua kwa muda mrefu katika maisha yangu pasipo mie mwenyewe kutambua. Hakika nilivyoomba ushauri kwa rafiki yangu ambaye yeye ni Member wa jukwaa lenu ambalo mimi binafsi sio member alikuja na ushauri mkubwa sana na hakusita kuniambia kuwa ushauri huu umetoka Jamiiforums. Hakika nilishangaa sana na nilipoufatilia ndipo leo ninaweza kuandika kwa ujasiri kuwa nimepata matibabu ambayo kwakweli yananipa majibu ya kuridhisha sana ingawa bado sijamaliza lakini nimesema nimwambie rafiki yangu alete hizi salama za shukrani za awali maana mwenye nashangaa sana.
  Nisiwachoshe kwa maneno mengi maana najua nyie ni watu makini sana wenye kufikiri kwa dhati katika kuwasaidia wale wenye shida.
  Nawaomba wale ambao ni Wakristo kuimba nami wimbo huu “Mungu amenihurumia jambo hili”
  Asanteni sana
   
 19. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Copy and paste!:A S-eek:

  Source: http://wapedia.mobi/en/Hemorrhoids
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hii bana ni case ya hospitali tu....
   
Loading...