Kutoka Olasiti - Arusha: Mazishi ya Marehemu wahanga wa Mlipuko na yaliyojiri

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Misa ya Mazishi ya wahanga wa mlipuko wa Jumapili iliyopita kwenye parokia teule ya Olasiti imeanza katika eneo lile lile mlipuko ulipotokea.

Misa inaongozwa na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu wa Dar es Salaam.

Maandamano yalianzia toka chumba cha kuhifadhia maiti, miili ikapelekwa makao makuu ya Asofu Mkuu, Burka. Hivi sasa imeshawasili kanisani na Askofu Mkuu Lebulu amesali sala ya kuipokea miili kanisani.

Askofu Mkuu amemaliza sala hiyo, kuna wimbo wa maombolezo unaimbwa kwa sasa.

Askofu amemaliza kubariki maji.

Wanaopenda kufuata live bonyeza link hii: Radio Maria Tanzania - FM 89.1 - Dar es Salaam - Streema Player

======================================
Updates
======================================

Mahubiri ya Kardinali Pengo

Ndugu zangu,

Nafasi hii inaunganisha mawazo ya furaha na uchungu kutokana na kilichotukutanisha leo.

Mazingira haya yanaweka ugumu wa kupata cha kusema. Ila sisi ni watu wa imani. napenda kueleza imani yetu kama tunavyopaswa kuwa kwenye mazingira haya.

Tumejumuika ili kuwaweka kwenye nyumba ya milele hawa marehemu, lakini pia tunatumia nafasi hii kubariki Kanisa.

Kila mbatizwa ni kiungo cha mwili wa Kanisa. Kila kiungo cha mwili kinapaswa kuungana na kichwa cha Mwili ambae ni Yesu Mwenyewe

Kristo akipitia kwa mdomo wa mtume Paulo anatufundisha kuwa "Msijaribu kushindana na uovu kwa uovu, lakini shindeni uovu kwa wema".

Katika viongozi waanzilishi wa dini, ni Yesu peke yake aliyetolea uhai wake kujenga imani ya wafuasi wake. Viongozi wengine hawajikutoa sadaka wenyewe, na baadhi wametoa sadaka ya maisha ya watu wengine kwa ajili ya kueneza imani yao.

Sisi Wakristu
Imani yetu inajengwa juu ya mwanzilishi wetu ambaye alitoa uhai wake ili kujenga imani yetu, na hakutoa uhai wa mtu yeyote kwa ajili ya kujenga imani yetu.

Katika masomo tuliyosikia leo, Somo la plili limetupa neno la Mtume Paulo Rum:12:17 linasisitiza hilo: usishinde uovu kwa uovu, bali shinda uovu kwa wema.

Soma la Kwanza limeeleza kuwa Paulo na Sila wanateswa kwa ubaya mkubwa sana na kuwekwa gerezani kwa ubaya. Na baada ya kufunguliwa kwa muujiza, askari wa magereza alitaka kujiua, lakini Paulo na Sila wakatenda lililo jema kuokoa maisha yake. Ni baada ya wema huo wokovu ulifika kwa askari huyo na jamaa yake yote wakaweza kumwamini Mungu.

Nawauliza waumini: "
Wale waliotekeleza ubaya huu, akija mbele yetu akasema ni mimi ndiye, tungefanya nini kama waumini kwa kufuata mfano wa Yesu?"

Mimi nawaambia
"Tujifunze kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo: 'Tusidiriki kulipia uovu kwa uovu, lakini tutende mema ili kushinda uovu'."

Lakini haya hayaondoi majukumu ya serikali, ambayo yanabaki, na si mimi ninayepaswa kuyasema, wenye mamlaka wanayajua majukumu yao. Mimi nawaambia ninyi waumini.

Uovu si kitu kinachopendeza. Warumi waliwatesa wakristo kwa karne tatu, na haikusaidia chochote Himaya ya Warumi, ambayo baadaye ilisambaratika. Lakini imani yetu imebaki.

Amemalizia kwa kusema:
Tukio hili na tukio la mauaji ya Padre Mushi, isiwe sababu ya kuacha amani ya nchi yetu isambaratike.

Lakini ni jukumu la wananchi wotte kuhakikisha nchi yetu haisambaratiki.

Wenye mamlaka watimize wajibu wao. Sisi wakristo tusamehe, tusijibu uovu, tudumishe amani na upendo katika taifa letu.

Tumsifu Yesu Kristu.

==================
Update Neno la Askofu Malasusa
==================
Tunaagana na ndugu zetu katika mwili.

Ni ibada yenye majonzi lakini ni yenye furaha kwa kuwa ndugu zetu wamelala katika imani na wataupata uzima wa milele.

Natoa pole kwa wafiwa na kwa Baba Askofu Lebulu.

Yesu yu hai nasi tunaomwamini tutakuwa hai, hata miili itakapoharibika, tutaurithi uzima wa milele.

Kama alivyosema Kardinali tusilipe ubaya kwa ubaya, lakini tusiwe waoga. Tumtangaze bila woga. Tuelewe pia kuwa hatutahukumiwa tu kwa maovu tuliyotenda bali hata kwa mema ambayo hatukuyatenda

Risasi wanazopigwa watumishi wa Mungu, mioto ya kuchoma makanisa, mabomu wanayotupiwa waumini, yasitukatishe tamaa.

Askofu Malasusa anaseama pia: Anatamani kama angefariki katika ibada kama marehemu hawa. Heri wafu wafao katika Bwana.

==================
Update: Salamu za Waziri Mkuu
==================

Ni siku ya majonzi, lakini ni siku ya kuwaombea ndugu zetu marehemu.

Tukio hilo limetokea, tuwaombee ndugu zetu marehemu.

Kwa niaba ya Rais na serikali yote, nawapa pole, naungana na wafiwa na kuwaomba wajitahidi kubeba msiba huu.

Anawapa pole waumini wa Olasiti. Tukio limetokea katika mazingira yasiyotarajiwa. Waliokuwepo tukio hilo limewashtua na bila shaka litabaki.

Anamshukuru Baba Paroko. Alipomtembelea alifarijika kwa maneno yake ambayo leo yamesemwa tena na Kardinali.

Anatoa pole kwa Baba Askofu Mkuu Josephat Lebulu, Mungu ampe nguvu ya kuendelea kuongoza waamini.

Kwa Mwadhama Kardinali, pole tena. Kwa kuwa jambo hili limetokea katika kanisa katoliki.

Anawaombea viongozi wote wa dini wasikate tamaa.

Anasema kuwa ni kujidanganya kudhani kuwa ukiua muumini mmoja utaua ukristu, Haitawezekana.

Hawa waovu wachache, serikali tutawasaka na kuchukua hatua za kisheria. wanajua kuwa kwa hatua ya sasa, hawataweza kufuta ukristo kwa njia hiyo.

Ukristo na uislamu zina historia ndefu. Tutajidanganya kuwa mufti akiuawa ukristo utauliwa.

Serikali itashugulikia kikamilifu kundi ambalo lengo lao ni kuharibu amani yetu Tanzania. Wanataka tushindwa kuishi kwa amani. tusikubali tufikie hapo.

Anasema tumeagiza vyombo vyote husika vifanye kazi kuhakikisha utulivu na amani vinaendeleza. kamata kamata zitaongezeka. Lakini ni kwa kuondoa hali hii inayotishia usalama wetu.

Anaomba ushirikiano wa wananchi wote. Waovu wako miongoni mwetu.

Tutaisaidia sana serikali tukiwajulisha waovu hao. Ametoa rambi rambi Sh 100 milioni.

====================================
Update: Neno la Shukrani toka Askofu Mkuu Lebulu
====================================
Kwa niaba ya mapade, watawa, walei wote alitoa pole kwa familia ya kanisa la Arusha.

Kwa msiba huu anasema Wakristu tunajiuliza Mungu una ujumbe gani kwetu?

Alitoa pole, kwa ndugu za marehemu watatu. Alitoa pole kwa wafiwa na kusema hakika tumeguswa sana na hata hatuna maneno ya kuelezea, tuliwatembelea mahospitalini na hakika watu wa Mungu wameumizwa sana. Pole sana kwa waumini wa kanisa hili na wakaazi wa eneo hili. Alisisitiza Tusikate tamaa!

Alitoa pole kwa wanafamilia ya Mungu wa Olasiti waliokuwa kwenye siku yao ya furaha ya kufungua parokia yao.

Alitambua majitoleo waliyofanya wana Olasiti kwa kumjengea Mungu nyumba. Walijenga nyumba ya Mungu kwa nguvu zao bila ufadhili toka nje. Wakati wanataka kumtolea Mungu shukrani zao wamekatishwa, lakini hakuna kukata tamaa.

Alitoa shukrani kwa wale walioonesha moyo wa utu kulaani unyama ule.

Aliishukuru serikali ya wilaya, mkoa na serikali kuu waliokuwa pamoja katika msiba huu. Na anamshukuru Waziri mkuu kwa uwepo.

Anashukuru na Serikali ya Zanzibar kwa moyo wa utu, kwamba walimtembelea na waliwafariji wakristo wote wa Arusha.

Aliwaambia waumini Msiogope! Kristo akiwa upande wetu hakuna atakayetushinda.

Kristo ametuambia katika Injili ya Yohane: Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Yesu aliwaambia pia Msiogope. Mkijua mafundisho yangu, mtaujua ukweli na ukweli utawaweka huru.

Anasema yeye kama baba anawaambia, lazima ifikie mahali tuseme INATOSHA, Tumwambie Mungu IMETOSHA. Wenye nguvu na silaha watatushinda, lakini tukiwa na Mungu hatutashindwa. Paulo na Sila walisali Milango ya gereza ikafunguka.

Tusali kwa nguvu zote.

Alimaliza kwa kuwaaga marehemu akiwataja kwa majina na kumwambia kila mmoja kwa heri!

================






Mapadre wa Arusha wakiwa wamebeba jeneza la mtoto Patricia.



Mapadre wakiwa wamebeba jeneza la mama Regina Laizer


Mapadre na Maaskofu mbele ya majeneza yaliyobeba miili ya marehemu wakati Askofu Lebulu anayabariki mara baada ya kuingia kanisani.



Askofu Lebulu akiwa ananyunyizia maji ya Baraka. Kulia ni Paroko wa Parokia hiyo. Kushoto kabisa ni Maaskofu Amani, Askofu Nkwande, Askofu Dallu, na aliyeshika fimbo yenye msalaba Kardinali Pengo.



Kardinali Pengo akisali sala, pamoja na Askofu Mkuu Josephat Lebulu



 
Kardinali Pengo ameanza kusali sala maalum.

Raha ya milele uwape ee Bwana, na Mwanga wa milele uwaangazie.
 
Sala mlangoni mwa kanisa imekamilika iliyoongozwa na Kardinali Pengo. Sasa miili inabebwa kuingizwa kanisani.

Maaskofu wengine waliopo ni Askofu Tarcisius Ngalalekumtw ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Askofu Renatus Nkwande wa Jimbo la Bunda, Askofu Damian Dallu wa Geita, Askofu Rogath Kimario wa Same, Askofu Anthony Banzi na Askofu Isaac Amani wa Jimbo la Moshi.
 
Wana jamvi, leo ni siku ya mazishi ya wale waliofariki kwa mliouko wa bomu, waru ni wengi sana ulinzi ni mkali zana ibada inaongozwa na Mhadhama Polipecap Pengo.
Nitashindwa kutoa picha kwani wstu ni wengi sana. Nitatoa matukio jinsi tunavyoendelea.
kanisa limesha barikiwa
Sasa marehemu ndo wanaungizwa ndani wako watatu.
Mama mmola, wanafunzi wawili, mmoka form one na mmoja darasa la sita.
 

Tunakushukuru kwa taarifa ila picha ni muhimu sana jitahidi
 

Mungu azilaze pema peponi roho za marehemu.
Lakini naona uongozi wa juu wa serikari pamoja na Bunge letu wametumia tukio hili kama nafasi ya kuzoa allowances. Naangalia misafara ya kwenda kuudhuria misa na mazishi. Watalipwa ngapi mpaka shughuli hii ikimalizika?
 
Wamemaliza kuimba Utukufu kwa Mungu juu.

Kardinali Pengo amesali sala ya Mwanzo ya Misa (Collect). Watu wanakaa kusikia neno la Mungu.

Somo la kwanza toka Matendo ya mitume: Matendo: 16:22-34.
 
Somo linazungumzia jinsi Paulo na Sila walivyotolewa Gerezani kwa miujiza baada ya kufungwa kwa udhalimu kwa ajili ya imani yao.

Tukio hilo liliwaongoa maaskari wa Gereza.

Paulo alimwambia Mkuu wa Gereza: mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka wewe na jamaa yako yote.

Mkuu wa gereza aliongoka na jamaa yake.

Somo limesomwa na Felician Mtei.
 
Inauma sana kwa kweli tumepoteza watu muhimu sana lol watoto hao mungu wangu
 
Somo la Pili linasomwa na Sista Advera Laizer toka Waraka wa Mtume Paulo kwa warumi 16: 9-12.

Somo linasema waumini wawe na furaha daima wanapopatwa na majaribu.
 
Mungu awatie nguvu na kuwafariji wafiwa na wote mliko huko kwenye msiba huu mzito'poleni'
 
Injili inasomwa Yoh: 14:1-14

Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu niaminini na Mimi. Nyumbani kwa Baba kuna makao mengi ila sivyo ningewaambia.....


.... Mimi ndiye njia na ukweli na uzima, mtu haji kwa baba ila kwa njia yangu...


.. aliyeniona mimi amemwona Baba

.... Anayeniamini atafanya ninayofanya mimi, na makubwa zaidi atafanya.

Mkiniomba lolote nitafanya.

Injili imesomwa na Padre Ciril Molel,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…