Dah! Hujawa mkweli kaka, labda kama yeye tayari ni developer wa lugha nyingine ndio iwe rahisi na kumchukua muda mfupi kiasi hiki, Pyhton 2 weeks??? Mimi hapa kipindi najifunza Pyhton nilitokea kwenye lugha zingine ila ilinichukua several months.
Mleta mada kwa ushauri wangu acha kujipangia muda, haya madude ukipanga muda utayachoka, kwanza kabisa hamna jinsi unaweza ukasoma language yoyote na kuimaliza, mimi hapa nina miaka kumi kwenye fani hii na sina lugha hata moja niliwahi kusema nimeimaliza, chukulia kama way of life, kitu cha kufanya kila siku, jitose humo humo na kuanza kuzisoma, kwa mfano nenda kwenye website ya W3schools hakikisha umefanya exercise zote humo kwenye website yao, usipende copy pasting, uwe unaandika mwenyewe.
Pia hakikisha kwa kila lugha unayopitia, kuna vitu vya msingi unavifahamu moyoni, yaani hata ukiamshwa kwa vibao utaziandika muda wowote. Hiyo ina maana uwe unafanya practice kila siku. Binafsi huwa najipa dk 15 kwa kila lugha ambayo ipo kwenye kapu langu, kujikumbushia na kujiongezea chochote humo, hivyo kila siku masaa matatu huishia kwenye kusoma na kutafiti kisha ndio ninaanza kazi zangu za kawaida.