Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Kama Wapinzani wana nia ya kushika Dola 2055, itabidi wajiandae kwelikweli kuwapata Viongozi Vijana wenye maono mapya badala ya kusubiria walioachwa na CCM ambao hawana Sera Mbadala wala nia ya kutumikia Nchi badala ya kutumikia Nyadhifa tu! Ni aibu kwa Chama Kikongwe cha Upinzani kufanya Siasa za ubabaishaji kwa kutoandaa Mgombea na kusubiri mtu akatwe na CCM!
Hakika kama hatutaambiwa Sera mbadala ya nini anakuja kufanya Mgombea wa Upinzani tofauti na kinachofanywa na CCM ni bora kuendelea kuipigia CCM milele kuliko kufanya majaribio ya Utawala na Mtu kupata Urais tu, badala ya Urais kupata MTU! Kwa mazingira ya 2015 na tuendako, Wapinzani bado hawana mtu mwenye sifa ya kutumikia Nchi badala ya kutumikia Wadhifa wa Urais tu! UKWELI MCHUNGU SANA HUU. LAZIMA KUUMEZA HIVYO HIVYO!!