Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Stendi ya Mawasiliano ni eneo lenye muingiliano mkubwa wa watu kutokana na uwepo wa soko pamoja na mabanda mengi ya biashara. Licha ya umuhimu mkubwa wa eneo hilo, upatikanaji wa huduma ya choo kwa sasa ni changamoto kubwa, hali inayosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara, wananchi wanaofika sokoni, pamoja na abiria.
Nilipofika eneo la soko, nilishuhudia baadhi ya watu wakilazimika kujisitiri haja ndogo nyuma ya jengo la choo, kwenye majani. Nilipouliza sababu ya kutotumia vyoo vilivyopo ndani, niliambiwa kuwa vyoo hivyo vimefungwa kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa madai ya kufanyiwa marekebisho.
Baada ya kufuatilia zaidi, niliona tangazo dogo la karatasi lililobandikwa kwenye mlango wa choo likieleza kuwa vyoo hivyo vimefungwa kupisha ukarabati, na kwamba wananchi watumie vyoo vilivyopo katika stendi ya zamani.
Hata hivyo, kwa mazingira halisi, vyoo vya stendi ya zamani vipo mbali na eneo la soko, jambo linalolalamikiwa na watu wengi hususan wanawake. Hali hii inawalazimu baadhi ya wananchi kutumia maeneo yasiyo rasmi kama mbadala wa choo, jambo linalohatarisha afya na mazingira.
Kinachozidi kuwashangaza wananchi ni kwamba, licha ya madai ya ukarabati, hakuna dalili zozote za uboreshaji au kazi zinazoendelea katika eneo hilo kama jitihada za kurejesha huduma hiyo muhimu kwa jamii.
Kutokana na hali niliyoiona, kuna dalili za uzembe na kutokuwajibika kwa baadhi ya watendaji husika. Hivyo nitoe wito kwa Manispaa ya Ubungo kuhakikisha huduma za choo zinarejeshwa kwa haraka. Endapo kuna maboresho yanayohitajika kufanyika, basi jitihada za dhati na za haraka zichukuliwe ili kuondoa kero hii inayowaathiri wananchi kwa muda mrefu.
Pia soma
~ Manispaa ya Ubungo: Vyoo viwili eneo la Stendi ya Simu 2000 vimesitishwa kwa muda kutokana na changamoto ya kujaa maji mara kwa mara
~ Kero: Vyoo vya Simu 2000 ni vichafu sana