Kusoma ni kuishi

Kusoma ni kuishi

Emmaloy

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Posts
216
Reaction score
231
KUSOMA NI KUISHI

Maisha ya kila binadamu yeyote yanategemea na namna siku yake inavyoisha. Mwanafunzi wa Tanzania anahitaji takribani miaka 23 hadi 28 ya kukaa darasani ili kuweza kuhitimu masomo yake ya kuanzia nursery hadi shahada ya kwanza (Degree/Bachelor). Sishangazwi na uwingi wa miaka tunayoitumia ila kitu cha msingi ni kutambua thamani ya kitu tunachokisoma pamoja namna ya kuishi wakati wa masomo. Maisha hayahitaji mbwembwe, acha kukaa na kubweteka kuwa, eti utaanza kujipanga na kuishi baada ya kumaliza masomo(chuo). Amka, panga njia stahiki na zenye mvuto zitakazokufanya uishi maisha mazuri baada ya kumaliza kusoma kwani muda ndo huu.Time the time before the time times you, kumbuka TIME MANAGEMENT IS LIFE MANAGEMENT.

Kijana anaejituma atakuwa na mkono mtiifu wenye shabaha ya kuyalenga mafanikio ili aweze kupata maisha bora yenye amani. Elimu ina manufaa pale inapotumika kututatulia changamoto ulizonazo, ni vyema kuanza kuishi mapema kipindi cha masomo kuliko kusubiri kuhitimu masomo ndipo uanze kujipanga, kama bado una mawazo jiandae kwa msongo wa mawazo huko mbeleni..FUTURE NI LEO. Nasisitiza pia, waambieni vijana wasome prepo sio club bali ni mahali pa kufanyia good preparation za masomo.

Emmaloy PF

2017..Maisha ya baadae hayaangalii baadae..✍
 
Back
Top Bottom